Kuna hili suala linaloitwa 'kubemenda'
mtoto, watu wanadai kuwa sperms huwa
zinaleta madhara kwenye maziwa ya
mama na kumdhoofisha mtoto kiafya na
wengine wanasema ukimshika mtoto
baada ya sex pia ina madhara.
kiukweli suala la Kubemenda ni
imani potofu (myth) na hakuna uhusiano
wa sperms na maziwa ya mama katika
kudhoofisha afya ya mtoto; iwe kwa
kushirikiana tendo la ndoa au kumshika
mtoto baada ya sex.
imani potofu (myth) na hakuna uhusiano
wa sperms na maziwa ya mama katika
kudhoofisha afya ya mtoto; iwe kwa
kushirikiana tendo la ndoa au kumshika
mtoto baada ya sex.
Je, nini maana ya kubemenda mtoto?
Kwanza hii imani potofu inaeleza kwamba
kubemenda mtoto ni pale wanandoa
wanapojihusisha na tendo la ndoa baada
ya mtoto Kuzaliwa (pale mke anapokuwa
tayari kiafya kwa tendo la ndoa baada ya
kujifungua) kwa maana kwamba sperms
huharibu maziwa ambayo mtoto
ananyonya, si kweli hakuna uhusiano
wowote kati ya maziwa ya mama na
sperms katika kuathiri afya ya mtoto.
Pili kubemenda mtoto ni kitendo cha
wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa na
mke kushika mimba miezi mwili tu au
mitatu tu baada ya kujifungua na kupelekea
kuzaa mtoto mwingine baada ya mwaka na
matokeo yake mtoto aliyetangulia Kuzaliwa
huwa dhaifu kiafya (huchelewa kutembea)
na huitwa ni mtoto ambaye
amebemendwa, kitu ambacho ni imani
potofu kwani kuna wanandoa wengi tu
wamezaa watoto waliopishana mwaka na
wote wana afya njema kabisa.
Tatu kubemenda ni kitendo cha
mwanandoa mmoja kutoka nje ya ndoa
(sex) na akirudi ndani huendelea na tendo
la ndoa na matokeo yake mtoto wa ndani
ya ndoa huwa dhaifu, pia ni imani potofu
hakuna kitu kama hicho.
Jambo la msingi ni kufuata ushauri wa
kitaalamu ambao ni wiki sita baada ya
kujifungua.
Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hii
imani potofu
Iwe wanandoa kujihusisha na tendo la
ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa au kuzaa
mwingine baada ya mwaka au hata kutoka
nje hakuna uhusiano na mtoto aliyezaliwa
kama suala la usafi na lishe bora
litazingatiwa kwa mtoto anayehusika.
Je, kulikoni mababu zetu wakaweka
imani kama hiyo kwa wanandoa?
Kama zilivyo imani zingine potofu kama vile
mwanamke mjamzito kutokula mayai
mababu zetu walikuwa na somo ndani
yake, inawezekana walitaka kuhakikisha
wanandoa wanashiriki vizuri katika kulea
mtoto kwa pamoja bila kupendekeza tabia
za uchafu na kujirusha nje na ndani ya
ndoa bila utaratibu.
Pia labda mababu zetu walihofia kitendo
cha mwanamke kutoa maziwa (chuluzika)
wakati wa tendo la ndoa hasa anapofika
kileleni (tangu akifungue hadi miezi 8 hivi)
na wakawa wanahofia kinaweza kuathiri
kiwango cha chakula cha mtoto hivyo ili
kuzuia ni kutunga imani (potofu) kwamba
mtoto ataathirika kwa mke na mume
kushiriki tendo la ndoa.
Je, ili mtoto asionekane amebemendwa
wanandoa wanahitaji kufanya kitu gani?
Ni vizuri kufahamu kwamba hakuna
uhusiano wa sperms kuharibu maziwa ya
mama wakati wa kumnyonyesha mtoto
hivyo wanandoa kushiriki tendo la ndoa
halina uhusiano wowote na mtoto kuwa na
afya mbaya kiasi cha kuchelewa kutembea.
Mtoto anahitaji watoto chakula bora chenye
viini-lishe vyote vinavyohitajika ili kukua
vizuri pia mama anahitaji kujiweka
mazingira safi (kuwa msafi) wakati
ananyonyesha, ahakikishe anasafisha
chuchu zake na mikono yake au kuzingatia
usafi kimwili kabla ya kumnyonyesha mtoto
iwe baada ya sex au muda wowote.
Ni jukumu la baba na mama wa mtoto
kuhakikisha wanatumia muda wao
kuhakikisha mtoto anapata lishe bora na
mahitaji yote ya msingi ya mtoto ili kukua
na kuwa na afya njema na si kujinyima
kujihusisha na tendo la ndoa wakihofia
mtoto kuonekana amebemendwa.
Pia suala la usafi wa mazingira ya mtoto
anapoishi (vyombo vya kutumia kwa
chakula cha mtoto, usafi wa mwili wa
mtoto na mama na baba pia) ni muhimu
sana kwani baada ya tendo la ndoa ni
muhimu kwa mume na mke kuhakikisha
wanakuwa safi tena bila kujihusisha na
kumnyonyesha mtoto huku hawajanawa au
kuoga.
MUHIMU
Suala la kubemenda (binafsi naweza kuita
ni utapiamlo au kwashakoo kingereza-
Kwashiorkor) huzungumzwa sana na jamii
za “mtanzania wa kawaida” huwezi kusikia
katika nchi zilizoendelea na watu ambao
wameenda shule na wanafuata misingi ya
afya na uzazi katika kulea watoto wao na
pia mke na mume kuwa karibu kimapenzi.
Huwezi kusikia takataka za neno
kubemenda katika nchi zilizoendelea
kama Canada, Sweden, Australia,
Ujerumani nk why?
0 comments:
Post a Comment