Monday, 25 August 2014

KUMTIBU MTU MWENYE MARADHI YA KWIKWI, MAZIWA YA MAMA KUONGEZEKA NA MARADHI YA MBA

Kama umeshikwa na kwikwi na inakusumbua kwa muda mrefu, chukua maji yaweka kwenye glasi kisha chukua taulo, yafunike na uyanywe kwa kuyachuja na taulo hilo mpaka yaishe.
Maji hayo yakiisha  na kwikwi yako itakuwa imekwisha mara moja.
***
Uwatu  ‘Fenugreek’ husaidia kuongeza maziwa kwa mama.
Pamoja na kutibu magonjwa mbalimbali kama kupunguza cholesterol mwilini na kushusha sukari kwenye damu, mbegu au majani ya uwatu yanasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza maziwa kwa mama ambaye hana maziwa ya kutosha kwa mtoto aliyezaliwa.
Mama anatakiwa kuhakikisha anakunywa kikombe cha chai kila siku kwa ajili ya kupata maziwa, ni tiba ya haraka sana, kama ataona maziwa yamemtosha anaweza kuacha

Angalizo
Ni tiba nzuri lakini ukinywa kwa wingi husababisha gesi tumboni kwa mama na mtoto, hivyo unatakiwa kuwa mwangalifu katika unywaji
Pia, akina mama walio na tatizo la kisukari hawaruhusiwi kunywa tiba hii kwani inapunguza sukari mwilini kwa asilimia kubwa sana
***
Tumia ‘aloe vera’ kuondoa mba kichwani
Kwa wale wenye tatizo la mba kichwani, mmea wa aloe vera ni tiba tosha kwani unasaidia kwa asilimia kubwa sana kuondoa mba.
Chukua jani moja la aloe vera, chuja maji yake kisha paka kwenye ngozi usiku kisha lala. 
Ukiamka asubuhi osha nywele zako kwa shampoo, kausha,  chukua mafuta paka chini kwenye ngozi yako ili isikauke kwani kukauka kwa ngozi ndiyo chanzo cha mba wa kichwani.

Tumia ‘apple’ kutibu tatizo la ukosefu wa choo ‘Constipation’
Kama una tatizo la kukosa choo, pendelea kula tunda la tufaha ‘ apple’  kila siku tatizo lako litakwisha mara moja.
Tunda hili lina uwezo wa kutengeneza majimaji yanayolainisha chakula tumboni kuliko papai.
Ukweli ni kwamba tufaha lina nafasi kubwa ya kutibu kuliko papai, hebu jaribu leo.

0 comments:

Post a Comment