Thursday, 1 May 2014

TUWI LA NAZI NI DAWA YA KUUWA VIRUSI VYA MARADHI MWILINI


KATIKA makala iliyopita tuliona jinsi mwili unavyoweza kujitibu wenyewe ukipata mlo sahihi. Leo tunapenda kuzungumzia faida za nazi, ambazo zinatokana na kuwa na mchanganyiko maalum wa aina nyingi za mafuta zijulikanazo kama ‘medium chain triglycerides’ au kwa kifupi (MCT’s).








Nazi ikiliwa na binadamu hugeuza aina hizo za mafuta kuwa tindikali ambayo kitaalamu huitwa ‘medium chain fatty acids’ au kwa kifupi (MCFA’s) ambazo huua na kutokomeza virusi vya aina mbalimbali mwilini.

Tui la nazi
Matumizi ya nazi kama tiba kwa waathirika wa virusi duniani yalilipuka kwa kasi mwaka 1990 mara baada ya mtafiti wa tiba kutoka Iceland, Bw. Halldor Thormar, kubaini maajabu ya tiba hii.

Waathirika wa virusi vya aina mbalimbali duniani waliotumia nazi walitoa ushuhuda wao wa namna walivyopata nafuu mara baada ya kutumia nazi kama tiba. Licha ya kuponya maradhi waliyokuwa nayo, iliwaboreshea afya zao na kuonekana kana kwamba si waathirika tena.





Dozi yake ni rahisi, unywaji wa glasi nne za tui la nazi kwa siku au vijiko sita vya mafuta ya nazi kila siku kwa muda wa kati ya miezi mitatu hadi minne, huweza kuondoa maradhi yote yanayosababishwa na virusi mwilini na pia kung’arisha ngozi na kuifanya kuwa nyororo.

Ushahidi wa faida ya nazi kama urembo upo kwa mabinti wa Kizaramo wanaowekwa ndani na kuchuliwa mwili mzima kwa machicha ya nazi kwa miezi kadhaa, ambapo wanapotoka nje huonekana warembo wenye ngozi nyororo waliyoipata kiasili bila kutumia ‘krimu’ au mafuta mengine ya gharama.

Kama sote tujuavyo, virusi vya Ukimwi hudhoofisha kinga ya mwili. Mwili unapokosa kinga hushindwa kuzuia virusi vya aina nyingine kukushambulia. Kwa kawaida tiba ya virusi huwa ni zile dawa zenye uwezo wa kushambulia virusi (antiviral), bakteria (antibiotic) na zile za kushambulia fangasi (antifungus).




Hata hivyo, dawa hizo ni kali sana kiasi cha kuwaumiza watumiaji na huwa na madhara (side effects) zinapotumiwa kwa muda mrefu, ukiachilia mbali gharama zake ambazo mwathirika mwenye kipato cha chini hawezi kuzimudu.

Lakini unaweza kujitibu maradhi yatokanayo na virusi kwa njia rahisi na salama. Kula nazi kwa wingi kadiri uwezavyo, kama ni muathirika basi anza kunywa tui la nazi glasi nne kwa siku na utaona maajabu ndani ya miezi mitatu tu. Kama tayari una vidonda visivyopona basi paka mafuta ya nazi kila utokapo kuoga, na matokeo utayaona bayana.

Related Posts:

  • KUONDOA CHUNUSI KWA KUTUMIA MANJANO Mahitaji  ya kuondoa chunusi kwa manjano - Vijiko viwili (2 tbs) vya unga wa binzari ya Manjano (Turmeric powder) - Kijiko kimoja (1 tbs) cha unga wa Riwa – wengine huita Liwa (Sandalwood) - Vijiko vinne… Read More
  • PILIPILI HUIMARISHA UJASIRI NA NGUVU MWILINI! Kama ilivyo kwa matunda na vyakula vingine kuwa na faida kiafya mwilini, pilipili nayo ni moja wapo. Licha ya kuogopwa na baadhi ya watu, lakini ina kiasi kingi cha vitamin C. Umuhimu wa Vitamin C mwilini,  … Read More
  • TIBA ASILIA YA TUMBO Watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tumbo lisilo la vidonda wala ugonjwa wowote ila utasikia anakwambia tumbo linanikata, huenda akawa anavurugikwa na tumbo au imetokea linasumbua tu. Tiba hii hapa Kwanza k… Read More
  • DAWA YA KUTIBU MUWASHO WA MWILINI Dawa ingine ya Muwasho  siyo lazima uwe wa mwili tu, bali kuna sehemu mbalimbali za mwili ambazozimejificha na fangasi uenda kujihifadhi katika sehemu hizo nazo unaweza kutumia maji ya aloe vera kwakutibu . Kwa … Read More
  • JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA PUMU (ASTHMA) JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA PUMU Mahitaji:   Karafuu 6  Karafuu  Maandalizi: Zitowe vichwa vyake kisha loweka hizo karafuu katika nusu gilasi ya maji usiku kucha   Matumizi: &nbs… Read More

0 comments:

Post a Comment