Sunday, 4 May 2014

FAIDA NA UMUHIMU WA KUMYONYESHA MAZIWA YA MAMA KWA WATOTO.



Maziwa ya mama ni mlo kamili wenye
 
virutubisho vyote vinavyotakiwa kwa
 
ukuaji wa mtoto mchanga.

Wataalamu wa lishe wanashauri
 
kwamba ni vyema mtoto azaliwapo
 
akanyonya maziwa ya mama kwa muda
 
wa miezi sita bila kuchanganyiwa na
 
kitu kingine kama vile, maji au maziwa
 
ya kopo au ya wanyama.

Kumchanganyia mtoto mchanga maziwa
 
mengine au kitu kingine tofauti na
 
maziwa ya mama, kitaalamu inaeleweka
 
kuwa ni kumhatarisha na magonjwa
 
mbalimbali, kwani mtoto mchanga
 
anahitaji uangalizi wa hali ya juu na
 
kinga yake dhidi ya maradhi hujengwa
 
kutokana na maziwa ya mama.

Hivyo mtoto anapochanganyiwa vyakula
 
au maziwa chini ya umri wa miezi sita ni
 
kumhatarisha na maambukizi ya
 
maradhi, hivyo kumfanya mtoto asikue
 
vizuri au kufa kutokana na maambukizi
 
ya maradhi.
Takwimu za lishe na afya
 
zilizotolewa hapa nchini zinaonesha
 
kwamba zaidi ya watoto wachanga
 
45,000 hufariki kila mwaka kutokana na
 
kutonyonyeshwa maziwa ya mama
 
ipasavyo au kwa wakati unaostahili.
 
Takwimu hizo ni kielelezo kwamba
 
baadhi ya jamii na wazazi hawatilii
 
mkazo umuhimu wa kunyonyesha
 
watoto wao, na hiyo inatokana na
 
sababu mbalimbali zikiwemo za kudai
 
maziwa ni kidogo au hayatoki.

Lakini
 
tafiti nyingine zisizo rasmi zimebaini
 
kwamba wapo baadhi ya mama
 
hawataki kunyonyesha watoto wao
 
pindi wazaliwapo kwa madai kuwa
 
wataharibu matiti yao!.

Taasisi ya Chakula na Lishe hapa nchini
 
imekuwa ikisisitiza watoto wachanga
 
kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa
 
wakati, ili kumjengea kinga mtoto na
 
kumfanya akue vizuri.
 
Wadau wa Lishe
 
katika Shirika la World Vision nchini,
 
wanasisitiza kuwa mtoto
 
mchanga anatakiwa kunyonya maziwa
 
ya mama kuanzia siku aliyozaliwa hadi
 
umri wa miaka miwili.

Wanasema Shirika hilo limekuwa likitoe
 
elimu mbalimbali kwenye jamii juu jinsi
 
ya kumnyonyesha mtoto kwani si
 
wakina mama wote wanaelewa ni muda
 
gani na kiasi gani mtoto anatakiwa
 
kunyonya.
 
 Wakizungumzia tafiti
 
mbalimbali zilizofanyika kuhusu
 
unyonyeshaji watoto wachanga,

Wanasema zipo tafiti zinazoonesha kuwa
 
hapa nchini asilimia 49, ya watoto
 
waliozaliwa huanza kunyonyeshwa
 
ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa.

 
Kadhalika, watoto zaidi ya asilimia 94,
 
huanza kunyonyeshwa ndani ya siku ya
 
kwanza baada ya kuzaliwa.

Wataalamu
 
wa lishe kutoka Taasisi ya Chakula na
 
Lishe (TFNC), wanasisitiza kuwa jambo
 
sahihi ni mama kumnyonyesha mtoto
 
wake ndani ya saa moja baada ya
 
kujifungua.

Hiyo inatokana na ukweli kwamba
 
maziwa ya kwanza ya mama huwa ni
 
mlo kamili wenye virutubisho vyote kwa
 
afya na kinga ya mtoto mchanga.

Hata
 
hivyo, kanuni hiyo haizingatiwi na mama
 
wengi na kwamba wengine huanza
 
kuwanyonyesha watoto wao baada ya
 
siku ya kwanza kuzaliwa.

Kwa mujibu wa taratibu na maelekezo
 
ya jinsi ya kunyonyesha mtoto kutoka
 
TFNC, ni kwamba mama aanzapo
 
kumnyonyesha mtoto anatakiwa
 
amnyonyeshe ziwa moja kwa muda
 
mrefu.
 
Kisha ziwa jingine amnyonyeshe
 
muda mwingine na kwamba mama
 
asiwe na haraka kunyonyesha mtoto
 
kwa muda mfupi na kisha kumkatisha.

 
Aidha anasema msisitizo umekuwa
 
ukitolewa pia pindi wajawazito
 
wanapohudhuria kliniki kwani hupewa
 
mafunzo na maelekezo jinsi ya
 
kunyonyesha watoto wao.

Endapo mama
 
watatilia maanani na kunyonyesha
 
watoto wao ipasavyo, upo uwezekano
 
wa kupunguza vifo vya watoto kwa
 
asilimia 22.

Faida za kunyonyesha mtoto
 
maziwa ya mama kuwa ni maziwa safi
 
na salama, hupatikana muda wote
 
katika joto sahihi kwa mtoto na
 
hayahitaji matayarisho.
 
 Kadhalika,
 
maziwa ya mama hayaharibiki ndani ya
 
titi na hata yakikamuliwa huweza kukaa
 
saa nane katika joto la kawaida bila
 
kuharibika, na saa 72,
 
kwenye jokofu.
 
Gharama yake ni ndogo ukilinganisha na
 
maziwa mbadala hivyo hupunguza
 
gharama za kununulia maziwa mbadala
 
na dawa.

 
Vilevile maziwa ya mama
 
hayaleti matatizo ya mzio (allergies)
 
kama pumu na magonjwa ya ngozi
 
 Mtoto asiachishwe
 
maziwa ya mama, bali anyone kila
 
anapohitaji; usiku na mchana ili
 
kuendeleza utokaji mzuri wa maziwa ya
 
mama.

Mtoto afikishapo umri wa
 
miezi sita aanzishwe chakula cha
 
nyongeza huku akiendelea kunyonya
 
maziwa ya mama. Mtoto apewe chakula
 
cha nyongeza kwa kutumia kikombe/
 
kibakuli na kijiko na vyakula vya
 
nyongeza viwe ni vya mchanganyiko wa
 
makundi.

Makundi hayo ni vyakula vya nafaka,
 
mizizi na aina za ndizi, vyakula vyenye
 
asili ya nyama, mboga na matunda,
 
mafuta na sukari (kwa kiasi). Vile vile
 
wataalamu wa afya wanashauri mtoto
 
aendelee kunyonya mpaka afikie umri
 
wa miaka miwili au zaidi na kusisitiza
 
kuwa, maziwa ya mama pekee ndio
 
chakula na kinywaji cha mtoto kwa
 
miezi sita ya mwanzo.

Wachambuzi wa masuala ya mtoto
 
wanasema, ikiwa mtoto ataanza
 
kunyonya maziwa ya mwanzo ambayo ni
 
ya njano, yana viini vingi vya kumkinga
 
dhidi ya magonjwa.

 
Watoto wanaopewa
 
maziwa ya mama pekee hawaugui mara
 
kwa mara, na wakiugua makali ya
 
ugonjwa hupungua na hupona
 
mapema.

Mtoto mchanga
 
hapaswi kupewa maji, kwani watoto
 
wanaonyonya maziwa ya mama pekee
 
hawapati kiu, kwa kuwa asilimia 80 ya
 
maziwa ya mama ni maji.

 
Hata nyakati za
 
joto kali, maziwa ya mama yanatosha
 
kukata kiu ya mtoto kwa miezi sita ya
 
 mwanzo.
 
Kwa utaratibu huo, ni wazi kwamba
 
mtoto hukua vizuri kwa kunyonya
 
maziwa ya mama kwa muda unaostahili
 
na tabia ya kuwapa maziwa mbadala si
 
chaguo jema kwa kuwa yana madhara.

Taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO),
 
zinasema kwamba asilimia 59, ya
 
watoto hawanyonyi maziwa ya mama
 
zao hali ambayo huhatarisha ukuaji wao
 
kwa kuwa maziwa mbadala ya
 
viwandani ndiyo hutumika.

Hata hivyo matumizi ya maziwa mbadala
 
kwa kwenye nchi nyingi yanatokana na
 
matangazo ya televisheni na vipeperushi
 
vingine, yenye ushawishi, ambayo
 
huwafanya watu wengi kushawishika
 
kuyatumia.

Unyonyeshaji bora wa
 
maziwa ya mama hupunguza kwa kiasi
 
kikubwa magonjwa na vifo vya watoto
 
wadogo.
 
Ili kufanikisha unyonyeshaji, wanawake
 
wanaonyonyesha wale chakula
 
mchanganyiko na cha kutosha. Ni
 
muhimu pia wasaidiwe shughuli
 
mbalimbali ili wapate muda wa
 
kupumzika na kunyonyesha vema.

Baadhi ya wanajamii wanaweza kuunda
 
vikundi vya kuelimishana kuhusu ulishaji
 
bora wa watoto wadogo kwani hii
 
itasaidia katika kutatua matatizo
 
mbalimbali yanayohusu ulishaji wa
 
watoto.

Hata hivyo wataalamu wamekuwa
 
wakishauri kuwa kumnyonyesha mtoto
 
ndio njia bora ya kumsaidia kuimarisha
 
mfumo wake wa kinga.
 
Maziwa
ya mama yana kinga zote muhimu na
 
mtoto akinyonya kwa muda upasao
 
madhara kama hayo yanaweza
 
kuepukika.

Wataalamu wa afya wakisema
 
hayo, kwenye jamii kuhusu suala la
 
Kumyonyesha mtoto
 
 bado suala la mtoto
 
halipewi kipaumbele kwenye
 
unyonyeshaji wa maziwa ya mama,

Bali
jamii hukimbilia matumizi ya maziwa
 
mbadala.

Maziwa mbadala hivi
 
sasa yamepewa kipaumbele na wazazi
 
wengi hivyo watoto wengi
 
hawanyonyeshwi ipasavyo maziwa ya
 
mama.

“Utandawazi na huku kuiga kwenda na
 
kisasa ndiko kunakoangamiza watoto
 
wetu, wengi wetu tumeacha
 
kunyonyesha watoto tumehamia
 
kwenye maziwa ya makopo ili tuende na
 
wakati

2 comments:

  1. Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

    Kwaheri Gerd Ulrich

    ReplyDelete
  2. Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe nikiwa nimesimama peke yangu bila mwili kusimama na mimi na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na mchawi huyu wa hodari Dk. ASUBUHI, baada ya kumueleza hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi akiniomba kuwa hatawahi. niache tena, miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa pia una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
    *penda uchawi
    * kama unataka ex wako nyuma
    * Acha talaka
    *kuvunja mawazo
    * huponya viharusi na magonjwa yote
    * uchawi wa ulinzi
    *Ugumba na matatizo ya ujauzito
    Wasiliana na Dk DAWN kwa barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
    Whatsapp: +2349046229159

    ReplyDelete