Thursday, 1 May 2014

FAIDA 12 ZIPATIKANAZO KWA KULA TUNDA LA CHUNGWA KIAFYA.

Kumbuka kuwa hata chungwa moja tu ukila lina kidhi yale mahitaji muhimu ya mwili ya kila siku (daily requirement), iwe chungwa lenyewe au juisi yake halisi.

1. UKOSEFU WA CHOO
Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula tumbuni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo. Aidha, kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.

 
2.UGONJWA WA MOYO
Kiwango kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’ vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease)!
 
3. SHINIKIZO LA DAMU
Virutubisho vya Magnesi (Magnesium) na ‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.

4. UGONJWA WA MAPAFU
Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.
 
5. MIFUPA NA MENO
Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno.

 
6. AFYA YA NGOZI
‘Anti oxidants’ iliyomo kwenye chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia huifanya ngozi ‘isizeeke’. 

7. KOLESTRO
Virutubisho vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake.
 
8. UKUAJI WA UBONGO
Chungwa moja lina kiasi cha asilimia 10 ya ‘folic acid’ inayohitajika mwilini kila siku. Madini haya ni muhimu kwa afya ya ngozi na ukuaji wa ubongo kwa ajili ya kuimarisha kumbukumbu na uwezo wa mtu wa kufikiri.
9. KINGA YA MWILI
Vitamin C iliyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara, yakiwemo malaria.
 
10. UGONJWA WA FIGO
Ulaji wa machungwa mara kwa mara, ukusaidia kujiepusha na ugonjwa wa figo kwa kiasi kikubwa.
 
11. UGONJWA WA MAFUA
Kutokana na wingi wa virutubisho vya kinga vilivyomo kwenye chungwa, ulaji wake mara kwa mara utakuepusha na magonjwa ya kuambukiza na vairasi (virus), kama vile mafua ambayo hivi sasa yanawasumbua watu wengi. Hivyo kula machungwa mengi kadii uwezavyo ili ujiepushe na mafua.
 
 
12. KINGA YA MAGONJWA MENGI
Chungwa, siyo tu linatoa kinga kwa magonjwa yaliyoainishwa hapo juu, bali pia hutoa kinga hata kwa magonjwa mengine kama vile baridi yabisi (arthritis, rheumatism), pumu, kikohozi, kifua kikuu, nimonia na kisukari. Nakushauri kula machungwa au juisi yake halisi kuanzia leo ili kupata faida hizo.

Related Posts:

  • FAIDA YA JUISI YA UKWAJU Tunda la ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwil… Read More
  • FAIDA YA MBEGU ZA TIKITIMAJI Faida ya kutafuna mbegu za tikiti maji TIKITI MAJI ni moja ya matunda yanayolimwa sana  katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania tofauti na miaka iliyopita. Hii inaashiria kwamba tunda la tikiti maji l… Read More
  • FAIDA YA TUNDA LA APPLE (TUFAHA) KIAFYA "Apple" kwa kiswahili nafikiri linaitwa tunda damu, Tunda hili liko la aina tofauti yako ya kijani yako mekundu na haya mekundu ndio yaliyo mazuri zaidi na pia yanasemakana matunda mazuri zaidi ni yale ya Euro… Read More
  • FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA NYANYA.... FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA NYANYA.... Hili ni tunda mashuhuri na lenye virutubisho ambalo kwa kawaida hutumika kama mbogamboga. Kwa wastani, watu hula takribani kilo 8 za nyanya kwa mwaka. Nyanya zina aina mbalimbali z… Read More
  • SIRI YA PAPAI KATIKA UREMBO WAKO TUNDA la papai lina vitamini C na E,  lina siri kubwa ya urembo na hutumika kutengeneza facial za aina mbalimbali. Papai limekuwa likitumiwa kama tunda kwa kula lakini pia kwa kupaka na humfanya mtu awe na ngozi ya a… Read More

0 comments:

Post a Comment