Tuesday 19 August 2014

MAAJABU YA MIMBA HONGERA KWA KUPATA MIMBA PARTI-5

Wiki yaIshirini naNne
· Daktari ataweza kusikiliza moyo wa mtoto
tumboni.
· Mtoto ana sm 32 na 500g. (vipimo kama
risiva ya simu) Mapafu yake bado hayawezi
kuhema nje, lakini mafigo, ini na kadhilika zipo
tayari. Labda anapenda kusikiliza musiki.

Wiki yaIshirini naTano
· Labda utapata shida ya kulala usingizi.
Unaweza kutaka kukojoa mara nyingi
· Nafasi ya mtoto inaanza kupungua.

Wiki yaIshirini naSita
· Tumbo la uzazi linaongezeka kwa sentimeta
moja kila wiki.
· Ngozi ya mtoto inaanza kuwa nzito zaidi --
huwezi kuona ndani ya mwili wake sasa.

Wiki yaIshirini naSaba
· Unaweza kuanza kutoa mwanzo wa maziwa
kutoka kwa matiti.
· Mtoto anaweza kufungua macho yake.
Anaweza kuona mwanga na giza.

Wiki yaIshirini naNane
· Utaongeza uzito wako mpaka wiki ya 36.
Tumbo la uzazi limefika kati ya utovu na kifua.
· Mtoto ana sm 38 na 900g

Wiki yaIshirini naTisa
· Unaanza kujisikia kama hakuna nafasi zaidi
tumboni.
· Ubongo wa mtoto inaendeleza zaidi. Anasikia
vizuri.

Wiki yaThelathini
· Jaribu kuweka miguu juu unapokaa.
· Mikazo ya tumbo la uzazi inaanza kubana
mtoto ingawa huwezi kusikia bado. Moyo
wake inapiga kati ya mara 120-160 kila
dakika.


Wiki yaThelathini na Moja
· Unaweza kukosa pumzi ukipanda mlima au
kubeba mizigo.
· Mtoto ana 1.8kg.


Wiki yaThelathinina Mbili
· Unasikia uzito wa tumbo lako.
· Mtoto anaweza kuwa na kwikwi. Ana sm 42.
Bado anahitaji kunenepa.
· Ujisikie mtoto akicheza tumboni isipungua mara
10 kwa siku.

katika utengenezaji wa mkusanyiko wa seli mucilini na viungo vya
mtoto hasa wakati huu wa mwanzo kabla ya mtoto kuzaliwa kuliko
wakati mwingine wowote wa uhai wake.
Baadhi ya vyakula vyenye asili ya protein kama vile
maharage makavu na vile vya jamii ya njegere, (choroko, dengu,
mbaazi na kunde), mbogamboga, nafaka na ngano havina amino
acids iliyo na uwiano sawia hivyo huitwa ‘protini isiyokamili.’
Vyakula hivi vikiliwa peke yake havikupi thamani halisi ya protin.
Hivyo, wakati wa ujauzito unashauriwa kula chakula kilicho na

protini ya kutosha kama vile samaki, kuku, nyama ya minofu isiyo
na mafuta, maziwa, jibini viliwe pamoja na jamii ya kunde.
Mbali na mahitaji yako kuongezeka kuhusiana na protini,
ujauzito unaongeza mahitaji ya lishe zenye madini ya chuma,

madini ya chokaa (calcium), vitamin A, C, D, E, B6, B12, thiamini,
riboflavin, niacin, fosiforasi na magnesium. (Kwa orodha kamili ya
vyakula vilivyopendekezwa, angalia kiambatisho). Wewe na mtoto
wako aliye tumboni mnahitaji zinki ambayo ni ya muhimu katika
kuunganisha protini na madini joto kwa sababu huathiri kikoromeo
cha mtoto, ambacho ndicho huanza kutengenezwa katika miezi ya
mwanzo ya ujauzito.

Ni muhimu kwenda kliniki ya akinamama wajawazito mara
unapojihisi kuwa na mimba. Wakunga wanaweza kuhakikisha
kwamba mimba inaendelea vizuri. Pia ni muhimu kipimwa damu
yako wadudu wa kaswende. Wadudu hawa wanaweza
kusababisha mtoto kufariki tumboni wakati wowote mpaka azaliwe,
lakini mara nyingi wewe huna dalili zozote za ugonjwa. Kaswende
inatibika kwa urahisi.

Miezi Mitatu ya Awamu ya Pili
Mtoto

Katika majuma kumi na mbili, kiinitete (embryo) hubadilika
na kuwa ‘kimjusi’ (fetus) na mnaweza kutambua kama ni
mvulana au msichana. Uso wa mtoto huanza kutakata na
kupendeza. Anaanza kuwa na ala za sauti (midomo, ulimi)
kama kungekuwa na hewa ndani ya tumbo sauti ya mtoto

ingesikika akilia. Wakati huu mtoto anakuwa na uti wa mgongo
na moyo ulio na vyumba vinne kama mtu mzima. Siyo tu
kwamba mtoto anaweza kupiga mateke, anaweza pia kupindisha
vidole vyake. Katika majuma kumi na sita, baadhi ya wamama
wajawazito huweza kugundua mwendo wa mtoto, kama vile
kupigapiga kama kuchezacheza ambako kunaelekea

kutambulika wazi kuwa ni mateke na kuruka kwa kusogea
mbele. Mtoto hufunikwa na vinyweleo, ambavyo baadaye
hubanduka (hunyumbuliwa). Katika mwezi wa nne mtoto hukua
na kurefuka kufikia kati ya sm 20 hadi sm 25, au tuseme urefu
wake huongezeka kama nusu ya ule atakaozaliwa nao. Uzito
wake utaongezeka mara sita japokuwa kwa sasa hivi uzito wake
utabaki kama 150g tu.

Katika juma la ishirini na nne, mtoto anakuwa na urefu wa
sm 30 na anakuwa amefunikwa na ute mzito ambao
hushikamana na vinyweleo, kazi ya ute huu ni kumlinda mtoto.
Watoto wengi huzaliwa wakiwa bado wamefunikwa na ute huu

mzito katika ngozi zao nyororo. Si tu kwamba wewe unatambua
jinsi mtoto anavyochezacheza, bali hata yeye hutambua wewe
unavyotembea na mazingira yanayokuzunguka. Mitetemeko,
sauti kubwa ya muziki au mitetemo zinaweza kumwamsha.
Katika mwezi wa sita, mtoto anaweza kufungua macho na
kuangalia vitu vinavyomzunguka. Hakika huyu ni mtu mdogo.

Mama

Katika awamu hii ya pili ya ujauzito wako, baadhi ya
mambo ya ajabu sana yatatokea. Utagundua kuwa miezi hii
mitatu awamu ya pili utajisikia kuwa na nguvu na kujisikia vizuri.
Kujisikia huku vizuri kimwili na kihisia, kunaweza kusababishwa
na kupungua kwa hali ya kujisikia kichefuchefu. Mwili wako na


Wiki yaThelathinina Tatu
· Ujisikie mtoto akicheza tumboni isipungua mara
10 kwa siku.
· Mtoto analala kichwa chini mpaka azaliwe.

Wiki yaThelathinina Nne
· Nusu ya uzito ambao umeongeza ni mtoto,
kondo na maji – nusu ni mwilini wako ili uwe na
akiba ya kunyonyesha mtoto.
· Mtoto anaona mwanga ukitoa nguo


Wiki yaThelathinina Tano
· Unaweza kuzidi kuota ndoto usiku. Labda
mgongo utaumwa.
· Mtoto ana sm 44 na 2.5kg.

Wiki yaThelathinina Sita
· Mtoto atatelemka chini kidogo -- tumbo
linapungua kidogo, lakini sehemu za siri
inaanza kusikia kubwa. Kukosa pumzi kutatulia
kidogo, lakini utataka kukojoa mara nyingi.
· Mtoto ni karibu tayari kuzaliwa.


Wiki yaThelathinina Saba
· Utapata shida kulala vizuri usiku.
· Mtoto anajizoea kuhema tumboni, ingawa yuko
majini. Pumbu za mtoto wakiume zitakuwa
zimetelemka kufika mfuko zao.

Wiki yaThelathinina Nane
· Mtoto anapunguza kucheza kwa sababu ya
nafasi ndogo. Lakini bado umsikie zaidi kuliko
mara 10 kwa siku.
· Mtoto anaongeza uzito wake 28g kwa siku.

Wiki yaThelathinina Tisa
· Unajisikia uzito sana na kuchoka.
· Maji tumboni la uzazi yanabadilishwa kila
masaa matatu. Matumbo ya mtoto yamejaa
majimaji yenye rangi ya kijani au meusi. Ulaika
wake umekwisha kutoka.


Wiki yaArobaini
· Mishipa wako imelainisha kidogo tayari
kuruhusu mtoto azaliwe. Mgongo unaweza
kuumwa.
· Mtoto yuko tayari kabisa kuzaliwa


0 comments:

Post a Comment