Tuesday, 19 August 2014

MAAJABU YA MIMBA HONGERA KWA KUPATA MIMBA PARTI -4




Wiki ya Kumi na Saba

· Unaweza kutoa jasho zaidi kuliko kawaida, na
labda pua inaziba. Unaweza kusikia tumbo la
uzazi limefika nusu njia mpaka utovu.
· Mtoto anakaa kwenye robo lita ya maji.
Anaweza kusikia kelele kubwa nje ya mwili
wako.

Wiki ya · Kama ni mimba yako ya kwanza, utatambua
akili yako tayari huwa vimeshapokea ile hali ya ujauzito na kujisikia
shauku ya uchungu na uzazi.

Katika wiki la kumi na nane la ujauzito wanawake wengi
wajawazito huanza kuvaa ‘tenite’ kwa vile wakati huu mimba
huanza kuonekana waziwazi. Bila kujali kama umeanza
kuonyesha mimba au la, muda mfupi tu utaanza kujisikia mtoto
akicheza cheza tumboni, akipiga mateke na kujigeuzageuza na

hata kuwa na kwikwi. Kitoto hiki kinakuwa na uwezo wa kulala na
kuamka kama mtoto mchanga aliyezaliwa; anapokuwa ameamka,
anajisogeza sogeza ndani ya yale majimaji akiwa huru kabisa
kama mtu aliyeko angani akielea kutoka upande huu kuelekea
upande mwingine, akipanda juu na kushuka chini.
Katika miezi mitatu ya pili tangu mimba kutungwa,

unapaswa kula zaidi vyakula vyenye majimaji – kwa kiasi cha
vikombe saba au vinane kwa siku. Unashauriwa kunywa maji,
maziwa, juisi ya matunda (maji ya matunda) au supu. Unahitaji
majimaji kwa sababu lile kondo la nyuma linapaswa kutoa damu

nyingi kwa ajili ya mtoto aliyeko tumboni. Ili kupata damu nyingi
unahitaji vitu vya maji maji zaidi. Vitu kama chai, kahawa na soda
si vizuri ukavipendelea kwa vile husababisha upoteze maji mengi
kwa kukojoa kojoa.

Wakati uliopita (zamani kidogo), wajawazito wengi
waliambiwa wapunguze chumvi katika vyakula vyao, lakini sasa
madaktari wametambua kuwa kitoto kichanga (au kwa lugha ya
kitaalamu fetus – kimjusi) kinahitaji chumvi ili kukua vizuri. Chumvi

itakusaidia pia wewe kutunza majimaji mwilini, hivyo, weka chumvi
katika chakula chako hadi ikolee, bila kuzidisha.
Wakati wa uja uzito, kinga yako ya mwili imepungua. Ni
muhimu kujilinda dhidi ya malaria. Nunua chandalua na kukitia
dawa ya kuwaua mbu. Dalili ya malaria pia yanabadilika wakati wa

mimba. Ukijisikia ovyoovyo, nenda kupimwa damu yako mapema.
Utapewa dawa ya SP mara mbili wakati wa mimba yako –
baada ya wiki 20 na wiki 30. Hizi zinawaua wadudu wa malaria
ambao wanakaa kimya mwilini, na kukulinda na kupungukiwa
damu kwa sababu ya malaria sugu.
Pia utapigwa sindano ya Tetanus (Pepo punda) kama huna
kinga, ili kulinda mtoto wakati akiwa mchanga

Mama

Sasa unaingia awamu ya tatu ya ujauzito wako. Mume
wako, jamaa zako na marafiki wanaweza sasa kujifurahisha kwa
kugusagusa tumbo lako, kwa vile sasa wataweza kuhisi mateke ya
mtoto.

Katika muda wa mwezi wa saba wa mimba, unaweza
kujisikia kutokwa na majimaji yakidondoka katika chuchu yenye
rangi ya njano haya yanaitwa ‘danga’ au kwa lugha ya kitaalamu
colostrum. (Unaweza kuona tena ‘Kolostrumi hii ikichuruzika
baada ya kujifungua, kabla ya maziwa yenyewe kuanza kutoka,
usiogope. Hii haina maana kwamba huwezi kutoa maziwa siku za
baadaye.

Katika mwezi wako wa nane, mtoto wako anakuwa na
shughuli nyingi utafikiri umebeba mwanariadha wa michezo ya

Olimpiki tumboni mwako! Hata kama mtoto wako atarudiarudia, au
hata akijirusha haraka haraka na kujigeuzageuza, usiogope. Hii
inaweza kuwa si kitu chochote isipokuwa ni kwikwi tu.
Kati ya wiki tatu na sita kabla ya kuzaliwa, kichwa cha mtoto
unaweza kukihisi kama tikiti maji kati ya mapaja yako. Unaweza

kujisikia usiye na raha ukitaka kukaa chini. Unaweza pia kujisikia
kama ni kitu cha kuchekesha na kujihisi kama kuna kengele
inagongagonga ndani ya uke wako, haya ni matokeo ya mtoto
wako kuinua kichwa chake kukishusha na kujigonga sehemu ya
chini ya nyonga zako.

Wakati huu utambue kuwa mtoto yuko tayari, kipindi hiki cha
miezi mitatu ya mwisho chaweza kuwa ni cha changamoto kwako
hasa kuhusiana na hisia zako. Akina mama wengi huanza kuhisi
shauku ya uchungu wa kuzaa, pengine huanza kuwaza juu ya
mipangilio ya kifedha itakuwaje baada ya mtoto kuzaliwa. Lakini
furaha ya matazamio na uzoefu mwingine waweza kumaliza
wasiwasi huu. Wazazi wote wawili wakizungumza kwa pamoja juu
ya kuzaliwa kwa mtoto yaweza kuleta furaha.

Kama hapo awali, lishe bora wakati huu wa miezi mitatu ya
mwisho ni ya muhimu sana. Chembe chembe za ubongo wa
mtoto huanza kujitengeneza haraka haraka, hasa katika miezi
miwili ya mwisho kabla mtoto hajazaliwa. Ule vizuri sasa, kwa

kuwa utakuwa unasaidia kuchangia upendeleo wa mtoto baada ya Wiki Mendeleo ya Mtoto na Mama Wakati wa Ujauzito


Wiki yaKumi naNane
· Kama ni mimba yako ya kwanza, utatambua
mazunguko ya mtoto akicheza tumboni.
· Mtoto anaanza kunenepa zaidi ingawa bado
unaweza kuona mishipa ya damu yake kwa
sababu ya ngozi nyembamba. Ana sm 20 na
anapenda kupiga teke.


Wiki yaKumi naTisa
· Unaona kwamba unanenepa kidogo, na tumbo
linaanza kueneza.
· Mtoto anaanza kupata jicho la meno ya pili
kwenye taya.


Wiki yaIshirini
· Unaweza kuanza kuona na macho michezo ya
mtoto, na mtu anaweza kusikia kutoka nje.
Atakuwa na kipindi anapolala, hasa ukitembea
kwa sababu unampembeza tumboni. Tumbo
la uzazi limefika utovu.
· Kuna glands kwenye ngozi ya mtoto
zinazotengeneza kama majimaji. Hii inafunika
ngozi yote ya mtoto kulainisha na kulinda.

Mtoto ana sm 25.

Wiki yaIshirini na Moja
· Unaweza kuanza kujisikia kiungulia.
(Heartburn)
· Mtoto ana 450g. Anacheza sana tumboni.


Wiki yaIshirini na Mbili
· Hutataka kusimama kwa vipindi virefu. Ufizi
unaweza kuvimba.
· Mtoto analala na kuamka tumboni.


Wiki yaIshirini naTatu
· 
Unaweza kutofautisha sehemu mbalimbali ya
mwili wa mtoto tumboni. Tumboni itasikia kama
inavuta wakati fulani.
· Mtoto bado hajanenepa kabisa, lakini
anafanana na kama atakavyokuwa
atakapozaliwa.

Wiki ya · Daktari ataweza kusikiliza moyo wa mtoto


kuzaliwa, kuhusiana na ujuzi wa kujifunza na nguvu za mwili.
Haishauriwi kuruka mlo wowote wakati wa ujauzito. Baadhi
ya wataalam wanahisi kuwa hata upunguzaji wa virutubisho
vyenye ubora wa juu unaweza kuchangia matatizo kwa mtoto
wako. Hivyo, ng’ang’ania ulaji ule ule wa chakula muhimu kama
ilivyojadiliwa huko nyuma.

Baadhi ya wataalam wanaona kwamba madini ya chuma ni
virutubisho namba moja ambavyo hukosekana kwa wajawazito;

upungufu wa damu hujitokeza baadaye, hivyo hakikisha unashika
barabara ongezeko la utumiaji wa vyakula vyenye madini ya
chuma. Ulaji wa vyakula yenye Vitamini C kama vile maji ya
machungwa, utaimarisha ufyonzaji wa chuma ndani ya mwili wako.

Vyakula Vyenye madini ya Chuma
Maini
Nyama ya Ng’ombe
Spinachi
Maharage makavu
Ngano

Katika miezi mitatu ya mwisho, mtoto anahitaji zaidi chokaa
(calcium) kwa ajili ya utengenezaji wa mifupa na meno. Iwapo
hutapata chenye chokaa katika mlo wako ambayo huhitajiwa na
kitoto (kimjusi) na kwa utengenezaji wa maziwa, basi itatolewa
katika mifupa na meno yako mwenyewe.
Usipunguze chakula ili mtoto azaliwe mdogo – kafanya
hivyo inaweza kuharibu afya yake
Wiki Mendeleo ya Mtoto na Mama Wakati wa Ujauzito


0 comments:

Post a Comment