Thursday, 1 May 2014

SEHEMU YA PILI; MAGONJWA YA AKILI YA NGONO YANAYOSUMBUA WATANZANIA WENGI ( EXHIBITIONISM)


Inaendelea toka makala sehemu ya kwanza nah ii ni sehemu ya pili
endelea
Kuwabaka wanyama
Hili limeshawahi kuandikwa na vyombo kadhaa vya habari na kuwashangaza watu wengi duniani ikiwemo pia katika Tanzania.
Zipo ripoti kadhaa za watu kuwabaka wanyama hasa wale wafugwao kama kuku, mbuzi, farasi na ngombe.
Kwa mfano, Kijana mmoja mkazi wa mkoa wa Tanga alifikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kumbaka na kumwingilia kinyume cha maumbile mbuzi wa jirani yake.

Katika tukio jingine, Yusuph Bakari mkazi wa Kata ya Kigera, Manispaa ya Musoma Mkoani Mara alinajisi kuku jike na kumsababishia maumivu makali na kusababisha afikishwe kwa afisa mifugo kwa uchunguzi zaidi.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Absalom Mwakyoma alithibitisha tukio hilo.
Huu ni  miongoni mwa magonjwa ya akili ya ngono na kwa kitaalamu ugonjwa huu unaitwa zoophilia na ni kosa la jinai katika nchi nyingi ikiwemo Tanzania.
 
Ndani ya daladala
Wanawake wengi wamekuwa wakilalamika kuwa wanapopanda katika magari ya abiria hasa nyakati za asubuhi au jioni pindi mabasi yanapokuwa yamejaa kupindukia, wapo wanaume ambao huwasogelea na kuwabana kwa kiasi kikubwa.
“Basi kama umewahi kukutana na hali hiyo ujue umekutana na wanaume wenye ugonjwa wa akili uitwao ‘ufroteri’. Ugonjwa huu wa akili huwakumba zaidi wanaume ambao hupenda kujisugua via vyao vya uzazi kwa watu wasio na ridhaa.
“Mara nyingi hutokea katika maeneo ya umma, au yenye msongamano. kila wanapogundua kuwa wameonekana wakifanya tendo hilo, hisia zao huisha hapo hapo na huondoka,”.
mara nyingi watu hawa si kuwa hawana wenza  bali wanapata hisia zaidi wanapojisugua katika maumbile ya mwanamke ambaye hafahamu nini kinaendelea.
 
Kipigo, majeraha
Umeshawahi kupata tetesi za wanawake ambao kila mara huamka na majeraha makubwa usoni na mwilini?
Usishangae kusikia kuwa mwanamke  huyo ana mwenza mwenye matatizo ya akili ya ngono.
Upo ugonjwa wa akili ya ngono ambao unahusisha vitendo halisi vya kujeruhi au kusababisha maumivu au kutoa manyanyaso.
“Kinachompa raha ya tendo hilo ni kumpiga mwenza wake, kumtukana wakati wa tendo au kumjeruhi, kumng’ata na kumuona akilia kwa uchungu au akitoka damu,”
Mtaalamu huyo anasema hali hii inapozidi huweza kusababisha  mauaji au majeraha ya kudumu na watu wengi hudhani ni manyanyaso ya kijinsia ya kawaida.
watu wengi wa kundi hili wamepata maradhi hayo kutokana na historia za maisha yao.
“Wengine waliwahi kubakwa, kuteswa au kufanyiwa vitendo kama hivi na hawakupata msaada wa kisaikolojia kuondoa ule uchungu. Hivyo wanaweza kuwa na matatizo haya kiufahamu”
Hapa Dk Ndaluka anasema hatua za kisheria zinahitaji kuchukuliwa ili kumlinda mwenza ambaye huathiriwa.
 
Kupiga chabo
Upo ushahidi kuwa baadhi ya vijana hudiriki kutoa fedha kwa walinzi au wahudumu wa nyumba za wageni ili wawape ruhusa ya kuangalia watu wanaofanya mapenzi   katika vyumba.
Lakini tofauti na wengi wanavyofikiri huu si ukosefu wa maadili tu, bali ni ugonjwa wa akili ya ngono ambao mtu hupenda kuwaangalia watu wanaofanya mapenzi, ambao ni wageni machoni pake (si ndugu wala jamaa)  na kukamilisha raha ya ngono. Kwa kitaalamu ugonjwa huu wa akili huitwa ‘voyerism’.
Kwa mfano,  Mhudumu wa Nyumba ya wageni ya Savannah iliyopo  Tabata, Ndosi Yakobo  anakiri na kusema kuwa vijana huomba kuja kuwachungulia wapenzi wanaoingia humo.
“Ieleweke kuwa watu wa aina hii hawana nia ya kufanya ngono na watu wanaowachungulia, na wanapogundulika tu kuwa wanafanya hivyo zile hisia huisha papo hapo,”
Watalaamu wa magonjwa ya akili wanaeleza kuwa watu wa kundi hili wanaweza  pia kupenda kuwatazama watu wakivua nguo au watu waliokaa utupu.
 
Mapenzi kwa njia ya simu
Wapo watu ambao hupata hisia za ngono kwa kuzungumza lugha ya matusi inayohusisha viungo vya mwili au vitendo vya kingono.
Huu ni ugonjwa wa akili ambao baadhi ya watu wanao pasipo kujua kuwa ni ugonjwa.
Baada ya teknolojia ya simu kuvumbuliwa,  ugonjwa huu umekithiri na sasa watu wenye tatizo hilo wanatumia simu kufanya mapenzi au kuzungumza lugha ya matusi, kisha kupata hamu ya mapenzi.
Kitaalamu, mapenzi kwa njia ya simu huitwa, ‘telephone scatologia’ na hivi sasa watu wanaweza kujiunga na huduma fulani ambayo huzungumza njia za kufanya ngono au jinsi ya kumfurahisha mwenza na kumbe kwa njia hiyo watu wanatimiza haja zao.
Ugonjwa mwingine unaoendana na huu ni ule wa kupata hisia za ngono kwa njia ya mitandao ya kijamii. Wanatumia  intaneti kuzungumza habari za ngono hadi wanatimiza haja zao.
“Huu ni ugonjwa unaoathiri zaidi na unawaathiri vijana. Mara nyingi wakianza hawawezi kuacha hadi watibiwe,”
Hata hivyo, yapo magonjwa mengine ya akili ya ngono madogo madogo ambayo yanaathiri watu wengi kwa mfano wapo watu wana mwamko mkubwa mno wa tendo la ngono kiasi cha kushindwa kulala wasipofanya hivyo.
wakati sasa watu kupata ushauri wa kisaikolojia na matibabu na wakubali kuwa haya ni magonjwa ya akili na siyo tabia.
kutokana na uelewa mdogo  wa magonjwa ya akili ya ngono watu wengi wamefungwa kwa sababu ya kuwajeruhi wenza wao nakuwabaka watoto wadogo.
kuhusu ugonjwa wa akili wa kuwabaka watoto (paedophilia) na kusema kuwa watu kama hawa wanaweza kuwa hatari katika jamii hivyo wanahitaji matibabu.
Nashauri kuwa wazazi wawalinde watoto na waache tabia ya kuacha mtoto apakatwe au kuogeshwa na kila mtu.
“Hawa mapedophilia ni wengi hapa nchini, bila kupewa matibabu na sheria kuchukuliwa watoto wengi wapo hatarini”
Licha ya matibabu ya kisaikolojia pia wagonjwa hawa huweza kupewa dawa za kupunguza kiwango cha vichocheo
                                      MWISHO WA MAKALA HII

0 comments:

Post a Comment