KUNA magonjwa mengi ambayo watu hukumbana nayo lakini leo tutajadili magonjwa ambayo hutoa majimaji au usaha sehemu za siri na huweza kusababisha muathirika kutopata mtoto.
Magonjwa hayo ni yale ya ngono ambayo huweza kuwapata watu wa rika na jinsia zote, hususan walio katika umri kati ya miaka 15 hadi 49.
Magonjwa hayo ni yale ya ngono ambayo huweza kuwapata watu wa rika na jinsia zote, hususan walio katika umri kati ya miaka 15 hadi 49.
Vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 24 wako katika hatari zaidi ya maambukizi ya magonjwa hayo ya ngono kwa kuwa wanapobalehe, hupata hisia au hamu ya kujamiiana.
Hali hii husababishwa na vichocheo au homoni zilizomo mwilini ambazo husababisha hisia za kufanya ngono.
Hali hii husababishwa na vichocheo au homoni zilizomo mwilini ambazo husababisha hisia za kufanya ngono.
MAKUNDI YA MAGONJWA YA NGONO
Kuna aina mbalimbali za magonjwa ya ngono ambayo yamegawanywa katika makundi kutokana na dalili zake.
Kuna aina mbalimbali za magonjwa ya ngono ambayo yamegawanywa katika makundi kutokana na dalili zake.
KUNDI LA KWANZA
Kundi hili ni magonjwa yenye dalili za kutokwa usaha au majimaji sehemu za siri (ukeni na uumeni) ambayo ni kisonono, trichomonas na candida.
Kundi hili ni magonjwa yenye dalili za kutokwa usaha au majimaji sehemu za siri (ukeni na uumeni) ambayo ni kisonono, trichomonas na candida.
KUNDI LA PILI
Pia kuna kundi la pili ambalo ni la magonjwa ya ngono ambayo dalili zake ni kutokwa na vidonda, ambayo ni kaswende na malengelenge sehemu za siri.
Pia kuna kundi la pili ambalo ni la magonjwa ya ngono ambayo dalili zake ni kutokwa na vidonda, ambayo ni kaswende na malengelenge sehemu za siri.
KUNDI LA TATU
Kundi la tatu ni magonjwa yenye dalili za kutokwa na uvimbe ambayo ni mitoki na pangusa sehemu za siri.
Kundi la tatu ni magonjwa yenye dalili za kutokwa na uvimbe ambayo ni mitoki na pangusa sehemu za siri.
Napenda ieleweke kwamba mtu anaweza kuwa na zaidi ya ugonjwa mmoja wa ngono kwa wakati mmoja. Kujitokeza dalili za ugonjwa wa ngono hutegemea aina ya ugonjwa, jinsi na kinga ya mwili.
Hatari kubwa ya makundi yote ya magonjwa hayo ni kwa wanawake au watu wa jinsia ya kike kwani asilimia 60 mpaka 70 (ya wanawake) wenye kisonono hawaoneshi dalili yoyote wakati wanaume ni kati ya asilimia 10 na 15.
Hivyo ni muhimu kwa kijana wa kiume akiona dalili za ugonjwa kumueleza mwenzi wake wa kike aliyejamiiana naye ili wote waende kwenye kituo cha huduma ya afya kwa uchunguzi na tiba.
DALILI KWA MWANAMKE
Mwanamke aliyekumbwa na maambukizi ya ugonjwa wa ngono mara nyingi hujisikia maumivu chini ya kitovu au kutokwa na usaha au majimaji yenye harufu mbaya sehemu za siri.
Mwanamke aliyekumbwa na maambukizi ya ugonjwa wa ngono mara nyingi hujisikia maumivu chini ya kitovu au kutokwa na usaha au majimaji yenye harufu mbaya sehemu za siri.
Anaweza kuwashwa sehemu za siri au akatokwa na vidonda na vipele kwenye nyeti zake, mdomoni na sehemu nyingine za mwili.
Wakati wa kujamiiana anaweza kusikia maumivu au akawa amevimba mitoki, kuota mafundofundo sehemu za siri na kukojoa mara kwa mara kunakoambatana na muwasho au maumivu.
DALILI ZA UGONJWA WA NGONO KWA WANAUME
Dalili za tatizo hili kwa wanaume ni kujisikia maumivu wakati wa kukojoa au kutokwa na usaha sehemu ya mbele kwenye dhakari.
Dalili za tatizo hili kwa wanaume ni kujisikia maumivu wakati wa kukojoa au kutokwa na usaha sehemu ya mbele kwenye dhakari.
Mgonjwa atasikia maumivu makali sehemu za siri wakati wa kukojoa; atatokwa na usaha pamoja na kuwa na vidonda sehemu za siri na mdomoni na atavimba mitoki na kupata malengelenge sehemu za siri.
0 comments:
Post a Comment