Saturday 3 May 2014

UJUE UGONJWA WA KICHOCHO NA NAMNA YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUO



Kichocho ni ugonjwa unaosababishwa na
minyoo ambayo humpata mtu anapotumia
maji yaliyo na vijidudu hivyo vya maradhi
 
hususan katika nchi za kitropiki (yaani
zenye hali ya joto jingi). Bilharzia ni jina la
kimelea cha ugonjwa huu.

Aina za minyoo au Chistosomes
inayosababisha ugonjwa wa kichocho kikuu
kinachomuathiri binadamu ni hii ifuatayo:
 
Mosi, Chistosoma mansoni ambayo imeenea
katika nchi 53 na kwenye maeneo kadhaa
ya Afrika, Caribbean, mashariki mwa
 
Mediteranean na Amerika ya Kusini. Aina ya
Pili, ni Chistosoma japonicum/ Chistosoma
mekongi, inayoathiri utumbo.
 
Tatu, Chostosoma intercalatum-
inayojulikana kama bilharizia ya mkojo. Na
nne, ni ile ya Chistosoma haematobium ,
ambayo inaziathiri nchi nyingi za
Afrika .
 
Ugonjwa wa kichocho unahesabiwa
kuwa ugonjwa wa pili unaonea kwa wingi
zaidi katika nchi zenye joto jingi.
 
Viini vya ugonjwa wa kichocho vilivyokomaa
huishi katika mishipa kwenye kibofu cha
mkojo na utumbo.

Kimelea cha kike hutaga mayai mengi
ambayo hutoka kwa mtu aliyeathiriwa na
kwenda kwenye maji wakati wa kukojoa au
haja kubwa.
 
Mayai yanapokuta maji huanguliwa na kutoa
viluwiluwi, ambao hupenya na kuingia
ndani ya konokono wa majini.
Aidha viluwiluwi hawa hukuwa ndani ya
konokono hao, kuongezeka na hatimaye
 
kutoka. Itafahamika kuwa viluwiluwi hawa
wana uwezo wa kupenya ndani ya ngozi ya
mwanadamu na wakisha penya huingia
hadi katika mishipa ya ini, ambako hukua na
 
kukomaa. Baada ya hapo huingia katika
mishipa ya kibofu cha mkojo na utumbo
mpana.

Vimelea hivi hutaga mayai kwa wastani wa
miaka 3 na nusu, ns vinaweza kuongezeka
 
zaidi. Mayai yanayotagwa katika kuta za
utumbo mpana na kibofu husababisha
madhara makubwa. Iwapo ugonjwa wa
 
kichocho hautatibiwa ipasavyo, unaweza
kusababisha matatizo ya ini, utumbo mpana
na ugonjwa wa figo.
Aidha maambukizo yake yanaweza kuenea
 
katika uti wa mgongo na hata wakati
mwingine kuathiri ubongo. Karibu watu
milioni 600 duniani wako katika hatari ya
kuambukizwa ugonjwa wa kichocho.

Hebu sasa tuangalie ugonjwa wa kichocho
 
unasababishwa na nini?
 
Masuala au matatizo yafuatayo yanapelekea
watu kupatwa au kuambukizwa ugonjwa
wa kichocho:
 
Umaskini uliokithiri, ufahamu mdogo
kuhusu ugonjwa huo, ukosefu au uchache
wa suhula za afya kwa jamii, usafi duni wa
mazingira tunayoishi n.k.. Ugonjwa huo pia
 
huweza kuenezwa kutoka kwa watu
wanaohama kutoka katika nchi nyingine
ambazo ugonjwa huo umeenea.

Katika siku za awali wakati vimelea vya
kichocho vinapoingia katika mwili wa
mwanadamu, kijipele au swimmer’s itch
 
hujitokeza. Aidha baada ya kupita mwezi
mmoja au miwili, mtu
 
aliyekwishaambukizwa huanza kujisikia hali
ya kuchoka, homa, homa ya baridi, huwa na
kikohozi kikavu, maumivu ya misuli,
 
maumivu ya tumbo, kuhara, na hukojoa
mkojo ulio na damu.

Kipindi hiki huenda sambamba na ukuaji wa
minyoo katika mwili wa mwanadamu na
hujulikana kama homa ya Katayama.
 
Kuweko damu katika mkojo ni dalili tosha ya
kuonyesha kwamba mtu huyo amepatwa na
kichocho cha mkojo au kitaalamu hujulikana
kama urinary bilharzias.
 
Na iwapo mgojwa hatatibiwa, anaweza
kupata madhara mengine makubwa katika
ini na bandama.

Kichocho huaathiri zaidi makundi yafuatayo:
Watu wazima wanaojishughulisha na kilimo
na wale walio katika sekta ya uvuvi.
 
Kichocho kinachoathiri kibofu cha mkono
huwaathiri watoto milioni 66 katika zaidi ya
nchi 54 duniani.
 
Kidha katika ameneo mengi watoto waliona
umri wa kati ya miaka 10 na 14
 
wanaambukizwa ugonjwa wa kichocho.
Kimsingi maradhi haya huathiri ukuaji wa
watoto na mahudhurio yao shuleni.

Mtu anatakiwa kumuona daktari iwapo
atakuwa amesafiri katika eneo ambalo lina
maambukizo ya kichocho, iwapo ngozi yake
 
itagusana na maji yenye vimelea vya
ugonjwa huo na iwapo atakojoa mkono ulio
na damu.

Ugonjwa wa kichocho unaweza kuzuiwa
kwa urahisi iwapo kanuni za kiafya
zitazingatiwa. Hata hivyo hadi sasa hakuna
chanjo iliyopatikana ya kudhibiti ugonjwa
huo. Si maji yote ni salama kwenye maeneo
 
yaliyo na ugonjwa huu. Sehemu hatari zaidi
za ugonjwa huo ni maeneo kama vile kingo
za maziwa, mito na mabwawa ambapo maji
 
yametuama na kuna uoto wa mimea.
Sehemu salama ni kama vile katika fukwe za
bahari na zile zenye mawimbi ambazo si
rahisi kukuta konokono wa majini.

Mabwawa ya kuogelea ni salama iwapo
yatanyunyiziwa dawa ya klorini.
 
Ili kuweza kukabiliana na kuzuia
maambukizo ya ugonjwa wa kichocho,
masuala yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:
 
Miongoni mwao ni kuacha kuoga kwenye
maji yaliyotuama kama vile ya kingo za
mabwawa, mito n.k.

 Hakikisha kuwa maji ya kunywa ni salama
kwa kuyachemsha na kuyachuja ili kuuwa
vijidudu maradhi.

 Unaweza pia kuchemsha maji ya kuoga
angalau kwa nyuzi joto 65 kwa muda wa
dakika tano.

 Maji yaliyohifadhiwa kwenye tanki kwa
muda usiopungua masaa 48 ni lazima yawe
salama kwa ajili ya kuogea.

 Kama unalima, unashauriwa kuvaa mabuti
marefu ya mpira.

 
Ni vyema tujue kuwa, mtu anapaswa
kumuona daktari baada ya kuwa na dalili za
ugonjwa na yeye ndiye atakayemuainishia
 
dawa za kutumia. Ni matarajio yetu kuwa
iwapo tutafuata kanuni na misingi yote hiyo
ya kiafya hapo juu, basi tutafanikiwa
 
kushinda vita dhidi ya maradhi ya kichocho.
Daima tutunze afya zetu!

0 comments:

Post a Comment