Thursday 26 June 2014

FAIDA YA VYAKULA VYA ASILI YA UNGA (KABOHAIDRETI)




VYAKULA VYA ASILI YA UNGA (KABOHAIDRETI):

Vyakula hivi vipo aina mbili yaani sukari na wanga.

a) SUKARI.
Sukari hupatikana kwa njia mbalimbali, kuna aina tatu za sukari, sukari ya kawaida hupatikana katika miwa na sugar beet (namna ya mbo
ga ambayo ina kiazi cheupe) ambacho hutumika kusindika sukari, sukari ya matunda ipatikanayo katika matunda na sukari ya maziwa ipatikanayo katika maziwa.

b) WANGA.
Wanga ni aina ya vyakula ambavyo hupatikana hasa katika nafaka za mashina chini ya ardhi (mizizi) vyakula vya aina ya wanga ni kama vile ngano, mchele, mahindi, mtama, uwele, ulezi, viazi vitamu, viazi vikuu, viazi mviringo, magimbi na ndizi.

MATUMIZI:
1) Kutengeneza mafuta.
2) Kufanya mwili uwe na joto.
3) Kuupa mwili nguvu.

UKOSEFU WA KABOHAIDRETI HUSABABISHA MARADHI YAFUATAYO:
1) Ukosefu wa mafuta mwilini.
2) Kudhoofika kwa nyama za mwili.
3) Uzito wa mwili kupungua.
4) Kutokua kwa mwili.

0 comments:

Post a Comment