Saturday, 10 May 2014

UTAFITI JELI YA NYANYA NI BORA KULIKO ASPIRINI




Utafiti mpya uliofanywa kwa majaribio umegundua kuwa katika mbegu za nyanya kuna mada asilia,

inayoweza kusadia mzungumzo wa kawaida wa damu na kuzuia damu isigande.



Mada hiyo iliyoko kwenye mbegu za nyanya iligunduliwa mwaka 1999 na Profesa Adim Dutta-Roy.




Jeli hiyo inayozunguka mbegu za nyanya, hunaweza kusaidia mzunguko wa damu.



Jeli hiyo isiyokuwa na rangi wala ladha, huzuia chembe za damu aina ya platelets zisishikane,

suala ambalo hupunguza uwezekano wa damu kuganda, kama inavyofanya aspirini lakini bila kuwa

na madhara.



Wachunguzi wa Uingereza wamesema kwamba, athari za geli hiyo huanza masaa matatu tangu

inapoanza kutumiwa na kudumu kwa masaa 18, hivyo inahitaji kutumiwa kila siku.



Wataalamu hao wamependekeza kwamba, kuongeza jeli hiyo katika vyakula mbalimbali kunaweza

kuepusha matumizi ya aspirini kwa ajili ya kuzuia hatari ya magonjwa ya mishipa ya moyo.


0 comments:

Post a Comment