Sunday, 4 May 2014

MAMBO YANAYO HARIBU AFYA YA BINADAMU


Mazingira 
ni jambo lingine
linaloathiri afya. Iwapo maji
tunayokunywa na kutumia ni safi
na salama, iwapo hewa
tunayovuta si chafu, maeneo
tunayofanyia kazi ni salama na pia
nyumba tunazoishi, basi afya zetu
huwa salama zaidi ikilinganishwa
na watu wanaoishi kwenye
maeneo yasiyo na maji safi na
salama au kuvuta hewa chafu na
kufanya kazi kwenye mazingira ya
hatari.

Uchunguzi uliofanywa na chuo
kikuu cha Zuyd nchini Uholanzi
umeonesha kwamba, kuvuta hewa
iliyochafuliwa kwa gesi za magari
kwa lisaa limoja kunatosha
kumpatia mtu mfadhaiko wa
kifikra au stress katika ubongo
wake.

Utafiti
 
mwingine uliofanywa na
chuo kikuu cha India cha Purdue
umebainisha kuwa, sumu kali
inayotokana na sumu ya risasi,
inayoweza kuiingia mwilini mwa
binadamu kutokana na kula vitu
vilivyoingiwa na sumu hiyo, nchini

Marekani huathiri maelfu ya
watoto kuliko kiwango dhaifu cha
sumu hiyo kinachoweza kuwepo
katika vifaa vya kuchezea na
mapambo yanavyosafirishwa.
Afya ya binadamu pia huweza
kuathiriwa na watu
wanaomzunguka.

Iwapo una familia unayoiangalia
au marafiki katika jamii yako, basi
una nafasi kubwa ya kuimarisha
afya yako kuliko mtu ambaye
anaishi pekee au hana familia na
marafiki.
Uchunguzi uliofanywa na chuo
kikuu cha Washington nchini

Marekani umegundua kuwa,
ushirikiano wa kifamilia ni jambo
zuri kwa mtu na hupunguza kesi
za watu kujiua, hasa wale
wanaopatwa na matatizo ya
mfadhaiko wa kifikra au
wanapokuwa na fikra ya kutaka
kujiua.


Vilevile tamaduni, mila na desturi
za jamii na jinsi watu
wanavyozithamini itikadi hizo,
zina nafasi kubwa katika afya zao
ingawa matokeo yake huweza
kuwa mazuri au mabaya.
Kwa mfano mazoea na mila ya
kuwakeketa au kuwatahiri watoto
wa kike na wanawake ina

Madhara makubwa kama vile
kuongeza kiwango cha
maambukizo ya magonjwa na
hata matatizo ya kiakili miongoni
mwa wasichama na wanawake
wanaofanyiwa jambo hilo.

Urithi wa jenetiki
 
ni suala jingine
linaloathiri afya za watu. Kuishi
muda mrefu, siha ya mwili kwa
ujumla na kupatwa na baadhi ya
magonjwa na hata kuzaliwa nayo,
ni masuala yanayoainishwa na jinsi
jeni zetu zilivyo mwilini tangu
wakati tunapozaliwa.

0 comments:

Post a Comment