Baada ya kusoma makala yangu ya leo
na kuzingatia nilichokiandika, bila shaka utaanza kuiangalia ndizi kwa mtazamo
tofauti na uliokuwa nao hapo awali. Ndizi mbivu ni tunda maarufu sana duniani
lakini ni watu wachache wanaojua uwezo, faida na maajabu yaliyomo kwenye tunda
hili.
Ndizi ina aina tatu za kipekee za
sukari zinazojulikana kitaalamu kama Sucrose, Fructose na Glucose na vilevile
ina kiasi kingi cha ufumwele (fibre) ambacho husaidia sana katika usagaji wa
chakula tumboni.
Ndizi ina uwezo mkubwa wa kuongeza
na kuimarisha nishati ya mwili. Unaweza kupata nishati ya kufanyakazi ya muda
wa dakika 90 kwa kula ndizi mbili tu. Bila shaka ndizi ni tunda muhimu sana kwa
wanamichezo. Hata hivyo, nishati siyo faida pekee unayoweza kuipata katika
ndizi, ni tunda lenye uwezo pia wa kuponya na kuzuia matatizo mengi ya kiafya:
MFAIDHAIKO WA AKILI (DEPRESSION)
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na
Chama Cha Afya ya Akili cha Taifa (MIND) cha nchini Uingereza, kwa watu wanaosumbuliwa
na tatizo la mfadhaiko wa akili, watu wengi waliondokana na tatizo hilo na
kujisikia vizuri baada ya kula ndizi mbivu. Hali hii inatokana na ukweli kwamba
ndizi ina kirutubisho kinachojulikana kama tryptophan, ambacho ni aina fulani
ya protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.
MATATIZO WAKATI WA HEDHI
Kama wewe ni miongoni mwa wale akina
mama wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa
kula ndizi mbivu na unaweza kuponywa. Vitamin B6 iliyomo kwenye ndizi,
hurekebisha kiwango cha sukari ambacho huweza kuathiri hali ya mtu.
UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA)
Ndizi ikiwa ni chanzo kizuri cha
madini aina ya chuma (iron), inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya upunguvu
wa damu kwa sababu madini ya chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu
mwilini.
SHINIKIZO LA DAMU
Tunda hili ni la aina ya kipekee,
lina kiwango kikubwa cha madini ya potasiamu (potassium) na wakati huo huo lina
kiasi kidogo sana cha chumvi (sodium) hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika
kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.
Ukweli huo, hivi karibuni umeifanya
Mamlaka ya Dawa na Chakula ya nchini Marekani, iwaruhusu wazalishaji na wauzaji
wakubwa wa ndizi nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana
na hatari ya shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.
NGUVU YA AKILI
Hivi karibuni, wanafunzi wapatao 200
wa Shule ya Twickenham nchini Uingereza, walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa
kula ndizi mbivu wakati wa mlo wa asubuhi (breakfast), wakati wa mapumziko na
wakati wa chakula cha mchana, ndizi ziliongeza uwezo wa akili zao. Utafiti
unaonesha kuwa potasiamu iliyojazana kwenye ndizi, ina uwezo wa kumsaidia
mwanafunzi kuamsha uwezo wake wa kujisomea.
KASUMBA (HANGOVERS)
Moja ya dawa ya haraka ya kuondoa
uchovu unaotokana na ulevi wa jana yake (hangover) ni kunywa ‘Milkshake’
iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali. Ndizi hutuliza tumbo, ikisaidiwa na
asali, hurejesha kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu wakati maziwa
hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake.
Mbali na matatizo yaliyoelezwa hapo
juu, ndizi pia husaidia katika matatizo mengine mengi kama vile kutuliza
mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kutuliza vidonda vya tumbo, kuondoa asidi
tumboni, kushusha joto mwilini, kurekebisha mapigo ya moyo, n.k
Hivyo ndizi ni tiba ya magonjwa
mengi na ni bora, ukiilinganisha na Tufaa (Epo (Apple), ndizi ina protini mara
nne zaidi, wanga mara mbili, vitamin A na chuma mara tano na vitamini na madini
mengine mara mbili zaidi ya tufaa.
Mwisho;
USIWEKE NDIZI KWENYE JOKOFU!
0 comments:
Post a Comment