Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii,
imepokea taarifa kutoka Shirika la
Afya Duniani (WHO) mnamo tarehe
22 Mei 2013, kuhusu kuwepo kwa
ugonjwa wa Nimonia
unaosababishwa na kirusi cha
“Novel Coronavirus”.
Taarifa hiyo
inaeleza kuwa,tangu ugonjwa huo
utokee mwishoni wa mwaka 2012
hadi tarehe 23 Mei 2013 idadi ya
wagonjwa wapatao 44 na vifo 22
viliripotiwa
Shirika la Afya Duniani
limethibitisha ugonjwa huu
kuwepo katika nchi za Mashariki ya
Kati yaani Jordan, Qatar, Saudi
Arabi na Falme za Kiarabu (UAE).
Katika bara la Ulaya, ugonjwa huu
umethibitishwa kutokea nchi za
Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza.
Katika bara la Afrika, ugonjwa huu
umetokea Tunisia.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
inapenda kutoa tahadhari ya
Ugonjwa huu kwa wananchi wote,
katika mikoa yote ya Tanzania na
hasa wale wanaosafiri kuelekea
maeneo tajwa yenye uthibitisho
wa ugonjwa huu.
Ugonjwa huu unaenezwa na kirusi
kiitwacho “novel coronavirus
(nCoV).”.
Dalili kuu za ugonjwa huu
ni kushindwa
kupumua kwa ghafla,
homa kali, kukohoa, na
kubanwa na mbavu na hatimaye
kupata Nimonia.
Dalili nyingine
ambazo zinaweza kutokea ni
pamoja na kupata maumivu
makali ya tumbo pamoja na
kuharisha.
Vile vile ugonjwa huu
unaweza kupelekea figo
kushindwa kufanya kazi na hata
kusababisha kifo.
Kipindi cha
kuonekana kwa dalili za ugonjwa
huu
ni kati ya siku 2 hadi 10 baada ya
kupata maambukizi.
Ugonjwa huu
hauna tiba wala chanjo.
Ugonjwa huu unaweza
kuambukizwa kutoka kwa mtu
mmoja kwenda kwa mwingine.
Njia za maambukizo bado
hazijajulikana ingawa uwezekano
mkubwa wa maambukizo ni kwa
kwa njia ya hewa (kukohoa/kupiga
chafya) au kwa kugusa majimaji/
makamasi kutoka kwa mgonjwa
aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa
huo.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
imechukua hatua zifuatazo katika
kukabiliana na tishio la ugonjwa
huu:
Kutoa taarifa ya tahadhari ya
ugonjwa huu kupitia kwa
Waganga Wakuu wote wa Mikoa
na Wilaya kwa Tanzania bara.
Aidha, taarifa hii pia imejumuisha
namna mgonjwa anavyoweza
kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa),
“Fact sheet” ya ugonjwa,
Mwongozo kwa watumishi wa
afya wa namna ya kuchukua
sampuli ikiwa ni pamoja na
vipeperushi vinavyoelezea jinsi ya
kujikinga na maambukizi ya
ugonjwa huu.
Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa
huu kupitia kwa Wataalamu wa
Afya katika Mikoa, Wilaya na
maeneo ya mipakani. Aidha
watalaamu hawa pia wanatoa
elimu kwa wananchi kuhusu dalili
za ugonjwa huu na jinsi ya
kujikinga na maambukizi ili
endapo ugonjwa huo utatokea
uweze kutolewa taarifa mapema.
Wizara inasisitiza kuwa hakuna
vikwazo vyovyote vilivyowekwa
kwa ajili kwa wasafiri
watakaokwenda au kurudi katika
maeneo tajwa yaliyothibitishwa
kuwa na ugonjwa huu. Vipeperushi
vya ugonjwa huu vimetumwa
katika maeneo ya mipakani ili
iwapo msafiri anayeondoka au
kurudi nchini akiwa na dalili tajwa
atoe taarifa kwa watumishi wa
afya wa mpakani ili hatua stahili
ziweze kuchukuliwa.
Kutoa mafunzo kwa watumishi wa
afya na mipakani wa namna ya
kutambua na kujikinga dhidi ya
maambukizo ya ugonjwa huu
pamoja na uchukuaji wa sampuli
iwapo mgonjwa atapatikana
Kupeleka vifaa kinga kwa ajili ya
watumishi wa afya
Wananchi wanashauriwa
kutokuwa na hofu kwani mpaka
sasa hakuna mgonjwa yeyote
aliyeripotiwa nchini. Wizara
inapenda kutoa tahadhari kwa
wananchi juu ya umuhimu wa
KUNAWA MIKONO VIZURI KWA
SABUNI NA MAJI MARA KWA MARA
na pia KUZUIA MDOMO NA PUA
KWA KITAMBAA AU KARATASI
LAINI WAKATI WA KUKOHOA AU
KUPIGA CHAFYA.
KUPIGA CHAFYA.
Pia wananchi wanashauriwa kutoa
taarifa kwenye kituo cha kutolea
huduma za afya kilicho karibu
mara watakapoona mgonjwa
yeyote atakayehisiwa kuwa na
dalili za ugonjwa huu.
dalili za ugonjwa huu.
0 comments:
Post a Comment