Saturday, 30 June 2018

MARADHI YATOKANAYO NA MAAMBUKIZO YA HEWA NA KINGA YAKE

Maradhi yatokanayo na maambukizo ya hewa na kinga yake.

FUNGU hili la magonjwa linajumuisha magonjwa yote yatokanayo na utumiaji wa hewa toka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Msingi wake mkubwa ni hewa yenye vijidudu vya maambukizo (germs) viingiapo katika mfumo wa upumuaji (respiratory tract) wa mtu mwingine.

Njia za uenezaji wa magonjwa katika kundi hili imeenezwa kutoka kwa mgonjwa mwenye vijidudu kwa kuzungumza, kukohoa, na kupiga chafya (sneezing-drops).

Magonjwa haya husambazwa kwa urahisi zaidi katika sehemu zenye msongamano kama mashuleni, katika vyombo vya usafiri, mahoteli na katika kumbi mbalimbali. Sehemu zote hizi ni lazima ziwe na hewa ya kutosha.

Magonjwa haya yamegawanyika katika sehemu kuu mbili na hii ni kutokana na sehemu ya maambukizo yake. Sehemu ya kwanza ni (URTI) Upper Respiratory Tract Infection ambayo inaathiri majimaji yanayotumika kuvilinda viungo hivyo sehemu ya juu (mucous membrane) katika pua, umio la hewa (trachea). Sehemu ya pili ni ile inayoathiri viungo vya chini ya upumuaji ijulikanayo kama (LRTI) Lowre Respiratory Tract Infection kama vile mapafu.

Pia magonjwa haya yamegawanyika tena kutokana na tabia yake, yapo yanayoshambulia kwa muda mfupi na yanayokuja kwa kasi yanafahamika kama (Acute Respiratory Tract Infection) kama vile mafua, kuvimba kwa umio la hewa. Na magonjwa yanayoathiri sehemu za upumuaji za chini (LRTI) kama vile kichomi (pheumonia) ambayo inaathiri mapafu.

Pia yapo yanayodumu kwa muda mrefu wa maambukizo yake (cronic Respiratory Infection - CRI) kama vile kifua kikuu (Tuberculosis) na kifaduro (whooping cough). Kwa ujumla magonjwa yanayotokana na maambukizo ya hewa hutokana na kuwepo kwa vijimelea ni yale ya bacteria na virus.

Magonjwa ya hewa yatokanayo na bacteria ni kifaduro (whooping cough), donda koo (Diphthenia), homa ya uti wa mgongo (meningitis) na mengineyo.

Uvutaji wa hewa ni jambo lisiloweza kuepukika kwani maisha ya kila kiumbe yanategemea hewa katika kuishi kwake, hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari dhidi ya kujikinga na magonjwa haya. Tahadhari hizo ni kuzingatia mambo yafuatayo:

Kuwepo na sehemu ya kuingizia hewa ya kutosha katika kila nyumba ili kuruhusu mzunguko wa hewa kuwa mzuri. Chumba kisiwe nasehemu moja tu ya dirisha, kwani dirisha kama hili kiafya halitakiwi.

Kama ni viwandani au sehemu zenye mkusanyiko wa watu au hata katika nyumba za kuishi ni vizuri uwepo mfumo huo wa asili na ukisaidiwana na mfumo wa hewa uliotengenezwa na binadamu (artificial ventilation).

Hii ni kuwepo kwa mtambo unaofahamika kama plennum system katika mtambo huu hewa hutibiwa, kwa maana vijidudu huuawa na hewa hupozwa na ikawa yenye unyevunyevu na hii inapatikana katika viyoyozi vile vile hewa huwa yenye ubaridi mzuri.

Mfumo mwingine ni ule wa kutoa vumbi vumbi ambalo linaweza kuathiri hewa na kutupwa nje kupitia mtambo maalum. Pia kuna mfumo uunganishao mitambo ya kutoa vumbi viwandani na kuleta hewa yenye ubaridi mzuri. Haya yote hufanywa kwa lengo zima la kupambana na maambukizo yanayotokana na hewa.

Kuepukana na msongamano. Msongamano ni hali ya mlundikano wa watu usiotakiwa kama katika usafiri, mikutano na kadhalika. Kwa ujumla msongamano ni zidio la watu kwa mfano chumba chenye ujazo wa mita 100 ni maalum kwa mtu mmoja, sasa badala ya kuwepo mtu mmoja akaongezeka mwingne hiyo tayari ni msongamano. Sasa ni muhimu kujiepusha na misongamano ili kuepuka maambukizo.

Kuwatenga wagonjwa ( Isolation): Hii ni kuwaweka wagonjwa mbali na watu ili pasiwepo na mawasiliano ya aina yoyote kati ya wagonjwa na wasiokuwa wagonjwa. Japo hali hii inawaathiri wagonjwa kisaikolojia, lakini athari waipatayo wagonjwa ni kidogo ikilinganisha na athari itakayopatikana ikiwa mawasiliano yataruhusiwa. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumezuia maambukizo ya magonjwa.

Kuwepo na utoaji wa elimu ya afya (Health Education): Kutokana na uzito wa maradhi na jinsi ya kujikinga na maradhi hayo, Wizara au Idara inayohusika inapaswa itoe elimu kwa jamii. Ili kujikinga na maradhi hayo watu wazingatie yafuatayo.

Watu wawe na tabia ya usafi (Personal Hygiene) katika kufunika midomo na pua wakati wa kukohoa au kupiga chafya.

Kutumia leso au karatasi wakati wa kupenga kamasi au kutoa makohozi.

Usiteme mate ovyo ndani na nje ya nyumba.

Pasiwepo matumizi ya kuchangia vikombe, mabakuli kati ya mgonjwa na wasio wagonjwa.

Kuvaa vifaa vya kuziba pua na macho (musks): Hii inatakiwa ifanyike viwandani na mahospitalini na husaidia viwandani kuzuia kuvuta hewa ambayo inamchanganyiko wa vumbi kwa kuifanya hewa ichujwe. 

Vile vile huzuia maambukizo ya watu wenye madhara kwa mfano mahospitalini. Pia hukinga maambukizo kwa watoto wazaliwao kabla ya siku kwa kuhakikisha hawapati hewa ipumuliwayo moja kwa moja kutoka 

kwa waganga, wauguzi au watu wenye maambukizo. Kwa kuzingatia hayo tutakuwa tumejikinga na maambukizo kwa njia ya hewa.

Chanjo: Watu hupata chanjo ili kuukinga mwili dhidi ya maambukizo ya magonjwa yaambukizayo kwa njia ya hewa.

Chanjo hutolewa na kitengo cha chanjo nchini EPI Expanded Programme on Immunization. Kifua kikuu 
(Tuberculosis) inazuiwa kwa chanjo ya BCG vaccines, ndui small pox ugonjwa huu umeondoshwa, haupo 

hivi sasa kutokana na jitihada za wataalamu. Surua (measles) hukingwa kwa measles vaccines donda koo (Diphtheria) pamoja na kifaduro (whooping cough) kwa pamoja hukingwa na DPT vaccines. Yote 

tuliyoyaeleza yanatokana na maambukizo ya hewa na jinsi ya kujikinga. Kwa kuzingatia ukweli usiopingika ni kuwa tuipe kinga kipaumbele kwani kinga ni bora kuliko tiba.

0 comments:

Post a Comment