Thursday, 26 June 2014

FAIDA YA VYAKULA VYA ASILI YA NYAMA (PROTINI)





VYAKULA VYA ASILI YA NYAMA (PROTINI):

Asili ya vyakula hivi hutokea kwa wanyama na mimea. Vyakula kama mayai, maziwa, maini, mafigo, nyama, jibini, samaki, kunde na aina zake, ufuta karanga, korosho, mchicha, mbegu za tikiti maji, mtama, mahindi, mchele, mihogo, viazi, viazi vikuu na nazi.

MATUMIZI;
1) Kutengeneza misuli.
2) Kutengeneza mafuta.
3) Kurudishia mwili chembe hai (seli) zile zilizokwisha chakaa na kutolewa nje ya mwili (kuujenga mwili)
4) Kuupa mwili joto.

MATOKEO YA UPUNGUFU WAKE:
1) Ukosefu wa chembe hai za mwili.
2) Mwili kutojengeka vizuri.
3) Kuchoka kwa mwili upesi na kuzeeka mapema.
4) Misuli ya mwili kulegea.
5) Utepetevu na kulegea kwa misuli.
6) Kushindwa kuyamudu magonjwa makubwa yanapoingia mwilini.
7) Mwili kuvimba.

0 comments:

Post a Comment