Saturday 27 September 2014

SARATANI YA MATITI NA NAMNA YA KUJICHUNGUZA MWENYEWE



Saratani ya matiti ni ugonjwa ambao huwapata wanawake na unatokana na athari za chembe ndogo ama seli kwenye matiti na matokeo yake ni kwamba hubadili mfumo wa kawaida wa kukua na kuongezeka.

Mabadiliko haya huanza polepole na yanaweza yakachukua muda mrefu hadi mtu kuweza kujua kama ana matatizo hayo. Ikiwa katika hatua hizo za mwanzo kwa kawaida huwa haina maumivu jambo hilo ni moja ya mambo ambayo huchangia baadhi ya wagonjwa kubaini tatizo hilo wakati tayari limekomaa.


Ni kutokana na sababu hizo, wanawake hutakiwa kuchunguza afya zao mara kwa mara kwa sababu ugonjwa huweza kutibiwa kirahisi iwapo utabainika mapema, miongoni kwa dalili mwa dalili za saratani ya mititi ni uvimbe kwenye matiti ama makwapa. Titi kubadilika kiumbo, titi kutoa majimaji yakiyochanganyika na damu ama chuchu kuingia ndani.

 Dalili zingine ni rangi ya ngozi ya titi kubadilika na kuonekana kama ngozi ya nje ya chungwa na ile hali yake ya kuonekana kuwa na ngozi laini hutoweka.
Mwanamke anaweza kujinguza mwenyewe maradhi haya ya saratani na kujua kama ameathirika ama la, kabla ya kufanya uchunguzi huu unapaswa kufahamu masharti yafuatayo:

Kama anayejichunguza ana umri zaidi ya miaka 20, anapaswa kuhakikisha anaufanya katika siku ya tano, sita na saba baada ya kumaliza hedhi. Unapaswa kufuata hatua kwa hatua katika uchunguzi huo. Hizi ni hatua zifuatavyo:

Utakiwa kuwa na kioo kikubwa kiasi ambachoo waweza kujiona vyema angalau kifua chote. Tafuta sehemu ambayo mwanga utakuwa unakupiga kifuani na kioo kuwa mbele yake.

Hii mara nyingi inapaswa kufanywa chumbani ambako mtu aweza kupata faragha kwa kuwa itampasa kuvua nguo angalu kifua kukiacha wazi. Kioo hicho waweza ukawa umekitundika ukutani ama sehemu yoyote ambayo utajiona vema ukiwa umesimama.

Vua nguo na kuhakikisha kifua na tumbo lipo wazi. Hatua ya kwanza jiangalie kwenye kioo ukiwa umesimama wima na umeweka mikono kiunoni. Angalia kama kuna mabadiliko katika umbo au rangi ya ngozi ya matiti na kama chuchu zinaonekana kutumbukia ndani ya titi.

Unaweza kulinganisha rangi kwa matiti yote mawili na kuona kama zinafanana. Kama yanatofautiana yawezekana kuna athari, pia kama moja ya titi litaonekana chuchu imeingia ndani, pia ni moja ya viashiria vya athari ya aina hii ya saratani.

Hatua ya pili, nyanyua mkono juu na viganja vishikane juu ya kichwa chako. Hapa chunguza kama kuna mabadiliko yoyote katika mlingano wa ukubwa wa matiti. Kama moja litaonekana kuwa kubwa zaidi ya jingine pia ni moja ya viashiria vya athari.
Hatua ya tatu, hii haihitaji kioo, unachotakiwa kufanya ni kusimama wima na kunyanyua mkono wa kushoto juu huku vidole vya mkoo wako wa kulia vikiwa vinabinya na kuachia kwa mzunguko kwenye titi kuangalia kama ndani kuna uvimbe.

Baada ya kumaliza kwa titi la kushoto vivyo hivyo utafanya kwa titi la kulia. Njia hii pia waweza kuifanya ukiwa umelala chali.

Hatua ya nne, ni ya kuchunguza matiti kwa kukamua na kuangalia kama kuna ute uliochanganyika na damu. Iwapo utakuwepo wa namna hiyo basin i kiashirio kwamba kuna uwezekano wa kuwa na athari za ugonjwa huu.
Yawezekana ukawa na uvimbe ama kitu kingine chochote lakini ikawa ni matatizo mengine yasiyohusu saratani. Wataalamu wa ugonjwa wa saratani ya matiti ndio watakaothibitisha kama una atahri hizo na si vinginevyo.
Wataalam waliofanya utafiti juu ya saratani ya matiti walibaini kwamba hali hiyo inaweza kusababishwa na sababu mbalimbali.

Sababu hizo ni kama vile kuanza hedhi katika umri mdogo, kukoma hedhi katika umri mkubwa, mwanamke kufikisha umri bila kuzaa na utumiaji wa mafuta mengi katika mlo.  

Mambo mengine yanaweza kuchangia saratani ya matiti ni mama kutonyonyesha baada ya kujifungua ana kumnyonyesha kwa muda mfupi. Kuna kina mama wenye tabia ya kutaka, kutonyonyesha kutokana na sababu zao mbalimbali ambazo mara nyingi siyo za msingi.

Mambo mengine ambayo yanachangia mtu kupata saratani ya titi ni unene kupata kiasi, kutofanya mazoezi mara kwa mara, uvutaji wa sigara, matumizi ya pombe kupita kiasi, wa wakati mwingine inaweza kurithiwa kutokana na historia ya saratani ya matiti katika jamii husika.

Mgonjwa wa saratani ya matiti aweza kupata tiba na kupona kabisa hivyo hakuna haja ya kuwa na wasi wasi. Hata hivyo, kama nilivyoeleza awali, mtu anapaswa kuibaini mapema kwa sababu ni wakati ambao anaweza akapatiwa tiba na kupona kwa urahisi.

Aina zote za saratani ni kwamba zinapaswa kuibainiwa mapema kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kuweza kuitibu na kupona bila ya mtu kupata matatizo mengi.  Zipo aina mbalimbali za tiba na mojawapo ni upasuaji. Upasuaji huu kwa kawaida hufanywa katika hatua za mwanzo.
Njia nyingine ni tiba ya mionzi au kupewa dawa. Jambo la kukumbukwa ni kwamba ugonjwa huu unaweza kusababisha kifo iwapo hautabainika mapema na kupatiwa tiba mwafaka.

Njia ambayo mtu aweza kujilinda asiathirike na saratani hii ya matiti ni kujichunguza mara kwa mara ili kubaini mapema ma kupatiwa dawa.
Kwa kawaida ,mwanamke anapaswa kuchunguzwa mara moja kwa mwaka ili kuona kama ameathirika na ugonjwa huo au la.

1 comments: