Saturday 27 September 2014

SATARANI YA MATITI (BREAST CANCER) 1-2-3

Leo tutaanza kujadili ugonjwa wa saratani au kansa ya matiti inayowashambulia zaidi wanawake japokuwa hata wanaume nao huugua.
Kama nilivyosema hapo juu kwamba ingawa, saratani ya matiti huweza kuwapata wanawake lakini wanaume pia hukumbwa, lakini imeonekana kuwa watu wa jinsia ya kike ni waathirika wakubwa zaidi wa saratani hii kuliko wa jinsia ya kiume.
Uwezekano wa kupata saratani hii huendana na umri wa mtu. Kadiri umri wa mtu unavyoongezeka ndivyo pia uwezekano wa kupata saratani hii unavyozidi kuwa mkubwa.
Wanawake walio na umri wa kuanzia miaka 50 wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maradhi haya kuliko walio na umri wa chini ya  miaka 45.
Wanawake ambao hawajazaa au kunyonyesha wapo kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya matiti. Wanawake wanaopata ujauzito kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 nao pia wapo. Lakini pia wanawake ambao familia zao zina historia ya ugonjwa huu wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya matiti ikilinganishwa na wale ambao hawana historia ya ugonjwa huu katika familia zao.
Kwa mwanamke aliye na ndugu kama vile mama, dada au mtoto ambaye aliwahi kupata saratani hii kabla ya umri wa miaka 50, uwezekano wa mwanamke huyo kupata ugonjwa huu ni mara mbili ya yule ambaye hana historia hii.
Wanawake wanaovunja ungo kabla ya umri wa miaka 12 nao wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu au wale wanaoacha kupata hedhi. Kwa kawaida wanawake huacha kupata hedhi wakishafikia kuanzia miaka 45, hali ambayo kitaalamu hujulikana kama Menopause.
Wanawake wanaoendelea kupata hedhi wakiwa na zaidi ya miaka 45, wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata kansa ya matiti lakini pia wanawake ambao wamewahi kupata ugonjwa huu kwenye titi la upande mmoja hapo kabla, wana uwezekano mkubwa wa kupata tena saratani kwenye titi la upande mwingine katika siku za usoni.

SATARANI YA MATITI (BREAST CANCER) - 2

WIKI iliyopita tulianza kuelezea kuhusu saratani ya matiti, ugonjwa unaosumbua baadhi ya akina mama na hata wanaume. Endelea kuelimika.
Wanawake ambao wamewahi kupata ugonjwa huu kwenye titi la upande mmoja hapo kabla, wana uwezekano mkubwa wa kupata tena saratani kwenye titi la upande mwingine katika siku za usoni.
Sababu nyingine inayoweza kusababisha saratani ya matiti ni ulaji wa vyakula venye mafuta mengi. Tafiti zinaonesha kuwa, wanawake wanaopendelea kula vyakula vyenye mafuta mengi wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.
Pia kuongezeka uzito ni miongoni mwa sababu zinazoweza kusababisha ugonjwa huo. Tafiti nyingine zimeonesha kuwa, wanawake wanene wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya matiti wakilinganishwa na wale walio na uzito mdogo au wa kati.
Hali kadhalika uvutaji sigara ni sababu nyingine inayotajwa kuchangia saratani ya matiti. Kuna matokeo yenye kukinzana kuhusu uhusiano wa uvutaji sigara na hatari ya kupata kansa ya matiti.
Wakati baadhi ya tafiti zinaonesha uhusiano wa karibu kati ya uvutaji sigara na uwezekano wa kupata saratani ya matiti, tafiti nyingine zinaonesha majibu tofauti kuhusu uhusiano wa uvutaji sigara na saratani ya matiti.
Hata hivyo, kwa ujumla, wanawake wanaojizuia kuvuta sigara huwa na afya njema zaidi kuliko wale wanaovuta sigara. Sababu nyinginezo ni unywaji pombe, historia ya tiba ya mionzi na matumizi ya dawa za kupanga uzazi.
Imeonekana kuwa wanawake wanaokunywa pombe zaidi ya chupa moja kwa siku wana uwezekano zaidi wa kupata kansa ya matiti kwa asilimia zaidi ya 20 kuliko wengine. Pia Wanawake ambao wamewahi kupata tiba ya mionzi hususani wakati wa ukuaji wa matiti, wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.

DALILI ZA KANSA YA MATITI(BREAST CANCER) - 3

Wiki mbili tumekuwa tukichambua ugonjwa wa kansa ya titi, leo tunaeleza dalili za maradhi haya.
Nijua kuwa wanawake wengi wanajiuliza ni zipi dalili za saratani ya matiti? Dalili ya awali inayoweza kutambulisha saratani ya matiti ni kuwepo kwa uvimbe kwenye titi ambao huwa na hali tofauti na sehemu nyingine za titi.
Hata hivyo, si kila uvimbe kwenye titi unaashiria uwepo wa saratani ya matiti. Uvimbe huu huwa mgumu, unaochezacheza au ambao hauko thabiti, ambapo wakati mwingine unaweza kuwa na maumivu makali au kusiwe na maumivu yoyote.
Uvimbe huu huwepo zaidi ya mzunguko mmoja wa hedhi kwa wale ambao hawajaacha kupata hedhi. Dalili nyingine ni pamoja na  kuwepo uvimbe kwenye sehemu za kwapa, sehemu ya titi kuingia ndani, hali  inayoashiria uvimbe usioonekana au usioweza kuhisiwa na mabadiliko kwenye chuchu, kama vile chuchu kuzama ndani au kuwa na nundu ndogondogo, 
chuchu kuwasha, kuhisi kama kuchoma, kidonda kwenye chuchu au chuchu kuwa na kovu ambalo huashiria saratani ya sehemu hiyo.
Dalili nyingine za kansa ya matiti ni kubadilika kwa umbo la titi na rangi ya ngozi kuwa nyekundu (redness/rush), ngozi ya titi kuwa kama ganda la chungwa (skin changes) na kuongezeka kwa joto kwenye titi.
Dalili hizi huashiria kusambaa kwa saratani mwilini. Dalili nyingine ni chuchu kutoa maji ambayo hayana rangi. Mara nyingine chuchu hutoa majimaji yenye rangi tofauti.
Baada ya kuzijua dalili kwa kawaida mgonjwa hushauriwa kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na wataalamu wa afya ili kuweza kutambua kuwepo tatizo hili na baada ya hapo kufanyiwa vipimo vifuatavyo ili kusaidia kutambua ugonjwa huu.
Vipimo vya kutambua kansa ya matiti kwa kawaida ni X-ray ya matiti au Mammogram ambayo ina uwezo wa kuonesha ulipo uvimbe kwenye matiti. Kingine ni Ultra-Sonography ambacho husaidia kutambua iwapo uvimbe uliopo ndani ya matiti umejaa maji ama la, ili  mgonjwa afanyiwe vipimo zaidi juu ya ugonjwa huo.

0 comments:

Post a Comment