Sunday, 31 August 2014

ONGEZEKO LA WANAUME WAGUMBA



Wanaume wengi hapa nchini na nchi nyingi za Afrika bado hawafahamu kwamba tatizo la ugumba si kwa wanawake pekee bali wanaume pia hukumbwa na tatizo hili tena kwa asilimia sawa kabisa na wanawake.Tafiti za kitabibu zinaonesha kuwa matatizo ya ugumba huwakuta wanaume kwa asilimia 50 kama ambavyo 50% inayobaki huwa ni kwa wanawake.
Kutofahamu huku kumekuwa mwiba mkali kwa wanawake pale inapotokea wanandoa wameishi zaidi ya mwaka mmoja bila mwanamke kufanikiwa kushika ujauzito wakati wanashiriki tendo la ndoa bila kinga yoyote.
Ugumba kwa wanaume maana yake mwanaume kupoteza uwezo wake wa kutungisha mimba ambao  alikuwa nao awali.
Hii maana yake ni kwamba mwanaume anaweza kuwa na uwezo mzuri wa kushiriki tendo la ndoa lakini hawezi kusababisha ujauzito.
Hili ni tofauti na tatizo la mwanaume kushindwa kabisa kushiriki tendo la ndoa, au lile la wanaume kuwahi kufika kileleni na baada ya tendo hilo moja hupatwa na uchovu mkubwa na kushindwa kurudia awamu nyingine dakika chache kukumbwa na usingizi.
Matatizo yote haya hutibika kama mwanaume ataamua kwa dhati kuchukua jukumu la kutafuta huduma/tiba katika hospitali/kliniki sahihi.
Katika makala haya, nitafundisha dalili, vyanzo, na jinsi ya kujikinga kuingia katika dimbwi la ugumba kwa wanaume.
Dalili za ugumba kwa wanaume
Mara nyingi wanaume wagumba huwa hawaoneshi dalili za moja kwa moja, jambo ambalo hufanya jamii kuwa na tabia ya kupeleka mzigo wa lawama kwa wanawake. Wanandoa wengi huanza kupatwa na wasiwasi wanapofikisha mwaka mmoja au zaidi bila mama kufanikiwa kushika ujauzito.
Katika kipindi hiki ndipo wanume nao huanza kuwa na mashaka japo wengi wao huwa hawaoneshi mashaka hayo waziwazi mbele ya wenza wao.
 Hata hivyo, dalili zifuatazo huashiria tatizo la ugumba kwa wanaume:
•Kushindwa kutotungisha mimba kwa miezi 12 au zaidi
•Kuwa na matatizo ya kufika kileleni kwa mfano kuwahi sana na au kuchelewa sana au kushindwa kabisa kufika kileleni
•Kutomaliza tendo la ndoa na uume kusinyaa wakati wa tendo
•Maumivu ya korodani
•Uvimbe kwenye korodani
•Kupungua kwa korodani au kupotea/kuingia ndani kwa korodani
•Kupungua kwa vinywelea, ndevu na hata nywele
•Kuwa na korodani ngumu kupita kiasi
•Kupoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa
•Tatizo la mwanaume kushindwa kabisa kuinuka.

0 comments:

Post a Comment