Sukari |
Wengi wetu
tumeshasikia ushauri wa
kula sukari kidogo, ushauri
ambao ni mzuri
kiafya.
Lakini licha ya tahadhari
mbalimbali zinazo tolewa
na wataalamu wa
afya kuhusu madhara
yatokanayo na ulaji
mwingi wa sukari, bado
idadi kubwa ya
watu hupenda kutumia
sukari kwa wingi
kwa njia mbalimbali.
Utumiaji wa sukari
siyo lazima ile
sukari nyeupe
( white ) au
kahawia ( brown ) pekee, bali
pia hata sukari
asilia inayo patikana kwenye
matunda, maziwa, asali, vinywaji baridi, pombe, baadhi ya
nafaka nakadhalika.
Hizo zote ni
aina ya sukari
ambazo zinatofautiana faida
na madhara.
Wakati viwanda vya uzalishaji sukari duniani vinaongezela, tatizo la
unene kupita kiasi
kwa biandamu nalo
linaendelea kuongezeka.
Sukari inahusika kwa
kiasi kikubwa na
tatizo la kuongezeka
kwa unene wa
kupindukia ( obesity).
Kwa watu wanene, ulaji wa sukari
hata kijiko kimoja
tu kwa siku, huchangia kwenye
tatizo.
Sukari ni ya
kuepukwa, siyo tu kwa
watu wanene, bali hata
kwa watu wengine
wenye kujali afya
zao.
Katika kitabu chake
kiitwacho “ LICK THE SUGAR HABIT ‘, Mwanalishe Nancy
Appleton ( PhD), ameelezea
sababu 146 za
kwa nini sukari
hudhoofisha afya zetu.
Zifuatazo ni baadhi
ya sababu hizo ;
i.
Sukari
huweza kuathiri ukuaji
wa homoni mwilini
( kitu ambacho ni muhimu kwa
kumfanya mtu kuishi
na afya njema
wakati wote )
ii.
Sukari
ndiyo chakula cha
saratani mwilini.
iii.
Sukari
huongeza lehemu ( cholesterol
) mwilini.
iv.
Sukari
huweza kusababisha kizunguzungu
na kudhoofisha mwili
kwa watoto.
v.
Sukari
huweza kudhoofisha nguvu ya macho
vi.
Sukari
huweza kuzuia utembeaji
wa protini mwilini
vii.
Sukari
huweza kusababisha mzio
wa chakula (
Food allergies )
viii.
Sukari
huchangia ugonjw a wa kisukari
ix.
Sukari
huweza kusababisha ugonjwa
wa moyo.
x.
Sukari
huweza kuharibu, umbo la vinasaba
vya mwili ( D.N.A )
xi.
Sukari
huweza kusababisha utukutu,
utundu na kukosa
umakini kwa watoto.
xii.
Sukari
huweza kuchangia kupunguza n kinga ya
mwili dhidi ya
magonjwa yatokanayo na
wadudu aina ya bacteria
( infectious diseases )
Hizo ni baadhi
tu ya hizo
sababu 146. Je, kwa kujua
sababu zote zilizo
thibitishwa kuhusu madhara
yatokanayo na sukari, kuna
sababu gani ya
kuendelea kupenda kutumia
sukari ?
Kitu kizuri pekee
kuhusu sukari ni kwamba,
kina ladha tamu na
tunapokula, tunajisikia raha. Hapa
ndipo pahali panahitajika
kuangaliwa kwa umakini.
Kiasilia, mwanadamu
ana ladha sita tofauti
zikiwemo za uchungu, utamu, ukali,uchachu, na ukakasi.
Hivyo kuacha kabisa
ulaji wa ladha
tamu, kunaweza kusababisha madhara
mengine ya kibaiolojia
na ndiyo maana
watu wengi hushindwa kujizuia
kutumia sukari, hasa kwa
watoto ambao kwao
huonekana ni jambo
lisilo wezekana kabisa
kuacha kulamba sukari.
Hata hivyo, kuna habari
njema kuwa unaweza kutumia
mbadala wa sukari
nna kupata ladha
ya utamu katika
vinywaji au vyakula
vyako bila kuwa
na madhara.
Moja ya mbadala
wa sukari anaye aminika na
wengi tangu enzi na
enzi , ni asali, ambayo
unaweza kuitumia kwenye
vinywaji mbalimbali bila
kuwa na madhara.
Hata hivyo,
baadhi ya wataalamu
wanasema kuwa asali nayo
ina ‘ fructose’ , huenda ikawa
na madhara pia, ingawa
kwenye vitabu vya
dini na baadhi
ya wanasayansi wameilezea
asali kama kitu
kisicho na madhara mwilini
licha ya kuwa
nayo ni tamu
kama sukari.
Sukari ya Stevia |
Baadhi ya wanasayansi
wamependekeza zaidi mbadala
wa sukari kuwa
ni “ Stevia” na “ Xylitol”, ambavyo vinatokana
na mimea na
majani, lakini vina ladha
ya utamu kuliko
hata sukari.
Sukari Ya Xylitol |
‘ Stevia’ na ‘Xylitol ‘
hutumika zaidi katika
nchi za Ulaya , Japan
na Amerika ya
Kusini, kwetu Afrika hazijulikani sana na
sidhani kama zipo.
0 comments:
Post a Comment