Sunday 2 November 2014

VIUNGO NA MATUMIZI YAKE KWA KILA SIKU KWA AFYA YAKO PART 2




Leo nimeona tuangalie baadhi ya viungo, matumizi yake na faida zake kwa afya zetu.
Viungo vimekua vikitumika sana kuleta ladha katika chakula au vinywaji mbalimbali,lakini pia huleta afya katika miili yetu.Endelea kusoma uone zaidi:


Kotimiri (Parsley)

Kotimiri ni aina ya mmea ambao majani yake na mbegu zake huweza kutumika kama kiungo katika vyakula.




Majani ya kotimiri husaidia kupunguza msokoto wa tumbo ambao mara nyingi hausababishi kuharisha.

Vilevile kiungo hiki huchochea vimeng’ e n yo tumboni na hivyo kuongeza hali ya kuhisi njaa.

Mbegu za kotimiri huweza kusaidia kuondoa maji ya ziada katika mwili. Kiungo hiki huweza kuongezwa
katika chakula wakati wa kupika au wakati wa kula.



Karafuu (Cloves)

Karafuu hutokana na mmea wa mkarafuu. Kiungo hiki huweza kutumika peke yake au kwa kuchanganya na viungo vingine. Kiungo hiki husaidia kuleta hamu ya kula na kuboresha uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile karafuu husaidia kupunguza kichefuchefu, kutapika na kuharisha.








Ni nzuri ikitumiwa katika supu, mchuzi, juisi ya matunda yenye uvuguvugu au vinywaji vingine vilivyochemshwa.




Binzari (Turmeric/Yellow Root) 

Binzari halisi hutokana na mizizi ya mmea wa binzari manjano ambao hufanana na ule wa tangawizi. Mizizi ya binzari huweza kukaushwa, kusagwa na kutengeneza unga wa binzari ya manjano ambao hutumika kama kiungo cha chakula. Vilevile binzari mbichi inaweza kutwangwa na kutumika kwenye




Mapishi mbalimbali. Binzari ikitumiwa katika chakula, hukifanya kuwa na rangi ya njano.

Binzari inaweza kutumika kwenye mapishi ya wali au vyakula vingine vya nafaka, pia kwe n ye mchuzi au maharagwe.

Binzari husaidia katika uyeyushwaji wa chakula na pia husaidia mwili usiharibiwe na kemikali mbaya.

Ni vizuri kuwa waangalifu tunaponunua binzari ile ya unga kwani wakati mwingine wauzaji huuza binzari ambayo si binzari halisi.

Binzari hii ambayo si halisi hutengenezwa kwa kutumia aina za unga wa nafaka ambao huchanganywa na rangi ya manjano na binzari kidogo.





Limau (Lemon)
Limau linaweza kutumika kama kiungo katika chakula na vinywaji kama chai au vinywaji vingine.




Limau husaidia kuboresha uyeyushwaji hasa wa protini na mafuta. Limau pia huweza kutuliza vidonda
vya kooni, kikohozi, homa na kuondoa msongo.



Binzari nyembamba (Cumin seeds)

Hizi ni mbegu nyembamba ambazo hufanana na mbegu za giligilani. Mbegu hizi huweza kusagwa na kutengeneza unga ambao hutumika kama kiungo katika mapishi mbalimbali mfano; supu, mchuzi, wali, n.k.




Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguza maumivu ya tumbo na hata kuharisha.



Mrehani (Basil)

Mrehani ni aina ya kiungo ambacho huweza kutumika kwa kuongezwa katika chakula. Kiungo hiki husaidia kupunguza kichefuchefu na kusaidia uyeyushwaji wa chakula na kutuliza maumivu ya kichwa. 





Kwa vidonda vya kinywani mrehani unaweza kutumika kwa kusukutua.




“Calendula”

Vikonyo vya maua ya ‘‘calendula’’ vina kemikali inayozuia kukua kwa vijidudu kama bakteria katika jeraha, ngozi na pia kupunguza hali ya mwako wa moto (anti-inflammatory function). Vilevile “c a l e n d u l a” hupunguza maambukizi mbalimbali katika mfumo wa chakula.





‘‘ C a l e n d u l a’’ inaweza kutumika kutibu vidonda. Vilevile inaweza kutumiwa kama kinywaji kilichochemshwa ili kuboresha uyeyushwaji wa chakula tumboni.




Pilipili (Cayenne pepper)

“Cayenne” ni mchanganyiko wa aina za pilipili za jamii ijulikanayo kama “capsicum”. Pilipili hizi huwa ndefu na nyembamba, mara nyingi huwa ni kali na zina rangi nyekundu. Jamii hii ya pilipili huweza kukaushwa na kusagwa na hivyo kutengeneza unga laini ambao huwa na rangi nyekundu.






“Cayenne” huweza kuongeza hamu ya kula. Pilipili hii inaweza ikatumika kwa kuongezwa kwenye chakula wakati wa kupika au wakati wa kula. Pia huweza kuongezwa katika juisi au maji ya kunywa. Hata hivyo ni vyema pilipili itumiwe kwa kiasi.




Shamari (Fennel)

Shamari ni kiungo ambacho mbegu zake hufanana na zile za binzari nyembamba. Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula na kupunguza gesi tumboni.



Shamari inaweza kutumika kama kiungo kwenye chakula. Mbegu za shamari zinawez a
kutumika kuandaa chai au kinywaji chochote cha moto. Ni vizuri ikitumiwa kwa kiasi.




Nanaa (Mint)


Nanaa ni majani ya mnanaa ambayo hutumiwa kama kiungo. Nanaa husaidia katika kuzuia hali ya mwako wa moto tumboni, kupunguza kichefuchefu, kuzuia kutapika na kuharisha. Pia huweza kupunguza maumivu ya tumbo na mkakamao wa misuli. Vilevile nanaa husaidia katika uyeyushwaji wa chakula tumboni.




Nanaa iliyooshwa vizuri kwa maji safi na salama inaweza kutafunwa. Vilevile inaweza kutumika kutengeneza kinywaji cha moto au kusukutua wakati mtu anapokuwa na vidonda kinywani




“Thyme” ZAATAR

‘‘T h y m e’’ inaweza kuzuia maambukizi yanayosababishwa na bakteria au fangasi. Vilevile kiungo hiki husaidia kupunguza kikohozi na kulainisha koo. Zaidi ya hayo “thyme” husaidia ukuaji wa bakteria wazuri wanaosaidia katika uyeyushwaji wa chakula tumboni. Inaweza kutumika kama kinywaji cha moto au kusukutua.






Meti (Methi)  UWATU

Meti ni majani ya mmea uitwao kwa Kiingereza

“Fenugreek”. Kwa Kiswahili inaitwa (Uwatu) Hii ni aina ya kiungo ambacho huchochea uvunjaji wa kemikali mwilini yaani umetaboli. Majani ya meti yanaweza kukaushwa na kutumika kama kiungo au kutumika yakiwa mabichi. Vilevile mbegu za “Fenugreek” UWATU huweza kukaushwa, kusagwa na kutumika katika kutengeneza unga wa viungo yaani “curry powders”. 


Meti inaweza kutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali ikiwa ni pamoja na mboga za majani na vilevile katika mapishi mbalimbali ya samaki.

0 comments:

Post a Comment