Thursday, 1 May 2014

HATARI: DAWA, KEMIKALI ZINAVYOSABABISHA WATOTO KUZALIWA NA VIUNGO VISIVYOKAMILIKA


Dawa zinazoleta madhara si zile
zinazotumika mara kwa mara, lakini kwa
bahati mbaya wapo wanawake
wanajigundua kwamba wamebeba ujauzito
na hawa wanajikuta wakitumia dawa hizo
ambazo mwishowe zinawaletea madhara
katika ujauzito na hawezi kugundua mpaka
atakapojifungua japokuwa wapo ambao
mimba zao huharibika.

Hili ni tatizo kubwa na ambalo linazidi
kujitokeza, lakini ambalo kama litaachwa
liendelee lilivyo litaiangamiza jamii
Kujifungua mtoto asiyetimia viungo vyake
vyote, mwenye matatizo ya viungo au
viungo visivyo vya kawaida hutokana na
vitendo au matukio hatarishi yaliyofanyika
katika mwili wa mama, kuanzia siku moja
hadi miezi mitatu tangu mimba kutungwa.
Kitu chochote ambacho ni sumu, dawa,
kemikali, mionzi na mgawanyiko wa seli
wakati wa uumbaji  wa mtoto zimetajwa
kuwa sababu kuu za tatizo hilo.
Madaktari mbalimbali wanazungumza na
wametoa sababu mbalimbali huku
wakisisitiza kuwa mpaka sasa dunia bado
haijapata sababu maalumu inayosababisha
matukio kama hayo kutokea, lakini zipo
sababu  zinazoaminika kuwa chanzo cha
hayo.
Dk Cyriel Massawe Daktari Bingwa wa
Magonjwa ya Wanawake na Afya ya Uzazi
wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anasema
mwanamke mjamzito hashauriwi kunywa
dawa ya aina yoyote ile kama hajapata
ushauri kutoka kwa daktari ni kutokana na
baadhi ya dawa kuainishwa kwamba
huenda yanaweza kuchangia kuvuruga
uumbaji siku za mwanzo za ujauzito.
 “Hali hiyo husababisha seli
kushindwa kugawanyika vizuri kila moja
kwenda kufanya kazi ile inayokusudiwa
katika uumbaji wa mtoto hapo ndipo tatizo
huanza kutokea.”
 
Mfano kuwa tatizo kubwa
linalowapata watoto walioungana pia
linaweza kusababishwa na kutogawanyika
vizuri kwa seli wakati wa utungwaji wa
pacha.
“Mfano mzuri ni watoto walioungana, hawa
ni wale wa mfuko mmoja. Yai moja
linapogawanyika mara mbili ni nadra
kutokea kosa, lakini katika uumbaji seli
zikishindwa kugawanyika vizuri na kufanya
uumbaji uliotimifu hapo pacha wataungana
matumbo, migongo, vichwa na sehemu
zingine za mwili au mmoja asitimie kama
ilivyotokea hivi karibuni,”
Iwapo mama hakutumia vidonge
au dawa za aina yoyote basi yawezekana
tatizo ni la kiasili na hali hii hutokea katika
hatua za mwanzo wa ujauzito na hata
mwanamke akienda hospitali huambiwa
kwamba atajifungua watoto mapacha lakini
hali huwa ndivyo sivyo.
Kuna idadi kubwa ya
wanawake ambao hutumia dawa miezi ya
mwanzo kabla ya kujigundua kwamba
ameshika mimba  huathirika zaidi.
“Dawa zinazoleta madhara si zile
zinazotumika mara kwa mara, lakini kwa
bahati mbaya wapo wanawake
wanajigundua kwamba wamebeba ujauzito
na hawa wanajikuta wakitumia dawa hizo
ambazo mwishowe zinawaletea madhara
katika ujauzito na hawezi kugundua mpaka
atakapojifungua japokuwa wapo ambao
mimba zao huharibika,”
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto
katika Hospitali ya Muhimbili, Dk Zaitun
Bokhary anasema mama mjamzito hutakiwa
kutumia dawa za ‘folic acid’ kabla na baada
ya ujauzito ili kuepuka kujifungua mtoto
mwenye tatizo la kichwa kikubwa
(Hydrocephalus) na Mgongo wazi (spina
bifida).
“Kama una mpango wa kupata mtoto siku
za usoni unashauriwa kutumia virutubisho
vya aina ‘folic acid’ hata kama unayo afya ya
kutosha na unapata mlo kamili. Na mara
baada ya kupata ujauzito endelea kutumia
kirutubishi hiki kwa muda wa wiki 12 za
ujauzito,” anasema Dk Bokhary
Dawa hizo huepusha mama
kupata mtoto mwenye tundu la uti wa
mgongo, kichwa kikubwa na midomo
iliyopasuka.
“Vipo vyakula vingi ambavyo vina
mchanganyiko wa folic Acid mfano spinach,
sprouts, broccoli, maharagwe (green beans),
na viazi, juice ya machungwa na
maparachichi,” 
Iwapo mama aliwahi
kupata mtoto mwenye tundu kwenye uti wa
mgondo, au  anatumia dawa za kifafa,
kisukari au seli mundu (sickle cell anemia) ni
vyema akatumia dozi ya juu ya folic acid.
Mtaalamu wa Afya-
anasema inakadiriwa watoto 200,000
huzaliwa na matatizo haya kila mwaka
duniani na zipo sababu mbalimbali
zinazosababisha matatizo haya. “Kwa
asilimia 60 hadi 70 hakuna sababu
iliyothibitishwa wengi wanasema ni sababu
za urithi na vinasaba.
Sababu nyingine ni
vimelea maradhi, dawa au sumu” anasema
Shita anabainisha baadhi ya dawa mabazo
kitaalam huitwa ‘teratogenic drug’  ambazo
zimekuwa mwiba mkubwa kwa wajawazito
na kusababisha wengi wao kujikuta
wanaathiri watoto wao wakiwa tumboni,
dawa hizi huweza kupita katika kondo la
nyuma (placenta) na kumuathiri mtoto aliye
tumboni.
“Ili kumaliza tatizo hili wanawake wote
wajawazito wanashauriwa kumwona
daktari kabla ya kutumia dawa ya aina
yoyote ile, hata hivyo ni vema wakawa
wawazi ila wengi wao wamekuwa wasiri
kueleza hali zao wanapokuwa kwa daktari,
baadaye anaandikiwa dawa zenye madhara
kwa ujauzito lakini daktari akijulishwa
atajua dawa ipi ni salama kwa mjamzito,”
Madaktari wamezitaja dawa zinazoweza
kusababisha matatizo hayo nanamna
zinavyoweza kuleta madhara ni zile za
antibiotiki  kama Tetracycline na klorofeniko.
Kitaalamu madawa haya hayatakiwi
kutumiwa na mama mjamzito kwani kwa
kufanya hivyo katika kipindi cha awali
hupelekea mifupa na meno  kuwa na
matatizo.
Dawa nyingine ni Metronidazole (flagilly)
ambapo wataalamu wanasema kama mama
atazidisha dozi inaweza kuleta madhara.
Phenytoin
Dawa ya Phenytoin inayotumika kutibu
magonjwa ya akili-mfumo wa fahamu kama
kifafa  huweza kuleta  madhara katika
ubongo, seli  za nyuma ya koo na matatizo
ya maumbile ya uso.
Dawa nyingi za kutibu saratani zina
kemikali  hivyo nazo huingia na kuzuia
ukuaji wa seli.
Vitamin A-retinol
Kuzidisha dozi ya kirutubisho hichi
husababisha watoto kuzaliwa na maumbile
yasiyo ya kawaida. Kama vile  mdomo
sungura (cleft) na uti wa mgongo kuwa
wazi, au tumbo kuwa bila ngozi, matatizo
sehemu za uso.
 Hizi ni dawa za vitamin A lakini hutakiwa
kutumika kwa umakini mkubwa kwani
zikizidi husababisha matatizo.
Matukio ya nyuma
Septemba 15 mwaka huu katika kitongoji
cha Changanyikeni kijiji cha Gissambalang,
Wilaya ya Hanang’, Mkoa wa Manyara Nchini Tanzania
mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina
la Mwanjaa Masagati alijifungua mtoto wa
kike mwenye vichwa viwili vilivyokuwa na
uso wa mbele na nyuma. Hata hivyo mtoto
huyo alifariki dunia baada ya kuishi kwa
muda wa saa moja.
 
Katika tukio jingine Februari 20, mwaka
huu pacha wa kiume (Elikana na Eliud)
walizaliwa Kata ya Uyole jijini Mbeya wakiwa
wameungana sehemu ya kiunoni.
Pili Hija (24),  mkazi wa Jang’ombe, Zanzibar
alijifungua watoto walioungana, huku
mmoja akiwa ni kiwiliwili.  Pili alijifungua
mapacha hao Agosti 18, 2013, nyumbani
kwake na baadaye kupelekwa kwenye
Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar baada ya
watoto kuonekana si wa kawaida.
Mapacha hao walifanyiwa upasuaji Agosti
29, 2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Kitengo cha Tiba ya Mifupa (Moi) chini ya
daktari wa upasuaji wa watoto, Dk Zaituni
Bokhary.
Mtoto aliyebaki ni yule aliyezaliwa akiwa na
kichwa, ilibidi kumuondoa asiye na kichwa
kwa sababu asingeweza kuwa binadamu
kamili. Dk Bokhary alisema hii ni mara ya
kwanza kwa jambo hilo kutokea katika
miaka ya hivi karibuni. Mara ya mwisho
lilitokea mwaka 1984
                            jiepushe na matumizi ya dawa yasiyo na maelekezo

0 comments:

Post a Comment