Ni kweli kwamba hakuna katika jamii mtu
ambaye hajawahi kupatwa na ugonjwa
huu. Unapoumwa kichwa mara kwa mara,
angalia sababu zifuatazo-
1- Harufu kali (nzuri au mbaya):Harufu kali
huweza kusababisha kuuma kichwa, kama
maji ya karafuu kali, Shampoo, eneo
lililopuliziwa uturi na sabuni ya rehe kali na
mengineyo.
2- Njaa: Miongoni mwa sababu
zinazosababisha kuuma kichwa ni njaa na
mlo usokuwa kamili wa kila siku, au
kutopata mmoja kati ya mlo wa kila sku, hii
hupelekea upungufu wa kiwango cha
sukari katika baadhi ya miili dhaifu.
3-Kutolala au kutopata mapumziko kama
ipasavyo.
4- Hali ya hewa: Ubadilikaji wa hali ya hewa
ni moja kati ya sababu zinazosababisha
kuumwa kichwa.
5- Kutokuwa na utulivu: Moja kati ya sababu
za maumivu ya kichwa ni kutokuwa na
utulivu kutokana na sababu kadhaa
zilizosababisha kutokea hali hiyo, kutokua
na utulivu husababisha kufikiria sana na
kupelekea ubongo kutofanya kazi ipasavyo.
6- Magonjwa mbalimbali yanayopelekea
msukumo wa damu kua juu (high blood
pressure, waswahili wamezoea kusema BP),
upungufu wa damu, nk
7.inaweza kuwa ni dalili ya magonjwa
mwengine tena kama malaria
Kabla na baada ya kufanya vipimo vya afya
basi tujitahidi kutotumia uturi kupita
kipimo hasa zenye harufu kali, tujitahidi
kupata chai ya asubuhi na mlo wa usiku
tusikose kwani chai na mlo wa usiku ni
muhimu zaidi katika kufanya kazi viungo
vya mwili, tujitahidi kupumzika wastani bila
kuzidisha masaa manane kwa kila siku,
tujitahidi pale tu tunapojihisi kuwa na
uchovu fulani haraka tupumzike kwa muda
wa nusu saa au kwa lisaa limoja, ama kwa
wale wasiokuwa na utulivu(stress), kama ni
mwenye familia ajitahidi kuongea na familia
yake ili kutatua tatizo lilokuepo kwani hali
ya kutokuwa na utulivu aghlabu katika jamii
husababishwa na kazi tunazofanya kila siku
kama hatukuzifanikisha hutokea hali hiyo,
kwa wasokuwa na familia wajitahidi
kuongea na washauri wao ili kupata utatuzi
wa tatizo lake. Sababu za kuumwa kichwa
si hizo tu bali ni nyingi ila muhimu ni hizo
tulozitaja hapo awali, la muhimu tujitahidi
kuwa salama na afya njema kwani kuwa na
afya njema shughuli zetu za kila siku
zitakwenda vizuri bila dosari.
0 comments:
Post a Comment