Saturday 10 May 2014

KUNYWA KAHAWA KUNAWEZA KUPUNGUZA HATARI YA KUPATWA NA KANSA YA KORODANI



Utafiti uliofanywa nchini Marekani umeonyesha kuwa, kunywa kahawa kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya

kupatwa na ugonjwa wa kensa ya korodani au prostate cancer.


Uchunguzi huo umeonyesha kwamba, wanaume wanaokunywa kahawa kwa wingi, hunguza hatari hiyo kwa

asilimia 60 ikilinganishwa na wanaume ambao hawanywi kahawa kabisa.


Kahawa inaathiri jinsi ambavyo mwili unayeyusha sukari, pamoja na kiasi cha homoni za jinsia, masuala ambayo

yanahusiana moja kwa moja na kensa ya korodani.


Watalamu hao wamesema kuwa, kampaundi za kibayolojia zilizoko katika kahawa zinazuia tishu kuharibika na

hivyo kupunguza uwezekano wa kensa ya korodani kukua.


Inafaa kufahamu kwamba, kensa ya korodani ni kensa ya pili inayowapata kwa wingi wanaume duniani na

kusababisha vifo. Kati ya wanaume 6 mmoja kati yao hupatwa na saratani ya korodani.

0 comments:

Post a Comment