Tuesday 19 August 2014

MAAJABU YA MIMBA HONGERA KWA KUPATA MIMBA PARTI -3


Wiki yaTisa
· Ufizi wako unaweza kuwa laini kuliko
kawaida na ni muhimu kupiga mswaki vizuri
mpaka utakapojifungua.
· Mtoto ana vidole vyake mikononi na miguuni.
Anaanza kucheza tumboni ingawa huwezi
kusikia bado. Mtoto ana uzito kama zabibu

Uchungu na Kujifungua
Uchungu hakika ni mojawapo ya mafumbo makubwa, kwa
kuwa sayansi bado haijatambua kitu gani kinachoanzisha. Hata
hivyo, yawezekana daktari wako ameshakueleza dalili za
waziwazi, japokuwa haiwezekani mama wajawazito wawili wakawa
na uzoefu ule ule wa uchungu. Kwa baadhi ya akinamama
uchungu kwao ni jambo gumu lisiloelezeka, wakati kwa wengine
uchungu ni maumivu ya kawaida.

Kabla kipindi hakijachanganya, unaweza kujisikia kubanwa
na misuli ambayo huchukuwa kiasi cha kati ya sekunde 15 hadi 20,
na kinarudia tena kila baada ya dakika 10. Kipindi hiki hujulikana
kama uchungu usio wa kweli. Wakati mtoto anapokuwa tayari kwa
kuzaliwa, mji wa mimba huanza kuwa mwembamba. Kutokana na
hali hii mtoto hujinyoosha na kuweka shinikizo katika mlango wa
uzazi. Yawezekana kukawa na kuvuja kwa ute wenye
kuchanganyika na damu kwenye uke wako, hii ina maana kuwa
mlango wa mimba unaanza kunyooka, au kutanuka, haya ni
maandalizi ya njia ya mtoto kupita.
Kwa baadhi ya wanawake, chupa hupasuka. Hii inajulikana
kama ‘kuvunjika kwa chupa.’ Inaweza kusababisha kuchuruzika
kwa maji, au kumwagika maji mengi. Kubanwa kwa misuli
kunaweza kutokea (kiasi cha sekunde 40 bila tukio), na kubanwa
huko kwa misuli kunaongezeka maradufu kadri mji wa mimba
unavyojivuta na kusukuma mtoto chini, wakati mlango wa mimba
unaposukuma juu na nyuma.
Kuzaliwa kwa mtoto kunaweza kuchukua kati ya saa moja
hadi masaa 14 pengine zaidi ya hapo. Mtoto wa kwanza kwa
kawaida huchukua kiasi cha saa 14; watoto wengine wataokuja
kuzaliwa baadaye na mama huyo watachukua kiasi cha saa nane.
Kiasi cha maumivu hutofautiana baina ya wawawake.
Kuzaliwa kwa mtoto si rahisi kwake pia Pumzi ya kwanza
ya mtoto ni ngumu sasa kwake; inaweza kufananishwa na mtoto
kupuliza pulizo. Mtoto mchanga anapaswa kutumia nguvu mara
tano zaidi kuliko kawaida kuvuta hewa ndani ya mapafu yake
madogo. Wakati kiunga mwana (umbilical cord) kinapotoka na
kukatwa, hapo ndipo mwisho wake wa kufanya kazi. Sasa mtoto
anajitegemea kwa mahitaji yote.
Miezi Mitatu ya Mwanzo
Mtoto
Katika muda wa majuma sita, kiinitete (embryo), ambacho
huanza kukua kinaanza na kichwa kuelekea chini, huwa na fuvu
ambalo lina macho yaliyo katika hatua za awali na masikio,
ingawaje wakati huo kiumbe hiki huonekana zaidi kuwa kama
kijisamaki kidogo chenye kichwa kikubwa kuliko umbo la mtoto wa
binadamu. Kiumbe hiki japo bado kina vipimo kama chembe ya
mchele, ukubwa wake ni mara 10,000 zaidi kuliko yai lilipoungana
na mbegu za kiume, na ukubwa inaongezeka mara mbili kila juma.
Kiumbe hiki tayari huwa na ubongo, figo, ini, mfuko wa kuyeyusha
chakula, mkondo wa damu, moyo uliogawanyika katika sehemu
mbili unaopiga piga na vichipukizi vifupi ambavyo baadaye hukua
na kuwa mikono na miguu. Kiumbe hiki ambacho huitwa kiinitete
kina matendo hiari ambayo hujitokeza yenyewe hasa katika juma
la saba japokuwa wewe huwezi kusikia kinapo jirusha.
Waweza kutambua sura ya kiumbe hiki kuwa ni sura ya
binadamu katika kipindi cha juma la nane. Kichwa kinakuwa ni
kikubwa kuliko kiwiliwili. Macho huzibwa na ngozi ambayo
baadaye hugawanyika na hutengeneza kope. Mikono, miguu
huanza kujitokeza na kukua, nazo mbavu huchomoza. Kiumbe
hiki huwa pia kina mifupa ambayo iko katika hali ya ulaini (kama
unavyoweza kuhisi ncha ya pua yako ukiigusa). Viungo vya uzazi
ambavyo ni vidogo sana huanza kuonekana japokuwa siyo rahisi
kutambua mtoto huyu anaweza kuwa wa kike au wa kiume. Uzito
wake ni chini ya ule wa kidonge cha aspirini!
Mama
Dalili ya kwanza ya mabadiliko ya ujauzito hutambuliwa
katika matiti yako – huanza kuvimba na ile sehemu ya chuchu
inayoonekana rangi ya udongo huanza kuwa nyeusi. Matiti yako
huanza kuwa laini na mazito. Mwili huanza kuwa mzito na mchovu
wakati unapokuwa unaanza kujirekebisha tayari kupokea maisha
mapya katika mwili wako hasa kama ni mimba yako ya kwanza


Vitu vingi hutokea ndani ya mwili wako katika miezi hii ya
mwanzo, hata hivyo huwa ni kwa kiasi kidogo sana kiasi
kwamba wanawake wengi ‘hawaonyeshi.’
Wanawake wengi wanaweza kupata ‘ugonjwa wa
asubuhi’ – kichefuchefu – ambacho kinaweza kutokea wakati
wowote katika siku. Unaweza kuondoa hali hii ya
kichefuchefu kwa kula chochote mara tu baada ya kuamka
asubuhi. Ili kuzuia kichefuchefu ambacho kinaweza kutokea
wakati wowote wakati wa mchana, hakikisha unapumzika vya
kutosha kwa kuwa uchovu unaweza kuchangia katika
kukuletea kichefuchefu. Njaa pia yaweza kusababisha
kichefuchefu, hivyo ili kukizuia, pata vitu vidogo vidogo vya
kutafuna wakati wa mchana.
Katika miezi hii mitatu ya mwanzo ya ujauzito mjamzito
huwa na jazba (hasira) sana. Jazba hizi pengine
husababishwa na mabadiliko katika vichocheo ambayo
hukufanya ujisikie vibaya pamoja na kichefuchefu. Ya
kupasa pia kujirekebisha kisaikolojia (kihisia) ukijichukulia
kuwa unaye mtoto ndani yako na majukumu mapya ambayo
utayapata si tu baada ya kuzaliwa mtoto bali hata kabla.
Lishe bora, kama ambavyo tumekwisha taja hapo
mwanzo, ni moja ya wajibu wa kuchukua kabla mtoto
hajazaliwa, kwa sababu mimba husababisha ongezeko katika
mahitaji yako ya vitamini na madini. Pale tu unapojihisi kuwa
umepata mimba, unapaswa kula chakula chenye lishe bora,
kwani chakula ulacho huchangia katika makuzi na maendeleo
ya mtoto. Madaktari wengi hutoa maelekezo ya matumizi ya
multi-vitamini au madini ambayo yametengenezwa maalum
kwa ajili ya mama wajawazito na watoto walioko tumboni.
Lakini ni muhimu zaidi kupata lishe bora wakati wa ujauzito
kuliko kumeza vidonge hasa miezi mitatu ya mwanzo kwa vile
katika kipindi hiki viungo vya uzazi vya mtoto ndio
vinatengenezwa. Protini huhitajika zaidi kwa mtoto
anapoendelea kukua na vyakula vingine vya kulikuza.
Proteini inayotokana na vyakula vya asili (yaani vinavyotoka
mashambani) hutengeneza viini viitwavyo ‘amino acid’
ambavyo huleta uhai ndani ya mwili, umuhimu wa protein ni


Wiki yaKumi

· Tumbo la uzazi lina vipimo kama chungwa,
lakini bado huwezi kusikia kwa kupima
tumboni.

· Kondo inatengeneza kichocheo cha
progesterone kuwezesha mimba kuendelea.
Mtoto ana vifundo vya miguu na mikono.
Ana sm 4.5.


Wiki yaKumi naMoja
· Utaanza kupona kwa hali ya kutapika. Kiasi
cha damu yako inaongezeka kutoka sasa
mpaka wiki ya 30.
· Mtoto ana ovary au pumbu zake, na
inaonekana kama ni wa kike au wa kiume.
Sasa, mwili wa mtoto karibu umekwisha
tengenezwa -- Sasa unahitaji kukua tu.


Wiki ya Kumi naMbili
· Unaanza kusikia tumbo la uzazi tumboni.
· Mtoto ana nyukope. Ana cheza zaidi
tumboni, na anajinyosha, kupiga miayo,
jinyonganyonga vidole vyake. Ana sm 6.5
na ana uzito wa 18g.


Wiki yaKumi naTatu
· Hutatapika tena kwa sababu ya mimba.
· Mtoto anaendelea kuongezeka vipimo
vyake. Ana sm 8.5 na uzito wa 28g.


Wiki ya Kumi naNne
· Kuchoka kumepungua kidogo. Unaanza
kujisikia na afya nzuri. Chuchu za matiti
zinaweza kuwa nyeusi zaidi.
· Mtoto ana nyushi na nywele kidogo.
Anakunywa maji ndani ya chupa ya uzazi
na kukojoa.
Kumi na 

Wiki ya Kumi naTano
· Utaanza kuona nguo zinabana kidogo.
Moyo wako umeongezeka nguvu wake
kwa asilimia 20.
· Nywele za mtoto zinaongezeka na kuwa
nyeusi kabisa. Anajaribu kunyonya
vidole vyake.


Wiki ya Kumi na Sita
· Unaanza kuweza kusikia mtoto akicheza
tumboni.
· Mifupa ya mtoto inaanza kuwa migumu.
Ana ulaika juu ya mwili wake wote. Ana
kucha za vidole. Angeweza kulala ndani
ya kikombe cha chai; ana vipimo kama
mkono yako. Ana sm 16 na 135g.

Ukuaji wa haraka haraka wa mtoto utakupunguzia nguvu
zako, hivyo jishibishe kwa chakula kingi chenye wanga, matunda
na mbogamboga. Usisahau vyakula vya mafuta, vyakula hivi huwa
vimejaa nishati iletayo nguvu mwilini. Mafuta pia yanakusaidia
kufyonza virutubishi, lakini kumbuka pia, mafuta yanaweza

kutengeneza calori. Mafuta yaletayo afya sana mwilini mwako ni
pamoja na yale yatokanayo na tende, karanga, mahindi, soya na
alizeti); mengine hutokana na korosho, mizeituni, njugu na
karanga. Vyakula vyenye protini pia vina mafuta, nyama, samaki,
maziwa na vyakula vyenye kutokana na maziwa kama vile jibini,
siagi ya karanga vyafaa sana
.

Miezi Mitatu ya Awamu ya Mwisho
Mtoto
Katika majuma ishirini na nane, mtoto huwa amekuwa sana
kiasi kwamba hawezi kujisogeza ndani ya tumbo lako. Ingawaje
siku zake za kujibinua huwa zimemalizika, anakuwa anatumia
muda mwingi kujinyonya dole gumba lake.
Nywele zake huwa zimerefuka. Wakati wa mwezi wa nane

(kuanzia juma la 32 hadi la 36) mtoto huongezeka uzito wake kwa
900g, uzito huu huchangiwa na mafuta ya kinga.
Kipindi fulani ndani ya kipindi cha mwisho cha ujauzito (kati
ya wiki ya 36 na ya arobaini), mtoto hujigeuza na kujituliza chini

katika nyonga, kichwa chake kikiwa kimegota sawasawa ndani ya
misuli ya nyonga zako. Hii ina maana kuwa mtoto tayari
anajiandaa na ana hamu ya kuzaliwa na wewe. Inapofika juma la
arobaini, au muhula, ukuaji wa mtoto kabla ya kuzaliwa huwa
umekamilika. Mtoto anakuwa shupavu mwenye urefu wa kati ya
sm 45 na sm 53. Mzito wa kati ya 2.5kg na 4.5kg



0 comments:

Post a Comment