Harufu mbaya mdomoni inachagizwa
na
mambo kadhaa ikiwamo tabia zetu za kila
siku na maradhi ya meno.
Wakati mwingine jambo hili laweza
kukufanya ushindwe kujiamini wakati wa
kuzungumza na watu. Lakini pia laweza
kuwafanya wanaokuzunguka wakushushe
thamani wakidhani wewe ni mchafu...na
kumbe una maradhi.
mambo kadhaa ikiwamo tabia zetu za kila
siku na maradhi ya meno.
Wakati mwingine jambo hili laweza
kukufanya ushindwe kujiamini wakati wa
kuzungumza na watu. Lakini pia laweza
kuwafanya wanaokuzunguka wakushushe
thamani wakidhani wewe ni mchafu...na
kumbe una maradhi.
Tatizo la kunuka mdomo linawapata baadhi
ya watu, ambao hata wakipiga mswaki,
lakini bado ananuka mdomo hata pale
anapotumia vitu vya kuufanya mdomo
unukie vizuri kama ‘Chewing gum’ pipi
hususan pipi-kifua na hata Big G bado mtu
mwenye tatizo hilo ataendelea kuwa na
harufu mbaya.
Wanasayansi wamekiri kwamba ni vigumu
sana mtu kufahamu kuwa ana harufu
mbaya kwa sababu ya mazoea lakini ni
rahisi sana kutambua harufu kutoka
kwenye kinywa cha mtu mwingine.
Unaweza kutambua kama una harufu
mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu
unayemuamini na pia unaweza kujua
harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya
kiganja na kunusa, wengine hupumua
mbele ya kioo na kunusa.
Pia unaweza kutumia kijiti cha
kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi
unaweza kutumia vifaa kama ‘Halimeter’,
‘Gas’ ‘Chromatography ‘na ‘BANA Test.
“Magonjwa ya kinywa
yanasababishwa na
mabaki ya chakula kwa kuwa mwili wa
binadamu una vijidudu aina ya bacteria
ambao kwa kitaalamu huitwa ‘normal flora’.
Wadudu hao mara wanapokula hutoa
tindikali ambayo husababisha magonjwa ya
fizi na kinywa.
mabaki ya chakula kwa kuwa mwili wa
binadamu una vijidudu aina ya bacteria
ambao kwa kitaalamu huitwa ‘normal flora’.
Wadudu hao mara wanapokula hutoa
tindikali ambayo husababisha magonjwa ya
fizi na kinywa.
Vitu vyenye sukari ikiwemo sukari ya
kawaida pia huchochea tatizo hili, lakini
mpangilio wa meno katika kinywa
huhifadhi mabaki na kuleta harufu mbaya,”
Anaeleza kuwa tatizo hili pia huchangiwa
na vijidudu vya ‘bacteria’ wanaojificha kati
ya jino na jino na wengine kama ana jino
lililotoboka vijidudu hivi hutumia nafasi ya
kujificha humo.
Lakini wale ambao wana tabia ya kulala
mdomo wazi, tabaka la juu la ngozi ya
mdomo huoza na kutoa harufu mbaya.
Unywaji Pombe: Unywaji wa pombe
husababisha kiwango cha kabohaidreti
kubaki mdomoni na kuoza hivyo
kusababisha magonjwa ya fizi.
Chanzo kingine kikuu cha harufu mbaya
ya kinywa ni pale ambapo chakula kingi
kinabaki mdomoni hasa hasa nyama.
Utumiaji wa chakula chochote
kitakachokaa ndani ya mfumo wa usagaji
wa chakula kwa muda mrefu kitaanza
kuoza, na siku zote nyama inapooza
huanza kutoa harufu mbaya ( kunuka ).
Kwa hiyo hiki nacho ni chanzo kikubwa
cha harufu mbaya ya kinywa.
Harufu hii ya mdomo inaanzia kwenye
kinywa na kushuka kwenye mapafu na
kusababisha tatizo hilo kuwa kubwa zaidi.
kinywa na kushuka kwenye mapafu na
kusababisha tatizo hilo kuwa kubwa zaidi.
Nini cha kufanya unapokuwa na tatizo Hili:
Cha kufanya iwapo una tatizo la kutoa
harufu kwenye kinywa hakikisha unapiga
mswaki mara baada ya mlo. Ili kuwaondoa
vijidudu vya bacteria wanaotokana na
mabaki ya chakula na pia kama unajino
lililotoboka ni bora kuling’oa au kulitibu kwa
njia ya kusafisha meno na kujaza risasi,
Pia unaweza kutibu kwa njia mbadala kwa
kutumia Ndulele ili kuondoa vijidudu vya
bacteria vinavyotoboa jino wasiambukize
meno mengine. (Ndulele zinafanana na
nyanya chungu lakini haziliwi).
Wale ambao wakipiga
mswaki damu zinatoka kwenye fizi, hiyo ni
dalilia hatari.
Matibabu ya fizi
“Tatizo la Fizi (Non Communicable disease)
kama yalivyo mafua makali, kifua, koo na
kisukari yanahitaji matibabu ya mara kwa
mara.
Ni vyema kusafisha meno kwa dawa na
kupata elimu ya jinsi ya kuepukana na tatizo
hili.
Wanawake wanaongoz
Wanawake ndio
waathirika wakubwa wa tatizo la meno
kwani kati ya wagonjwa 10 ambao
amekuwa akipata tiba kwa siku katika hospital ya
waathirika wakubwa wa tatizo la meno
kwani kati ya wagonjwa 10 ambao
amekuwa akipata tiba kwa siku katika hospital ya
Hurbet Kairuki Iliyopo Dar es salaam,
saba ni
wanawake huku watoto wadogo wakifuatia
kwa tatizo la kuvunjika meno kutokana na
kula vitu vyenye sukari nyingi.
wanawake huku watoto wadogo wakifuatia
kwa tatizo la kuvunjika meno kutokana na
kula vitu vyenye sukari nyingi.
“Watoto hawanuki mdomo lakini wengi
wanaokuja hapa wametoboka meno na
wengine yamevunjika na hii inasababishwa
na mfumo wa maisha, wanapewa vyakula
laini hawahitaji kutafuna sana, vyakula vya
makopo, chipsi, na watoto kuanzia umri wa
miaka mitano hadi tisa ndio wanaongoza
kwa tatizo hili,” anasema daktari moja katika
hospitali ya KAIRUKI.
Ushauri aina ya vyakula vya kujiepusha na
magonjwa ya meno, watu
warudi kwenye vyakula vya asili kwani
meno hujisafisha yenyewe.
Kupiga mswaki
Wengi wetu tumezoea kupiga mswaki
asubuhi tu, lakini tunakula vitu vingi kutwa
nzima na kisha kulala na mchanganyiko wa
vyakula hivyo katika ulimi na meno.
Wengi wetu tumezoea kupiga mswaki
asubuhi tu, lakini tunakula vitu vingi kutwa
nzima na kisha kulala na mchanganyiko wa
vyakula hivyo katika ulimi na meno.
Wataalamu wa afya wanasema, mtu
anatakiwa kupiga mswaki mara tatu kwa
siku asubuhi anapoamka, baada ya chakula
cha mchana na wakati wa kulala. Akiweza,
apige mswaki kila baada ya mlo.
Magonjwa ya kinywa alisema
kama tatizo linaanzia mdomoni ni vyema
mgonjwa akatumia dawa maalumu ya
kusukutua kinywa kwa muda maalumu
ambayo itasaidia kuwaua bakteria
wanao sababisha harufu mbaya ya
kinywa.
Lakini pia nashauri watu kutumia dawa
maalumu ambayo itaenda kuondoa
uchafu wote uliooza na uliogandamana
tumboni na kwenye mapafu ambao ndio
chanzo cha kutokwa na harufu mbaya
ya kinywa.
Tahadhari kwa vitu
vifuatavyo:
Epuka: Kula vyakula kama vitunguu maji,
vitunguu swaumu, unywaji wa pombe,
vyakula vyenye protini nyingi kama vile
samaki, matumizi ya sukari, kahawa na
baadhi ya aina za dawa za mswaki.
“Pombe hukausha kinywa, Kinywa kikavu
huchochea mazalio ya bakteria wanao
sababisha harufu mbaya ya kinywa,”
Usivute sigara: “ Kama kweli mgonjwa
ana nia ya kumaliza tatizo la kutokwa na
harufu mbaya ya kinywa anapaswa
kuachana na uvutaji wa sigara kwani
sio tu unasababisha harufu mbaya ya
kinywa bali pia utakausha kinywa chako
na hivyo kusababisha mazalio ya
bakteria wasababishao harufu mbaya ya
kinywa.
Unywaji Kahawa: Kahawa ina tindikali
ambayo husababisha kuzaliwa kwa
bacteria wanaosababisha harufu mbaya
ya kinywa.
Zingatia: kunywa maji mengi kila siku
angalau lita tano kwa siku, kwani kwa
kufanya hivyo kutakusaidia kuosha
chembechembe za vyakula ambavyo
vimebaki mdomoni na vilevile usaidia
kuepusha mdomo kuwa mkavu.
Pia watu kujenga
utaratibu wa kuzifanyia uchunguzi afya zao
mara kwa mara sio tu ya kinywa bali ya
mwili mzima kwa ujumla kwani kuna
baadhi ya watu wananuka mdomo lakini
hawajitambui kama wana hilo tatizo lakini
kwa kufanya hivyo watajitambua na
kushauri angalau mara tatu kwa mwaka
kwa afya ya kinywa na mara moja kwa
mwaka kwa afya ya mwili mzima.
0 comments:
Post a Comment