Kimeta ni ugonjwa wa hatari unasababishwa na vimelea vya bacteria. Bacteria hawa hujulikana kama Bacillus anthracis,bacteria ambao wana uwezo wa kufanya mbengu.Mbegu hizi ni seli ambazo huweza kukaa kwa miaka kadhaa (karne na milenia) hata katika mazingira magumu zikiwa zimelala na huweza kurudia hali ya uhai pale zinapopata mazingira ya kufaa.
Kuna aina tatu za kimeta kulingana na eneo la mwili lililoathiriwa. Ugonjwa huu unaweza kuathiri ngonzi,mapafu na njia ya chakula.
Unapataje maambukizi?
Kimeta hakiambukizwi kati ya mtu na mtu
Kutoka kwa wanyama.
Binadamu huweza kupata maablmbukizi toka kwa wanyama iwapo watagusana na mazao ya wanyama waliothirika na ugonjwa huu au kuvuta mbegu au kula chakula ambacho hakikuva vizuri kutoka kwa mnyama alieathirika.
Kimeta kama silaha.Kimeta pia kimehusika j ugaidi.Mwaka 2001 kimeta kilitumiwa nchini marekani na kusababisha vifo.Kutokana na ukweli kwamba kimeta huwezwa kuzalisha maabara ,imekuwa silaha ambaye imekuwa ikitumiwa na magaidi.
Hatari ya ugonjwa huu inategemea sehemu ilipoathirika. Maambukizi kwenye mapafu husababisha kifo kwa kiasi kikubwa.Maambukizi kwenye matumbo ni hatari pia kwani huweza kusabibisha vifo kwa nusu wagonjwa waliopata maambukizi.Maambukizi ya ngozi hayasababishi vifo kwa kiasi kikubwa kwani asilimia 80 ya wagonjwa hupona hata bila kupata tiba yoyote.
Dalili za kimeta
Dalili hutofautiana hasa kulingana aina ya ugonjwa
Maambukizi ya ngozi: Dalili ya awali ni Kipele kidogo ambacho hufanya lenge. lengelenge hili baadae hufanya kidonda chenye weusi katikati.Vitu hivi vyote haviumi
Njia ya chakula: Dalili za awali ni Kichefuchefu,kukosa hamu ya chakula, Kuhara damu,homa ikifuatia na maumivu makali ya tumbo.
Njia ya hewa: Dalili za awali hujitokeza kama dalili za mafua, maumivu ya misuli,pamoja na homa. Baadae dalili zingine hujitokeza kama kikohozi, pumzi kubana na uchovu.
Dalili hujitokeza ndani ya siku saba tangu mgonjwa akutane na bacteria. Pia dalili baada ya kupata maambukizi ya njia ya huweza kujitokeza ndani ya wiki moja au hata baada ya majuma sita.
Matibabu ya Kimeta
Antibiotics hutumika katika matibabu ya aina zote tatu za ugonjwa huu. Utambuzi wa awali pamoja na matibabu ni muhimu.
Kukinga baada ya kuambukizwa
Matibabu ni tofauti kwa mtu ambae amepata maambukizi ya kimeta lakini hajaanza kuugua. Wahudumu wa afya hutoa dawa za antibiotics mfano ciprofloxacin au doxycycline pamoja na chanjo.
Matibabu baada ya maambukizi
Treatment after infection.
Kwa kawaida matibabu huchukua siku 60. Mafanikio hutegemea aina ya ugonjwa na muda wa kuanza matibabu.
Kinga.
Kuna kinga ya kuzuia ugonjwa wa kimeta katika nchi zilizo endelea lakini kwa sasa inatolewa kwa watu walioko kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi.
Kinga.
Kuna kinga ya kuzuia ugonjwa wa kimeta katika nchi zilizo endelea lakini kwa sasa inatolewa kwa watu walioko kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi.
0 comments:
Post a Comment