Saturday, 10 May 2014

UTAFITI TIKITI MAJI CHUNGU LINASAIDIA KUZUIA KENSA YA MATITI



Utafiti mpya umegundua kuwa mada zinayotokana na tikitimaji ambazo ni mboga mboga zinazopatikana sana India, China na Amerika ya Kusini zinaweza kusaidia 

kuwaepusha wanawake na kensa ya matiti. Kwa mujibu wa uchunguzi huo uliochapishwa

kenye jarida la Utafiti wa Kensa, majimaji (extract) yanayotolewa katika tikitimaji chungu yanayojulikana kama 'karela' kwa kihindi yanaweza kupunguza kasi ya 


kukua kwa seli za kensa ya matiti au hata kuua kabisa seli hizo. Ratna Ray aliyeongoza

uchunguzi huo anasema kwamba, tikitimaji chungu zina uwezo wa kuzuia kensa na kuchelewesha kutokea ugonjwa huo wa saratani ya matiti, lakini bado haijathibitika iwapo mboga mboga hizo zinaweza kutibu ugonjwa huo.


Wanasayansi wanasema kuwa uchunguzi zaidi unapaswa kufanywa ili kuhakikisha uwezo na usalama wa tikitimaji chungu kuhusiana na suala hilo. 


Ratna Ray aidha anasema kuwa, kutumia lishe asilia ni suala linalopewa umuhimu mkubwa hivi sasa na sayansi katika kuzuia ugonjwa wa saratani ambao umekuwa ukiongezeka siku baada ya siku. Mtaalamu huyo vilevile

amesema, katika siku za usoni watafanya uchunguzi utakaowahusisha watu wengi zaidi walio na hatari ya kupata kensa ili kuona iwapo tikitimaji chungu zitawazuia wasipate ugonjwa huo au la.



Kwa muda mrefu tikitimaji chungu ambazo zina Vitamin C na mada ya flavonoid zimekuwa zikijulikana kwa kuwa na uwezo wa kuzuia kisukari na kupunguza kiwango cha sukari katika damu.

0 comments:

Post a Comment