Saturday, 12 July 2014

MAMBO YA KUYAFAHAMU JUU YA MARADHI YA KANSA (CANCER)


1. 
Kuna zaidi ya aina 100 za saratani,na kiungo chochote cha mwili kinaweza
kuathirika

2. Asilimia 70 ya vifo hutokea katika nchi zenye kipato kidogo na cha kati
                        
3. Aina 5 za  kansa zinazosababisha vifo  duniani kote ni : mapafu, tumbo, ini, utumbo mpana na koo
                            
4. Matumizi ya tumbaku ni mojawapo ya sababu kubwa  inayosababisha  kansa duniani ambayo huzuilika   na husababisha 22% ya vifo ya vyote vya kansa                           
5. Moja ya tano ya saratani duniani kote yanatokana na maambukizi sugu, kwa mfano human papillomavirus (HPV) husababisha kansa ya kizazi na hepatitis B virusi (HBV) husababisha kansa ya ini.
                             
6. Baadhi ya Saratani  mfano matiti, kizazi na kansa ya utumbo mpana zinaweza kutibiwa na kupona  kama zitagundulika mapema na kutibiwa vya kutosha.
                                 
7. Wagonjwa wote wenye haja ya kutuliza maumivu wanaweza kusaidiwa kama elimu ya sasa kuhusu kudhibiti maumivu  na huduma ya  faraja itatumiwa kikamilifu
                                 
8. Zaidi ya 30% ya kansa zinaweza kuzuiwa, hasa kwa kuacha kutumia tumbaku,  lishe bora , kufanya mazoezi na  kudhibiti matumizi ya pombe. Katika nchi zinazoendelea hadi 20% ya vifo vya kansa yanaweza kuzuilika kwa chanjo dhidi ya maambukizi ya HBV na HPV.

0 comments:

Post a Comment