Monday, 5 May 2014

LISHE NI TIBA YA NGUVU ZA UZAZI


 
NDUGU msomaji mpendwa.
Katika makala ya wiki iliyopita tuliona namna tiba za dawa kali (antibiotic) zinavyozidi kuleta utata kwa matumizi ya binadamu na tukaona kuwa katika siku za hivi karibuni wengi wamekuwa wakikimbilia zaidi tiba za mitishamba na vyakula kama suluhisho.
 
Tiba za vyakula na mitishamba wengi wameikubali pale wanapopatwa na matatizo ya nguvu za uzazi kuliko dawa kali kama vile Viagra na nyinginezo kwa kuwa matokeo ya matumizi ya lishe kama tiba yameleta matokeo mazuri bila athari mwilini.

Nguvu za uzazi wengi huita nguvu za kiume, lakini hata wanawake pia hupatwa na matatizo haya na hujikuta wakitafuta suluhisho kwa waganga kama ilivyo kwa wanaume. Nguvu za uzazi ni tatizo sugu hasa kwa wenye umri wa kuanzia miaka 45 na kuendelea, kwa sababu mwili hauna uwezo tena wa kuzalisha homoni za uzazi kama wakati wa ujana.

Ndoa nyingi huingia mashakani katika kipindi hiki huku vyanzo vya tatizo vikiwa vingi vikihusisha msongo wa mawazo na tatizo la kujichua (masturbation) ambalo limeongelewa sana katika medani ya tiba.
 
Tafiti zinasema asilimia 98 ya binadamu duniani hujichua na asilimia 2 wanaobaki huongopa tu kwa kuwa tendo la kujichua na staili zake ni siri ya anayejichua.
Unapoona nguvu za uzazi zimepungua basi elewa kuwa ulaji wa vyakula vya asili, yakiwemo matunda na mboga za majani, umeshuka na ukianza kuvitumia taratibu vyakula asilia nguvu nazo huanza kurejea.

Katika maendeleo ya sayansi na teknolojia, njia mbalimbali za kumrahisishia maisha mwanadamu zimekuwa zikivumbuliwa kila siku, likiwemo suala la lishe. Leo kuna makampuni kadhaa, kama vile GNLD, Forever Living, Vativa, n.k, ambazo zimekuwa mstari wa mbele wa kutengeneza vyakula na bidhaa za asili.

Makampuni haya yalichokifanya ni kukusanya vyakula asilia na kuvitengeneza kwa teknolijia ya kisasa kwa njia ya vitengo kwa lengo la kutoa lishe kwa njia hiyo rahisi. Nativa wanayo bidhaa inayojulikana kwa jina la Go! Ambayo ina vidonge vyenye vitamin A, C, E, B6, B12, nafaka na madini ya zink.

Mchanganyiko huo ni maalum kwa kumpa mlaji vitamin na madini muhimu ya kujenga mwili wake iwapo mtu huyo atakuwa hana nafasi ya kupata na kuvitumia vyakula asilia wakati wote. Mchanganyiko huo unaaminika kusaidia katika kuimarisha nguvu za uzazi na unashauriwa kutumiwa na watu wenye matatizo hayo pamoja na kuongeza uimara na mg’aro wa ngozi.

Ili kujiepusha na tatizo la ukosefu wa nguvu za uzazi, ni vyema kujiepusha sana na ulaji wa vyakula vya kawaida ambavyo vimezoeleka na pengine ni rahisi mno kupatikana mijini. Vyakula hivyo ni pamoja na vile vinavyopikwa kwa kutumia mafuta mengi, vyakula vya kusindika (vya kwenye makopo) na vilivyopikwa baada ya kuondolewa virutubisho (processed foods).

Orodha ya vyakula hivyo ni ndefu, lakini chache kati ya hivyo vingi ni pamoja na chipsi mayai, unga mweupe unaotumika kupika ugali ambao ni ndiyo chakula cha familia nyingi, mkate mweupe, unywaji wa chai iliyowekwa sukari nyingi, n.k

Badala yake, tunashauriwa kuwa na utaratibu wa kula matunda na mboga za majani kwa wingi katika milo yetu ya kila siku na hata pale tunapokula vyakula visivyo na virutubisho kutokana na mazingira tuliyonayo, ni vizuri tukajua jinsi ya kufidia kwa kula vyakula asilia.

0 comments:

Post a Comment