Sunday, 29 June 2014

TATIZO LA UUME KUSINYAA




TATIZO LA UUME KUSINYAA

Mwanaume anayepatwa na tatizo hili anapokuja kujigundua huona kama mabadiliko makubwa yaliyotokea ghafla katika viungo vyake vya siri. Mwanamke mwenye tatizo hili pia naye huona kama tatizo geni linaloanza ghafla. 

Kwa kawaida hali hii hutokea katika umri mkubwa kwa mwanaume na mwanamke yaani kuanzia umri wa miaka hamsini lakini ikitokea katika umri chini ya miaka hamsini basi ni tatizo. Wapo vijana wenye matatizo haya ambayo vyanzo vyake tutakuja kuviona katika safu hii.

CHANZO CHA TATIZO
Hali ya kusinyaa kwa viungo vya uzazi kwa mwanamke na mwanaume hutokana na kuwepo kwa msukumo hafifu wa damu sehemu hiyo, maambukizi sehemu za siri ambayo huwa ya muda mrefu hasa kaswende, hitilafu katika misuli ya uke na sehemu za siri za mwanaume inayoathiriwa na kaswende virusi vya HIV, ugonjwa wa kifua kikuu na hata baadhi ya magonjwa sugu ya ngozi. Matatizo mengine yanayochangia hali hii ni ugonjwa wa kisukari.

Matatizo katika mishipa ya damu vilevile huweza kusababishwa na magonjwa ya moyo au mishipa ya damu inayosambaa sehemu hizo. Misuli inaposinyaa kwa mwanamke nayo huweza kusababishwa na magonjwa kama tulivyoona, uke unasinyaa pia huweza kusababishwa na uzazi wa mara kwa mara na karibu kufanya ngono mara kwa mara na wanaume tofauti na hitilafu katika mfumo wa homoni. 

Mwanamke anapata tatizo hili la kusinyaa uke endapo pia homoni au kichocheo cha Estrogen' kitakuwa kimepungua mwilini na kufanya mafuta yapungue ukeni. Kwa upande wa mwanaume homoni inayopungua kwa mwanaume ni Testosterone.

DALILI ZA TATIZO
Mwanaume mwenye tatizo hili hasa kijana, ingawa kwa wazee ni hali ya kawaida, kijana huanza kuona mfuko wa pumbu hulegea na kushuka sana, usinyaa na kujikunja kunja, kokwa huinekana ndogo na mishipa mikubwa ya damu huanza kujitokeza na mishipa mbegu toka katika kende huonekana wazi. Uume huwa kama wa mtoto mdogo na mishipa ya damu huchomoza wazi. Nguvu za kiume hupungua sana na endapo ukiweza tendo la ndoa la kwanza unawahi kumaliza na kushindwa kabisa kupata tendo la pili.

Mara kwa mara maandalizi kabla ya tendo la ndoa kwa mwanaume mwenye tatizo hili ni kuchezea sana uume kwa kuurusharusha au kuupiga piga kidogo kidogo ili kuamsha au kuhamasisha msukumo wa damu. Baada ya hapo uume huanza kusimama taratibu na endapo utasimama basi inabidi uwahi tendo na kama utachelewa, basi uume utalala na kushindwa tena kufanya tendo kwa siku hiyo. 

Mwanamke yeye daima huwa mkavu na wakati wa tendo hapati hisia zozote hadi tendo linapokwisha na kama mwanaume hana tatizo lolote na mwenye nguvu za kutosha basi mwanamke atapata michubuko na maumivu na kuhisi karaha ya tendo na hawezi kufika kileleni.

UCHUNGUZI
Tatizo hili kama tulivyoona husababishwa na magonjwa mbalimbali, pia yapo matatizo na magonjwa mengine yanyochangia hali hii, magonjwa kama kisukari, endapo ugonjwa utakuwa wa muda mrefu unaweza kuathiri hali hii. 

Tabia ya kujichua kwa mwanaume na mwanamke pia huweza kuathiri au kusababisha tatizo hili kama mtu atakuwa amejichua au kupiga punyeto kwa muda mrefu kwani msukumo wa damu sehemu za viungo vya uzazi utakuwa umeathiriwa.

Viungo vya uzazi vinaweza kupooza kutokana na hitilafu katika mishipa ya fahamu. Mishipa ya fahamu inapoathirika viungo hupooza (paralysis of genitalia) na mwanaume kushindwa kabisa kufanya tendo la ndoa na ukeni hakuna kabisa mawasiliano yanayoleta msisimko.

Vipimo vya damu na mkojo na vingine ambavyo daktari ataona vinafaa vitafanyika.

MATIBABU NA USHAURI
Tiba hutolewa kadiri daktari atakavyoona inafaa. Matibabu hutolewa katika kliniki za matatizo au magonjwa ya kinamama ambapo na kina baba hutibiwa matatizo haya. 

Baada ya uchunguzi tiba itatolea kuona kama hitilafu ni maambukizo au katika mfumo wa homoni. Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba zaidi.

Related Posts:

  • 15 Harmful Side Effects Of Aspirin You Must Be Aware Of We have all heard of ‘Aspirin’! It is one of the most commonly used drugs. But, most of us are unaware of the purpose it serves and the side effects of its overdose.Aspirin, also known as acetylsalicylic acid, is a salicyla… Read More
  • 10 Surprising Side Effects Of Watermelon Come summers and we can find watermelons everywhere! The perfect summer fruit, watermelons with high water content, make for great thirst quenchers. Watermelons are not just tasty and refreshing but are healthy too! They c… Read More
  • 10 Harmful Side Effects Of Ginseng Tea Ginseng is an ancient herb, which offers remedies for many diseases. It is also known as the king of all herbs. It protects our body and also helps our body fight innumerable diseases. Ginseng is an adaptogen, which is cap… Read More
  • 5 Side Effects Of Garlic You Should Be Aware Of Allium sativum, commonly known as garlic is a member of the onion genus species, Allium. It falls into the broad category of onions, shallots, leak and chive and is usually of a pungent nature in smell and taste. Originati… Read More
  • 10 Unexpected Side Effects Of Peppermint Tea Peppermint—the word conjures up images of bubble gums, right? But, peppermint is also used to provide flavor to various other products. Some of them are toothpaste and tea. It is an active ingredient in various medicinal a… Read More

2 comments: