Tuesday, 4 September 2018

PSYCHOLOGY: SAIKOLOJIA DALILI 7 KUWA MKEO ANAHITAJI UMSIKILIZE




PSYCHOLOGY: SAIKOLOJIA DALILI  7 KUWA MKEO ANAHITAJI UMSIKILIZE
Wakati fulani kitu pekee ambacho mwanamke anakihitaji ni mtu wa kumsikiliza. Njia maridhawa ya kumsaidia mkeo katika
matatizo yake, kwanza ni kumsikiliza na kumakinika kwa anachosema kisha utoe maoni yako juu ya suluhisho la tatizo husika iwapo ataomba ufanye hivyo.
Iwapo hutambui ujumbe ambao mkeo anajaribu kuutuma, basi Famasia ya Ndoa Maridhawa inakuletea ishara saba za wazi zinazoonesha kuwa mkeo anahitaji sana umsikilize:

1. ANAPOONESHA TABASAMU AMBALO SIO HALISI:
Mwanamke anayeweza kutabasamu hali ya kuwa hajisikii vizuri, basi huyo ni mwanamke madhubuti, lakini bado anahitaji faraja yako. Mkumbatie na umuombe afunguke.
2. IWAPO SIKU NZIMA ALIKUWA PEKE YAKE NA WATOTO
Anahitaji kupata mazungumzo ya mtu mzima. Kama ni mama wa nyumbani, bila shaka atakachokuwa akikisikia kwa siku nzima ni makelele ya watoto, vilio vyao na sauti za vipindi vya katuni. Unaporudi nyumbani muulize kuhusu siku yake ilivyokuwa ili kumpa mazungumzo ya kiutu-uzima ambayo alikuwa na shauku nayo kwa kutwa nzima.
3. ANAPOKUWA KIMYA KULIKO KAWAIDA
Anapokuwa na ukimya usiokuwa wa kawaida, anaweza kuwa na hasira au msongo. Mkumbatie na umuulize kinachoendelea akilini mwake.

4. ANAPOSEMA KWA HASIRA "SAWA"
Iwapo uko kwenye ndoa kwa muda mrefu au unazifahamu silika za wanawake, anaposema "sawa" yaweza kumaanisha "sio sawa". Yumkini tatizo lisionekane, lakini huhitaji kuchimbua kutafuta mzizi wa tatizo. Muulize tu mambo gani hayako sawa na namna unavyoweza kusaidia kuyaweka sawa. Atapenda sana kuona kuwa unajali sana hisia zake.

5. ANAPOKUWA KATIKA MOOD NZURI
Anataka umsikilize anapokuwa na furaha kwa kiwango kilekile anachotaka umsikilize anapokuwa na huzuni. Muulize kuhusu siku yake ilivyokuwa. Yumkini anatamani kukupa habari njema.

6. ANAPOCHOSHWA NA MAJUKUMU YA KUTWA NZIMA
Tengeneza utayari wa kumsikiliza pindi anapokuwa na siku iliyojaa majukumu kayaya. Mkumbushe namna unavyothamini yote anayoyafanya kwa ajili yako na familia yenu pia. Hatua hii maridhawa itamthibitishia kuwa yote anayoyafanya yanaonekana na kumpa hamasa ya kuendelea kufanya mambo mazuri na kujituma zaidi.

7. ANAPOJIANDAA KULALA
Tengenezeni mazingira na utaratibu wa kuzungumza kabla ya kulala. Mweleze namna siku yako ilivyokuwa na usikilize upande wake pia. Muda huu wa ukuruba huwaleta pamoja kihisia, na atafurahia kutumia dakika hizo za mwisho kuzungumza nawe.
Kaka yangu, zichunguze ishara zinazoonesha kuwa mke anahitaji umsikilize. Anahitaji uwe pembeni yake anapokuwa na msongo au anapokuwa na furaha. Aidha, kwa upande wako pia, kama unataka mkeo akusikilize, mwambie. Ndoa yenye afya huimarika zaidi pindi wanandoa wanapokuwa na uwazi, ukweli na wakawa tayari kusikiliza.

Related Posts:

  • SHERIA ZA KUWA MAARUFU MWENYE MAMLAKA NA USHAWISHI KATIKA JAMII Hakikisha ujuzi wako haumfuniki mkuu wako au watu wengineUnaweza isiwe ujuzi pekee, lakini hata uwezo wako wa kiakili, mali na uelewa. Hakikisha hauutumii kwa majivuno kuonesha jinsi unavyowazidi wenzako kazini, kwenye bi… Read More
  • MBINU 6 ZA KUIMARISHA UHUSIANO Watu wengi ambao wako kwenye uhusiano wanalalamika kuwa wenzi wao hawawaoneshi upendo kama ilivyokuwa siku za mwanzo za uhusiano wao. Wanaeleza kuwa wanaona uhusiano wao unalegalega na mapenzi yanapungua taratibu kama ba… Read More
  • NAMNA YA KUTAMBUA TABIA YA MTU Hakuna anayependa kusahihishwa, kugombana au kukemewa mbele za watu, hii ndiyo tabia ya watu wajeuri na walio na tabia za kitukutu. Mara nyingine hudhani wanapata sifa. Wako watu wa jinsi hii ambao hawawezi kukugombeza a… Read More
  • HATUA SABA ZA KUTATUA MIGOGORO INAYOTUKABILI Watu wamekuwa wakifanyiana ukatili, nchi zinapigana vita kwa sababu ambazo kama mwanzo zingepata wajuzi wa kuitatua isingeleta madhara makubwa (L. Ron Hubbard, Mtafiti wa Sayansi ya Jamii kutoka Marekani anathibitisha … Read More
  • MSONGO WA MAWAZO NA JINSI YA KUKABILIANA NAO KUNA baadhi ya watu kati yetu ambao wanaweza kufuga mawazo ya kuachwa na wapenzi wao kwa miaka mitano mfululizo, huku wengine wakitumia miezi mingi kuondokana na huzuni iliyotokana na kutukanwa na wazazi, kufokewa na bos… Read More

2 comments:

  1. Hello, I Like your blog, I wanted to leave a little comment to support you and wish you a good continuation. Wish you best of luck for all your best efforts.
    You can also check:benefits of cumin

    ReplyDelete
    Replies
    1. I am FRED and i want quickly recommend DR NCUBE for a Job well done by
      curing me from the genital herpes disease that have be giving me sleepless night. if you want to contact him, Simply do that via email drncube03@gmail.com or 
      call/whatsapp +2348155227532
      he also have #herbs for
      #hiv/aids
      #cancerdisease 
      #fibroid 
      #diabetes

      Delete