Saturday 30 June 2018

MARADHI YA MIGUU KUWAKA MOTO (PERIPHERAL NEUROPATHY)



Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili 

yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na 

hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo

1.Mtu kuhisi ganzi

2. kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.

3.maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi,
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:

1.Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).

2.Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi

3.Uzito mkubwa wa mwili,

4.Ugonjwa wa kisukari,(diabetic polyneuropathy).

5.Shinikizo la damu,

Nina kuuliza Swali je una uzito wa mwili kilo ngapi? Una miaka mingapi? umeowa au umeolewa? 

Unao ugonjwa wa kisukari? unao ugonjwa wa Maradhi ya Presha? Kapime huenda una Ukosefu wa Kupungua kwa virutubisho Mwilini? Ukipata majibu wasiliana na mimi kwa Private messege

4 comments:

  1. Replies
    1. I am FRED and i want quickly recommend DR NCUBE for a Job well done by
      curing me from the genital herpes disease that have be giving me sleepless night. if you want to contact him, Simply do that via email drncube03@gmail.com or 
      call/whatsapp +2348155227532
      he also have #herbs for
      #hiv/aids
      #cancerdisease 
      #fibroid 
      #diabetes

      Delete
  2. Did you know that there’s a host of back and spine-related issues that are more prevalent in women than men? This includes lower back pain, a guide to back care exercises for women and more, and the risks can get higher as females get older, particularly at post-menopausal age.

    ReplyDelete