Shirika la afya duniani
(WHO) linasisitiza mama kumnyonyesha mtoto kwa kipindi cha miezi sita bila
kumwanzishia vyakula vingine.
WHO inaelekeza kuwa baada
ya miezi sita mama anaweza kumwanzishia vyakula vyingine motto wake huku
akiendelea kunyonya maziwa ya mama angalau mpaka atakapofikia umri wa miaka
miwili au ziadi.
Pia, mtoto anyonyeshwe
saa moja baada ya kuzaliwa, anyonyweshwe pale anapohitaji mara nyingi kwa kadri
anavyohitaji usiku kwa mchana na mama anashauriwa kutotumia chupa kumpatia
maziwa mtoto.
FAIDA AZIPATAZO MAMA KWA
KUMNYONYESHA
MTOTO.
Maisha huwa rahisi kwa
mama anayenyonyesha kwani akilinganisha na maziwa ya mama ya fomula (yale ya
kutengeneza viwandani), maziwa ya mama hutumia nguvu kidogo au zaidi, hapo
baadaye baada ya mama na motto
kutulia na kuzoeana maziwa hutiririka kwa wingi
zaidi, huitaji kuwa na kazi ya kusafisha chupa na chuchu yake
kwa mashine
maalum za kuchemshia vyombo ili kuua viini vya maradhi, maziwa ya mama
hayahitaji kununua, kupima
wala kuchanganya, hayahitaji uamke usiku mwingi na
uyapashe, maziwa ya mama hupatikana kwa haraka na kwa muda sahihi pale mtoto
anapohitaji.
KUNYONYESHA KUONAOKOA
FEDHA.
Kwa mzazi huhitaji
kununua vyombo na maziwa ya fomula,kwa mwaka inakubidi kutumia zaidi y ash
milioni 4 ili kugharamia maziwa ya fomula na vyombo, pia
inaonyesha
watoto
wanaonyonyeshwa hawapatwi na maradhi mara kwa mara hivyo basi huokoa pesa nyingi ambazo zingetumika
kwa
matibabu.
KUNYONYESHA KUNAKUFANYA UJISIKIE
MWENYE FURAHA.
Kugusana kimwili wakati
wa kunyonyeshana na mtoto aliyezaliwa ni uhimu kwani mtoto huwa na usalama
zaidi, hupata joto sahihi na kutopata usumbufu wowote,
unapomnyonyesha panakuwa
na ukaribu wa kimwili hivyo hufanya uhusiano wako na mtoto kuimarika zaidi
hivyo
humpa mtoto faraja na kwako pia.
Pia, mtoto huzoea harufu
yako na kujiihisi mwenye usalama, hali hii ya mtoto kukutambua hukufanya
kujihisi
kupendwa na mtoto wako,
Mtindo uliobuniwa uitwao
kangaroo ambapo mama humbeba mtoto kwa mfano wa mnyama kangaroo ambavyo mtoto
wake, umeokoa maisaha ya watoto waliozaliwa kabla ya
muda na wenye uzito mdogo
kwani huwapa joto, kusaidiwa maziwa kutiririka na pia huimarisha uhusiano wa
mama na
mtoto.
Pia ukaribu wa kugusana
kimwili husababishwa mwili kuzalisha zaidi kichocheo (homoni) cha oxtixini,
kichocheo hiki kinasaidia maziwa kutiririka na kumpa utulivu mama.
KUNYONYESHA KUNAKUEPUSHA
NA MARADHI.
Tafiti zinaonyesha kuwa
kunyonyesha kunappunguza kupata magonjwa ya saratani ya matiti na vifuko vya
mayai ya uzazi, kisukari cha aina ya pili na pia huondoa sonono baada ya
kujifungua.
KUNYONYESHA NI NJIA YA
UZAZI WA MPANGO.
Kunyonyesha ni moja ya
njia ya uzazi wa mpango wa kiasili. Njia hii ya kunyonyesha ina uwezo wa kuzuia
mimba kwa asilimia 98 katika miezi sita tangu kujifungua.
HUOKOA MUDA WAKO KAZINI.
Kunyonyesha kunamwepusha
mtoto na maradhi ya mara kwa mara hivyo kunaokoa muda mwingi wa kumuuguza
mtoto.
FAIDA KWA JAMII.
Tafiti za hivi karibuni
zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya watoto wangelinyonyeshwa kwa miezi sita bila
kupewa vyakula vingine kungeweza kuzuia vifo vya watoto karibu 1000 na kuokoa vifo hivi, hivyo kunajenga ustawi wa jamii na taifa la kesho.
0 comments:
Post a Comment