Saturday, 10 May 2014
UTAFITI TUNDA LA KOMAMANGA HUWEZA KUZUIA KENSA YA MATITI ISITAMBAE MWILINI
Uchunguzi mpya umeonyesha kwamba, katika tunda la komamanga kuna kemikali zinazozuia kensa ya matiti isitambae.
Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarida la Utafiti wa Kuzuia Kensa umeoneysha kwamba, kemikali ziitwazo ellegitannins zinazopatikna kwa wingi kwenye komamanga, zinaweza kuzuia
kimeng’enya (enzyme) aina ya aromatase, suala ambalo huzuia kukua kwa homoni ya estrogen inayopatikana katika kensa ya matiti.
Shiuan Chen Kiongozi wa uchunguzi huo amesema kwamba, kemikali hizo kupunguza uzalishwaji wa estrogeni, na kusaidia kuzuia seli za kensa ya matiti zisizaliane, pamoaja na tezi la ugonjwa huo lisikue.
Aromatase, ni kimeng’enya ambacho hugeuza homini ya androgeni kuwa estrogeni, na kushambulia kimeng’enya hicho ndio lengo kuu la dawa za kupambana na kensa za matiti inazosababishwa na homoni ya estrogen.
Huko nyuma pia chunguzi zilionyesha kwamba tunda la komamanga lina faida kubwa kiafya hasa kwa kuwa na anti oxidanti nyingi na vitamini mbalimbali, ambazo hulifanya tunda hilo liweze kusaidia katika kupambana na magonjwa ya saratani, matatizo ya moyo na hata ugonjwa wa kusahau uzeeni au Alzheimer.
Anti oxidanti huzuia radikali huru ambazo ni hatari sana kwa miili yetu. Uwezo huo humepekea mwili kukabilina na magonjwa mbalimbali hata ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe.
Kama huwezi kupata tunda la Komamanga sokoni, basi unaweza kutumia juisi ya komamanga na daima tutunze afya zetu!
Utafiti mpya uliofanywa kwa majaribio umegundua kuwa katika mbegu za nyanya kuna mada asilia,
inayoweza kusadia mzungumzo wa kawaida wa damu na kuzuia damu isigande.
Mada hiyo iliyoko kwenye mbegu za nyanya iligunduliwa mwaka 1999 na Profesa Adim Dutta-Roy.
Jeli hiyo inayozunguka mbegu za nyanya, hunaweza kusaidia mzunguko wa damu.
Jeli hiyo isiyokuwa na rangi wala ladha, huzuia chembe za damu aina ya platelets zisishikane,
suala ambalo hupunguza uwezekano wa damu kuganda, kama inavyofanya aspirini lakini bila kuwa
na madhara.Wachunguzi wa Uingereza wamesema kwamba, athari za geli hiyo huanza masaa matatu tangu
inapoanza kutumiwa na kudumu kwa masaa 18, hivyo inahitaji kutumiwa kila siku.
Wataalamu hao wamependekeza kwamba, kuongeza jeli hiyo katika vyakula mbalimbali kunaweza
kuepusha matumizi ya aspirini kwa ajili ya kuzuia hatari ya magonjwa ya mishipa ya moyo.
0 comments:
Post a Comment