Sunday, 8 June 2014

MAMA WAJAWAZITO WENYE KUONGEZEKA UZITO SANA WANA HATARI YA KUPATWA NA KISUKARI CHA MIMBA



Kina mama wenye mimba ambao huongezeka uzito kwa kasi katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito wanakabiliwa na hatari ya kupata kisukari cha mimba (gestational diabetes). Kifafa cha mimba ni hali ambayo wanawake ambao huko nyuma hawakuwa na ugonjwa 

wa kisukari huonekana kuwa na ongezeko la sukari katika damu kwa mara ya kwanza wakati wa ujauzito. Kwa mujibu wa uchunguzi mpya, mama wajawazito ambao wataongeza uzito wa gramu 403.70 kwa wiki wako katika hatari ya kupata kisukari cha ujauzito zaidi 

ikilinanishwa na wale watakaoongeza uzito wa chini ya gramu 272.15 kwa wiki. Bi. Monique Hedderson aliyeongoza uchunguzi huo amesema kuwa, ongezeko kubwa la mafuta ya mama mwanzoni mwa mimba kunaweza kukaathiri kwa kiasi kikubwa tishu za mwili na 

kuzifanya zisikubali insulin, jambo ambalo taratibu husababisha kisukari cha ujauzito. Kwa ajili hiyo wataalamu wameshauri kwamba, wakina mama wenye mimba hasa wale wanene na wenye uzito mkubwa wanapaswa wajiepushe na kuongezeka uzito mwanzoni mwa mimba ili wasipwatwe na kisukari cha mimba.

Sio vibaya kutambua kwamba, asilimia 4 ya kina mama ambao watapata kisukari wakati wa ujauzito wanakabiliwa na hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari baadaye maishani mwao, hiyo ikiwa ni pamoja na watoto wao. Kisukari cha ujauzito kina dalili kadhaa lakini kwa kawaida huainishwa kwa vipimo (screening) vinavyochukuliwa wakati wa ujauzito.

Related Posts:

  • DALILI ZA KUSAMBAA KWA KANSA YA TITI Wiki iliyopita tuliendelea kueleza matatizo ya kansa ya matiti, leo tunaelezea dalili za kusambaa kwa saratani hii mwilini.Kitendo cha kansa kusambaa mwilini kupitia mkondo wa damu na limfu huitwa metastasis.  Kusa… Read More
  • UGONJWA WA ZINAA WA TRICHOMONIASIS . Leo pia tutaendelea kuyajadili magonjwa ya zinaa ambapo tutazungumzia ugonjwa wa Trichomaniasis, ambao huwaathiri sana wanawake kuliko wanaume. I. Ugonjwa wa Trichomoniasis ni ugonjwa unaosababis… Read More
  • TATIZO LA UTOKWAJI MAJIMAJI MACHAFU KATIKA VIA VYA UZAZI VYA MWANAMKE-3 WIKI iliyopita tulijadili vyanzo vya tatizo hili linalowakabili wanawake wengi ambavyo ni maambukizo/mashambulio katika ya fangusi aina ya candida au bakteria aina ya chlamidia kwenye njia ya uzazi ya mwanamke, ulaj… Read More
  • TATIZO LA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA MWILINI Harufu mbaya ni kitu kisichompendeza mtu yeyote. Unapotoa harufu mbaya toka mwilini mwako, haikupendezi wewe mwenyewe wala mtu wa jirani. Kama kitu hukipendi wewe na ukakiona hakifai basi usimlazimishe mwenzio akipende a… Read More
  • TIBA YA SARATANI YA MATITI - 6 Tumekuwa tukielezea ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wiki tatu na hii ni sehemu ya mwisho nikiamini kuwa sasa wengi wameuelewa. Wiki iliyopita tulielezea tiba kwa kemikali na leo tunaendelea na tiba kwa njia ya homoni. … Read More

0 comments:

Post a Comment