Friday, 4 July 2014

MAMBO YA KUYAFAHAMU JUU YA MARADHI YA KANSA (CANCER)



                     
     1
Kuna zaidi ya aina 100 za saratani,na kiungo chochote cha mwili kinaweza
kuathirika
                             2
Asilimia 70 ya vifo hutokea katika nchi zenye kipato kidogo na cha kati

                              3
Aina 5 za  kansa zinazosababisha vifo  duniani kote ni : mapafu, tumbo, ini, utumbo mpana na koo
                               4
Matumizi ya tumbaku ni mojawapo ya sababu kubwa  inayosababisha  kansa duniani ambayo huzuilika   na husababisha 22% ya vifo ya vyote vya kansa
                                5
Moja ya tano ya saratani duniani kote yanatokana na maambukizi sugu, kwa mfano human papillomavirus (HPV) husababisha kansa ya kizazi na hepatitis B virusi (HBV) husababisha kansa ya ini.
                                  6
Baadhi ya Saratani  mfano matiti, kizazi na kansa ya utumbo mpana zinaweza kutibiwa na kupona  kama zitagundulika mapema na kutibiwa vya kutosha.
                                  7
Wagonjwa wote wenye haja ya kutuliza maumivu wanaweza kusaidiwa kama elimu ya sasa kuhusu kudhibiti maumivu  na huduma ya  faraja itatumiwa kikamilifu
                                  8
Zaidi ya 30% ya kansa zinaweza kuzuiwa, hasa kwa kuacha kutumia tumbaku,  lishe bora , kufanya mazoezi na  kudhibiti matumizi ya pombe. Katika nchi zinazoendelea hadi 20% ya vifo vya kansa yanaweza kuzuilika kwa chanjo dhidi ya maambukizi ya HBV na HPV.

0 comments:

Post a Comment