KWA
mujibu wa wataalamu na watafiti wa masuala ya afya ya mwanadamu, zama
za matumizi ya dawa za ‘antibiotic’ zinazoaminika kutibu magonjwa mengi
ya kuambukiza, zimeanza kutoweka baada ya dawa hizo kubainika kukosa
uwezo wa kuua vijidudu, licha ya ukali wake.
Baadhi
ya watumiaji wameanza kubaini ukweli huu baada ya kujikuta wanatumia
dawa hizo kwa wingi bila kupata ahueni ya matatizo waliyonayo, badala
yake wamejikuta wakipatwa na madhara mengine ya kiafya, hasa kwa akina
mama ambao huambukiza watoto walio tumboni na athari zake kuonekana
mtoto anapozaliwa.
SABABU ZA HALI HII
Kuna sababu kadhaa za dawa
kuishiwa nguvu, chache kati ya hizo ni pamoja na ukweli kwamba kuna aina
nyingi za bakteria sugu ambao wanabadilika kila kukicha na kwa kasi ya
juu kuliko utafiti unaofanywa na wataalam kuboresha dawa hizo.
Aidha, makampuni mengi yanayotengeneza dawa hizo, baadhi yameacha
kuvumbua aina nyingine ya dawa za ‘antibiotic’ za kuendana na mabadiliko
ya bakteria, sababu ya kuacha kuendeleza dawa hizi ni faida ndogo
wanayoipata kwa aina ya dawa hizo.
Utakumbuka kwamba makampuni mengi ya dawa yako kibiashara zaidi
kuliko kuokoa maisha ya watu, hivyo yameacha kuendeleza utafiti wa dawa
hizi na badala yake yamejikita kwenye kutengeneza dawa zenye faida kubwa
kama vile dawa za saratani, magonjwa ya moyo, kisukari, presha na
ukosefu wa nguvu za kiume!
Kwa muda mrefu zimekuwepo makala kadhaa kwenye magazeti na majarida
ya afya duniani yakitahadharisha madhara ya dawa za ‘antibiotic’, lakini
Dr. Ajun Srininasan ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na
Kuzuia Magonjwa nchini Marekani (CDC), anasema kuwa hivi sasa mwisho wa
‘antibiotic’ umeshawadia na hatuna njia nyingine zaidi kutumia njia
asilia za kujikinga na maradhi.
NINI CHA KUFANYA?
Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa, kuna njia nyingi za kufanya ili kujikinga na maradhi. Kwa sababu tutakuwa hatuna chaguo lingine, pengine sasa ndiyo wakati muafaka wa kuzijua na kuzitumia njia hizo, ambazo zaidi zinahusisha ulaji wa vyakula sahihi.
Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa, kuna njia nyingi za kufanya ili kujikinga na maradhi. Kwa sababu tutakuwa hatuna chaguo lingine, pengine sasa ndiyo wakati muafaka wa kuzijua na kuzitumia njia hizo, ambazo zaidi zinahusisha ulaji wa vyakula sahihi.
Mungu ameumba kila aina ya vyakula na kila kimoja kina kazi na faida
yake mwilini. Vyakula vinavyoaminika kuwa na virutubisho asilia sawa na
vile vya dawa za ‘antibiotic’, ni pamoja na kitunguu saumu (garlic),
mdalasini (cinnamon), asali (honey), mwanga wa jua na vitamin D.
Upigwapo na mwanga wa jua la asubuhi unajipatia vitamin D mwilini ambayo
ni moja kati ya vitamini zinazodumisha kinga mwilini.
Mwili ukiwa na kinga ya kutosha, siyo rahisi kupatwa na maradhi ya
kuambukiza na yale ya mlipuko, kama uvimbe, vipele, kifua kikuu, mafua
ya muda mrefu, saratani, n.k. Ili kuupa mwili uwezo wa kujikinga
wenywewe, unatakiwa kuzingatia suala la kula matunda, mboga za majani,
hususan vitunguu na nyanya aina zote bila kusahau suala la kufanya
mazoezi.
Aidha, ukiwa na kinga imara asilia, hata inapotokea ukalazimika
kutumia dawa za ‘antibiotic’ zitaweza kufanya kazi kama kawaida, kwani
usugu wa vijidudu huimarika zaidi pale kinga asilia inapokosekana kabisa
mwilini. Kwa maana nyingine, usugu wa vijidudu huimarishwa zaidi na
mwili wenyewe.
0 comments:
Post a Comment