Sunday, 8 June 2014

TIKITIMAJI CHUNGU ZINASAIDIA KUZUIA KENSA YA MATITI



Utafiti mpya umegundua kuwa mada zinayotokana na tikitimaji ambazo ni mboga mboga zinazopatikana sana India, China na Amerika ya Kusini zinaweza kusaidia kuwaepusha wanawake na kensa ya matiti. Kwa mujibu wa uchunguzi huo uliochapishwa kenye jarida 

la Utafiti wa Kensa, majimaji (extract) yanayotolewa katika tikitimaji chungu yanayojulikana kama 'karela' kwa kihindi yanaweza kupunguza kasi ya kukua kwa seli za kensa ya matiti 
au hata kuua kabisa seli hizo. Ratna Ray aliyeongoza uchunguzi huo anasema kwamba, 

tikitimaji chungu zina uwezo wa kuzuia kensa na kuchelewesha kutokea ugonjwa huo wa saratani ya matiti, lakini bado haijathibitika iwapo mboga mboga hizo zinaweza kutibu ugonjwa huo.
Wanasayansi wanasema kuwa uchunguzi zaidi unapaswa kufanywa ili kuhakikisha uwezo na usalama wa tikitimaji chungu kuhusiana na suala hilo. Ratna Ray aidha anasema kuwa, kutumia lishe asilia ni suala linalopewa umuhimu mkubwa hivi sasa na sayansi katika 

kuzuia ugonjwa wa saratani ambao umekuwa ukiongezeka siku baada ya siku. Mtaalamu huyo vilevile amesema, katika siku za usoni watafanya uchunguzi utakaowahusisha watu wengi zaidi walio na hatari ya kupata kensa ili kuona iwapo tikitimaji chungu zitawazuia wasipate ugonjwa huo au la.
Kwa muda mrefu tikitimaji chungu ambazo zina Vitamin C na mada ya flavonoid zimekuwa zikijulikana kwa kuwa na uwezo wa kuzuia kisukari na kupunguza kiwango cha sukari katika damu.

Related Posts:

  • FAIDA ZA KIAFYA ZITOKANAZO KWA ULAJI WA TENDE Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, tende ndiyo tunda linaloliwa kwa wingi, pengine kuliko tunda lingine. Pamoja na kuwa ni tunda lenye ladha tamu na nzuri mdomoni, lakini kisayansi pia limethibitika kusheheni madini … Read More
  • FAIDA ZA KUTUMIA JUICE YA TANGAWIZI AU CHAI YA TANGAWIZI Katika miaka 500 iliyopita tangawizi ilianza kutumika mashariki ya mbali, kama vile China na India wakitumia kwa kutibu maradhi mbali mbali. Katika hili zao la tangawizi kuna vyanzo vya: Mangenisium Mangne… Read More
  • JUISI NA FAIDA ZAKE MWILINI LEO nitaongelea faida za kunywa juisi katika mwili wa binadamu.Kuna  juisi za aina mbalimbali na matumizi yake yanategemea na malengo ya mtumiaji. Inawezekana watumiaji wengi wanakunywa juisi bila kujua umuhimu au kaz… Read More
  • UMUHIMU WA KUNYWA MAJI YA LIMAO KILA ASUBUHI. UMUHIMU WA KUNYWA MAJI YA LIMAO KILA ASUBUHI. 1.Huongeza Kinga yako ya mwili hasa kupambana na magonjwa madogo kama mafua, na kikohozi kutokana na kuwa na vitamin C 2. Husafisha Mfumo wako wa chakula, ku… Read More
  • ZIJUE FAIDA ZA NDIZI KATIKA MWILI WA BINADAMU! TOFAUTI na vyakula vingine, ndizi zinafaida kubwa sana katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa wataalamu wa lishe, ndizi zina virutubisho vya aina mbalimbali kama vile, protini, mafuta, kalishiamu, wanga, fosiforas, mad… Read More

0 comments:

Post a Comment