Sunday 2 November 2014

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KULA SAMAKI WA AINA YA DAGAA KIAFYA



KATIKA TIBA YA LISHE (DAGAA NA FAIDA ZAKE)

Kwa imani ya watu wengi, dagaa ni
kitoweo cha kimaskini, huonekana kuwa
kununua dagaa sokoni au ‘super market’
kwa ajili ya kitoweo, ni dalili ya muhusika
kuishiwa au kuwa na bajeti ndogo.

Tunapoangalia umuhimu wa dagaa na
faida zake katika mwili wa binadamu,
tunagundua kuwa uwe maskini, tajiri au
bilionea, kama unajali afya yako, dagaa
ni muhimu kula kuliko mapochopocho
unayokula kifahari.


Katika makala ya leo tutaangalia faida za
kiafya za dagaa, ambao kama tulivyoona
katika makala mbili mfulululizo zilizopita
kuhusu korosho na karanga, wana faida
kubwa sana katika kupambana na kutoa
kinga ya magonjwa hatari ya moyo!


FAIDA KWA AFYA YA MOYO

Kama ilivyo kwa karanga na korosho,
dagaa nao wameonesha kuwa na faida

kubwa kwa wenye matatizo ya magonjwa
ya moyo. Dagaa wana virutubisho vingi

na miongoni mwa virutubisho hivyo kuna
kiwango kikikubwa cha Omega-3 Fatty


Acids (EPA & DHA).

Katika tafiti nyingi za magonjwa ya moyo
na tiba zake, virutubisho vya Omega 3

vimeonekan kuwa dawa au kinga kubwa
sana ya magonjwa ya moyo. Chanzo
kikuu cha virutubisho hivyo si vingine
bali ni samaki pamoja na dagaa.

Aidha, dagaa pia ni chanzo kizuri cha
Vitamin B12, ikiwa ni chanzo kizuri cha
pili baada ya maini. Vitamin hii

hufanyakazi kubwa ya kuboresha ustawi
wa moyo na hivyo kuwa chakula kizuri
cha kumpa ahueni au kinga madhubuti
mlaji dhidi ya magonjwa ya moyo.


AFYA YA MIFUPA

Dagaa ni chanzo kingine kizuri cha
madini ya ‘Calcium’ yenye jukumu la
kuimarisha mifupa ya mwili, lakini pia
kwenye dagaa kuna vitamin D ambayo
huwa nadra sana kupatikana kwenye
lishe.


Vitamin D
 hufanyakazi muhimu ya
kuimarisha afya ya mifupa kwani ndiyo
inayosaidia unyonywaji mwilini wa
madini ya ‘calcium’. Vile vile dagaa ni
chanzo kizuri cha madini aina ya
‘phosphorus’, ambayo nayo huimarisha
mifupa.


DAGAA NA MARADHI YA KANSA

Kwa miaka mingi, watafiti wameona jinsi
ambavyo dagaa inavyoweza kudhibiti seli

zinazosambaza saratani mwilini. Hivyo
imethibitika pasi na shaka kuwa

virutubisho vilivyomo kwenye dagaa
huweza kutoa kinga kubwa dhidi ya
ugonjwa wa saratani.


WAMEJAA PROTINI

Kama una upungufu wa protini mwilini,
basi kula dagaa kwani wao wana
kiwango kikubwa cha kirutubisho hicho.

Protini husaidia uzalishaji wa ‘Amino
acids’ ambazo ni muhimu kwa uzalishaji
wa chembe hai mwilini na uimarishaji wa
mfumo wa kinga ya mwili (body immune
system).


TAHADHARI


Wagonjwa wa figo na wale wenye
matatizo ya ‘gout’, wanashauriwa kula
dagaa kiasi kidogo na kwa tahadhari

kubwa au kuepuka kabisa. Sababu
inayotolewa ni kwamba, kama ilivyo kwa
baadhi ya vyakula vingine, dagaa huwa
na vitu (purine) ambavyo vinaweza

kuwasumbua watu wenye magonjwa
hayo, vinginevyo dagaa siyo chakula cha
kukosa kula! 

0 comments:

Post a Comment