Friday 24 April 2020

RAIS WA MADAGASCAR ATANGAZA KUWA MADAGASCAR IMEGUNDUA TIBA YA CORONA: WHO YAPINGA VIKALI DAWA HIYO

RAIS WA MADAGASCAR ATANGAZA KUWA MADAGASCAR 
IMEGUNDUA TIBA YA CORONA: WHO YAPINGA VIKALI DAWA HIYO

Wakati wanasayansi duniani wakihangaika kupata chanjo na tiba ya virusi vya corona, Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amezindua dawa ya mitishamba inayotibu' COVID-19.

Hata hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) na Marekani wamepinga vikali tiba  hiyo ya COVID-19 baada ya Rais Rajoelina kutangaza dawa hiyo. WHO na Marekani imeitaka Madagascar kukoma kuendelea na matumizi ya dawa hiyo mara moja na endapo itakaidi kuacha matumizi ya dawa hiyo huenda Shirika hilo la Afya Duniani na Marekani zikalazimika kutoipatia msaada zaidi wa kupambana na janga la Corona.

Taasisi ya taifa ya tiba nchini Madagascar (Anamem) pia imepinga matumizi ya dawa hiyo inayoelezewa na Rais Andry Rajoelina kama yenye uwezo wa kuzuia na kuponyesha corona.

Taasisi hiyo imesema kuwa mitishamba inaweza kudhuru afya ya mtu kwani "hakuna ushahidi wa ufanisi wake kisayansi".

Mmea huo unatarajiwa kutolewa bure kwa watu wenye uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na na virusi vya corona.

Ikizinduliwa kwa jina Covid-Organics, dawa hiyo imetengenezwa kutoka kwa mmea artemisia (pakanga) ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria. Mmea huo ni tiba maarufu ya malaria nchini Madagascar na kwa muda mrefu umetumika kutibu malaria kwa mafanikio makubwa.

Dawa hiyo imepakiwa kwenye chupa na kutangazwa kama chai ya miti shamba baada ya kujaribiwa kwa watu 20 kwa kipindi cha wiki tatu, katibu wa Rais Lova Hasinirina Ranoromaro ameiambia BBC.

Baada ya janga la Corona kutangazwa duniani, Rais aliwataka watafiti kuja na tiba ambayo kwa bahati nzuri 'waliipata kwamuda muafaka'.

"Vipimo vimefanyika na tayari wagonjwa wawili wa COVID-19 wamekwishapona kutokana na tiba hii," Bwana Rajoelina alisema katika uzinduzi wa Covid-Organics uliofanyika katika taasisi ya utafiti ya Madagascar- Malagasy Institute of Applied Research (Imra), ambayo ndiyo iliyotengeneza dawa hiyo ya mitishamba.

"Kinywaji cha dawa hii ya mitishamba huonesha matokeo katika kipindi siku saba," alisema Rais huyo mwenye umri wa miaka 45, ambaye aliwataka watu kuitumia kama hatua ya kujikinga na kujitibu ugonjwa wa corona.

Dkt Charles Andrianjara, Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti ya Imra, anaafiki kuwa Covid-Organics inapaswa kutumiwa kama kinga.
Lakini alijihadhari zaidi kuzungumzia zaidi juu ya matumizi ya dawa hiyo kama tiba, lakini akasema kwamba uchunguzi wa kimatibabu umeonyesha "dalili ya ufanisi wake kama tiba", shirika la habari la AFP lilimnukuu akisema.

Kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi kimekwisharekodi hadi sasa wagonjwa 121 wa virusi vya corona, na hakuna vifo kutokana na ugonjwa huo hadi sasa.

WHO YAPINGA DAWA HIYO, YASEMA 'HAKUNA NJIA ZA MKATO'

Ikizungungumzia uzinduzi wa Covid-Organics, WHO imeambia BBC kwamba shirika hilo la dunia halishauri "matibabu ya kibinafsi ya dawa zozote... kama njia ya kinga au tiba ya Covid-19."

Lilirejelea kauli za mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ambaye ni raia wa Ethiopia kwamba "hakuna njia za mkato" za kutafuta dawa ya kupambana na virusi vya corona. Majaribio ya kimataifa yanaendelea kupata tiba yenye ufanisi , WHO iliongeza.

Swali ni Je, kwa nini Marekani na WHO hawaamini kwamba kinga na tiba ya Corona Virus inaweza kupatikana Africa?

Nini maoni yako?

Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti

2 comments:

  1. I am FRED and i want quickly recommend DR NCUBE for a Job well done by
    curing me from the genital herpes disease that have be giving me sleepless night. if you want to contact him, Simply do that via email drncube03@gmail.com or 
    call/whatsapp +2348155227532
    he also have #herbs for
    #hiv/aids
    #cancerdisease 
    #fibroid 
    #diabetes

    ReplyDelete
  2. Am Lisa by name, i was diagnosed with Herpes for 3years ago i lived in pain with the knowledge that i wasn't going to ever be well again i contacted so many herbal doctors on this issue and wasted a large sum of money but my. condition never got better i was determined to get my life back so one day i saw mr Brown post on how Dr Aba saved him from the VIRUS with herbal medicine i contacted Dr Aba on his email address dr.abaherbalhome@gmail.com we spoke on the issue i told him all that i went through and he told me not to worry that everything will be fine again so he prepared the medicine and send it to me through courier service and told me how to use it,after 14days of usage I went to see the doctor for test ,then the result was negative,am the happiest woman on earth now. this testimony is real.thanks to Dr Aba God bless you. you can also reach him on his whatsApp number +2348107155060   

    ReplyDelete