Sunday 8 June 2014
SIRI ZA KASI YA MBEGU ZA KIUME ZAGUNDULIWA!
Wataalamu wanasema wamegundua kwamba mbegu za kiume huanza kwenda kwa kasi wakati zinapofika karibu na yai la mwanamke, suala ambalo huenda siku zijazo likasaidia katika kupatikana dawa ya kuzuia mimba ya wanaume. Vitundu vidogo vilivyoko juu ya mbegu hizo za kiume huziwezesha
kubadilisha PH yake ya ndani, ambayo hufanya mkia wa mbegu hizo uanze harakati. Wataalamu hao wa Chuo Kikuu cha California huko San Francisco wanasema kuwa, ugunduzi huo unaweza pia kusaidia kuelezea kwa nini marijuana huwafanya wanaume wawe tasa na kwamba suala hilo litaleta mabadiliko makubwa katika kufahau suala zima la uwezo wa kuzaa wa mwanaume.
Kwa kawaida mbegu za wanaume hazianzi kwenda mbio baada tu ya kumwagwa, na ili kuweza kulifikia yai la mwanamke huhitajia kujiepusha na kasi hadi pale zinapokaribia yai. Wanasayansi kwa muda mrefu wamekuwa wakifahamu kwamba mwendo wa mbegu za kiume umekuwa ukisimamiwa na PH ya
ndani, na kuwa kwake katika hali ya asidi au alikali lakini walikuwa hawafahamu ni jambo gani hasa linalowezesha kubadilika PH hiyo. Wataalamu wamesema, sasa wamejua kuwa ili kuongeza PH ili iwe ya alkali, mbegu huhitajia protoni zinaoitwa Jettison, na kwamba wamegundua vijitundu vidogo vilivyoko
juu ya mbegu hizo ndio huruhusu mabadiliko hayo. Daktari Yuriy Kirichok aliyeongoza utafiti huo anasema, iwapo utafungua vijitundu hivyo, protoni inatoka nje, na wao wamefahamu molekuli ambazo huruhusu protoni hizo zitoke nje. Anaendelea kueleza kwamba, vijitundu hivyo vilivyopewa jina la Hv1
proton Channels, hufunguka pale inapofikia wakati muafaka wa kufunguka na hutegemea kitu kingine kinachoitwa, anandamine. Anandamide ziko katika mirija ya uzazi ya mwanamke katika eneo ambalo ni karibu na yai.
Katika marijuana kuna mada inaitwa cannabidoid ambayo inaaminika kuwa inapunguza uwezo wa anandamide, suala ambalo sasa limeweza kuelezea ni kwa nini marijuana kusababisha ugumba kwa wanaume. Dk, Kirichok anasema kwamba, marijuana pia huzipa kasi mbegu za kiume mapema, na
huzifanya ziungue baada ya masa kadhaa. Watafiti hao wanatupa moyo kwamba, kwa kufahamu vyema masuala hayo, sasa ni wazi kuwa wanaweza kutafuta dawa ya kuzuia mimba kwa wanaume. Kwani kwa kuziziba molekuli hizo, pengine wakafanikiwa kuzuia na kutoruhusu mbegu isikutane na yai, na njia hiyo ikatumika kama dawa ya kuzuia mimba kwa wanaume.
0 comments:
Post a Comment