Viungo ni kitu muhimu kwenye chakula na huleta ladha ya kufanya
chakula kiwe na hamu zaidi ya kuliwa. Lakini viungo ni si tu huleta
ladha katika chakula lakini pia ni muhimu kwa afya.
Leo tuangalie baadhi ya viungo na umuhimu wake kwa afya zetu:
Chai
Hiki ni kinywaji ambacho hutengenezwa kwa kutumia maji ya moto namajani ya chai. Wakati mwingine sukari na maziwa huongezwa.
Mara nyingine watu wanapotengeneza vinywaji vya viungo huviita
“chai” hata kama havina majani ya chai.
Ukweli ni kwamba chai ni yale majani ya chai.
Faida zake mwilini: Chai ya kijani (Green Tea) hupunguza uzito kwa wale wenye uzito uliozidi mwilini.
Kitunguu saumu (Garlic)
Kitunguu saumu ni kiungo ambacho kimekuwa maarufu kwa matumizi
mbalimbali. Vipo vitunguu saumu vya rangi nyeupe ambavyo mara
nyingi huwa na tumba kubwa ambazo ni chache.
Vingine ni vile vyenye rangi ya zambarau au pinki ambavyo huwa na tumba ndogo na nyingi. Vitunguu hivi vina ubora sawa.
Faida zake mwilini: Husaidia katika uyeyushwaji wa chakula,shinikizo la damu,kuzuia kuharisha na pia hupunguza fangasi za kinywani,maambukizi katika koo na hata mkanda wa jeshi.
Kitunguu saumu kinaweza kutumika katika mapishi ya chakula, chai au
kinywaji chochote cha baridi au cha moto. Mtu anapotumia vitunguu
saumu atumie kwa kiasi. Inashauriwa kutumia vitumba visivyozidi sita
kwa siku hasa kama vitatumika vibichi .
Tangawizi (Ginger)
Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa tangawizi. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa kutengenezwa unga. Ta n g a w i z i inaweza kutumika katika vinywaji vilivyochemshwa. Pia huweza kuongezwa kwenye vinywaji vingine au kwenye chakula.
Iliki (Cardamom)
Iliki ni mbegu zinazotokana na mmea wa iliki ambazo hutumika kama kiungo. Mbegu hizi huweza kusagwa au kutwangwa na kuongezwa kwenye chakula aukatika vinywaji.
Faida zake: Iliki ni nzuri katika kusaidia kupunguza maumivu, kichefuchefu au kutapika. Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula na huongeza hamu ya kula.
Mdalasini (Cinnamon)
Mdalasini ni kiungo kinachotokana na magome ya mmea wa mdalasini. Kiungo hiki huweza kusagwa au kutumika bila kusagwa. Vilevile mdalasini huweza kuongezwa kwenye chakula au katika vinywaji vilivyochemshwa au baridi.
Faida zake:Mdalasini huweza kusaidia kupunguza matatizo kama mafua au flu, vidonda vya kinywani na hata fangasi za ngozi. Vilevile kiungo hiki huongeza hamu ya kula, pia husaidia kupunguza baadhi ya matatizo katika mfumo wa chakula kama kichefuchefu, kutapika au kuharisha.
Kinywaji kilichochemshwa chenye mchanganyiko wa mdalasini na tangawizi hutuliza kikohozi.
Giligilani (Coriander)
Giligilani ni aina ya kiungo ambacho majani na mbegu zake huweza kutumika kama kiungo katika mapishi ya vyakula mbalimbali kama nyama, supu au mchuzi.
Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula na kupunguza gesi tumboni. Pia husaidia kuzuia maambukizi ya bakteria na fangasi.
0766025808 nahitaji iliki na karafuu
ReplyDelete