Tuesday, 12 August 2014

DALILI YA MTU MWENYE UPUNGUFU WA DAMU MWILINI



Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za da damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali seli mundu, ujauzito, hedhi nzito, kurithi, magonjwa sugu na Lishe duni yenye ukosefu wa madini ya folic, chuma na vitamini B12.

Dalili zifuatazo zinakuwezesha kutambua kama una tatizo la upungufu wa damu hivyo kukusaidia kuwahi hospitali au kubadili mfumo wa chakula ili kuepuka madhara makubwa ya baadae.
  • Kushindwa kupumua vizuri
  • Vidonda kwenye ulimi au mdomoni
  • Sehemu nyeupe ya jcho kuwa bluu
  • Ngozi kuwa na rangi ya kijivu
  • Kucha kuwa dhaifu
  • Kusikia hasira na kuhamasika haraka
  • Kuchoka sana kuliko kawaida
  • Maumivu makali ya kichwa
  • Kupungua kwa uwezo wa kufikiria
  • Kusikia kichwa chepesi pale unaposimama
  • Miguu na mikono kuwa ya baridi sana
  • Uchovu wa mara kwa mara
MATIBABU 
Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya Chuma kutokana na visababishi vya tatizo. Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizi huweza kutumika hosipitali ambamba na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko katika hali mahututi huweza kuongezewa damu.

Related Posts:

  • USICHOKIJUWA KUHUSU GAUTI (GOUT) NA MADHARA YAKE MWILINI                                  Ukitembea katika jamii hasa mijini utawasikia watu wengi hasa wanaume wanapokunywa bia na kula supu … Read More
  • MATATIZO KATIKA UZALISHAJI WA MBEGU ZA KIUME Matatizo katika uzalishaji  wa mbegu za kiume huwatokea wanaume na ni chanzo kikuu cha kutopata watoto kwa wanandoa au watu walio katika mahusiano na wanatafuta mtoto. Hili pia ni tatizo la ugumba  kwa … Read More
  • UJUE UGONJWA WA DENGUE SIKU chache zilizopita Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini ilitoa taarifa kuhusu kuwapo ugonjwa wa homa ya dengue. Hadi asubuhi ya Jumanne iliyopita mpaka sasa wagonjwa wapatao 37 walikuwapo nchini Tanzania … Read More
  • MALARIA UGONJWA UNAOWAUMIZA VICHWA WANASAYANSI Malaria ni ugonjwa unaoathiri watu wengi duniani ikiwamo Tanzania.  Ugonjwa huo husababisha vifo vya watu milioni 2.7 kote duniani, ambapo vifo vingi hutokea barani Afrika. Ugonjwa wa malaria huonekana katika … Read More
  • UFAHAMU UGONJWA WA UKOMA Ugonjwa wa ukoma unaambukiza, kama mtu ataambatana na mtu mwenye ugonjwa huo kwa muda mrefu sana, na ambaye hajapatiwa matibabu, mtu huyo inawezekana naye akaambukizwa ugonjwa huo.  Dalili: Dalili za ugonjwa huu… Read More

0 comments:

Post a Comment