Huenda
tumewaona wengi wao kama mashujaa, vijana wa kisasa au hata dada zetu
wanaokwenda na wakati, kumbe ni wagonjwa wa akili.
Unasikiliza
taarifa ya habari kwenye vyombo vya habari.
Unasikia
kuwa, mwanamume amembaka mtoto wa miezi mitatu. Unaihoji nafsi yako. ni jambo
gani lililosababisha akafanya ukatili huo? Je, ni tamaa kali ya ngono?
Wengine
hudhani ni kisasi au imani za kishirikina na kwamba wahusika wametumwa.
Huu
ni upotoshaji, lakini ukweli ni kuwa hayo ni magonjwa ya akili ya ngono ambayo
yanawakumba asilimia 35 au zaidi ya Watanzania wote.
Watanzania
hawa wanaugua magonjwa haya kwa wakati mmoja na kusababisha madhara mbalimbali
kijamii, kiuchumi na migogoro katika familia na katika uhusiano.
Watu
wenye magonjwa haya, si lazima watembee wakiokota makopo, kuvua nguo au kuwa na
nywele ambazo hazijachanwa.
Hawa
ni watu wa kawaida ambao tunafanya nao kazi, wenye uwezo mkubwa katika taaluma
au pengine ni wazazi au hata walezi.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Akili na mtaalamu wa waathirika wa dawa za kulevya,
Augustine Godman anasema, magonjwa ya akili kwa ujumla wake yanaweza kuzidi
1,886 lakini yapo yale ya ngono ambayo pengine yana changamoto lukuki kwa
mwanadamu hasa Watanzania wasiofahamu kuwa ni magonjwa ya akili.
Magonjwa
ya akili ya ngono kuwa ni yale
yanayohusisha athari , upungufu au
mparaganyiko au vitu visivyo vya kawaida katika tendo la ngono.
“Mtu
anaweza kuwa na matatizo ya kihisia au
ya kisaikolojia au vya kitabia katika
suala la ngono na huweza kusababisha madhara au kutopata mafanikio,”
Daktari
huyu ambaye amewahi pia kufundisha Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili
(Muhas), kitengo cha magonjwa ya akili anasema
watu wengi wana magonjwa ya akili ya ngono, lakini hawajui kama ni
magonjwa na wanaendelea kuishi hivyo
hivyo wakidhani ndivyo walivyo na baadhi wakipata matatizo katika jamii,
wengine kufungwa jela au kupigwa kutokana na tabia hizo.
Mara
nyingi tumekuwa tukiona wanawake wanavaa mavazi ya nusu uchi, wakizianika nje sehemu kubwa za miili yao.
Tabia
hizo ambazo pengine huweza kuigwa na
wengine ni miongoni mwa magonjwa ya
akili ya ngono kwani watu wanaopenda kufanya hivyo hujisikia raha na amani watu
baki au wageni wenye jinsi tofauti wanapoyaangalia maungo yao na kushtuka.
“Kwa
kitaalamu, ugonjwa wa akili ya ngono wa kupenda kuacha mwili wazi unaitwa ‘exhibitionism’ ambapo mtu huweza
kuamua kuacha maziwa, mapaja au kwa wanaume kuvaa suruali inayoelekea kuanguka
kutoka maungoni,”
Watu
aina hii hutosheka kimapenzi mara tu wanapoona wanaume au wanawake wengine
wameyaona maungo yao. Hata hivyo,
anasisitiza kuwa hutosheka pale tu watu wageni wanapoyaona maungo yao.
Mhadhiri
wa Sosiolojia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Thomas Ndaluka anasema, baadhi
ya magonjwa haya yanasababishwa na historia ya mtu.
Anasema
hata hivyo mparaganyiko kama ule wa kupenda kuacha maungo wazi, unaambukiza kwa
maana ya kuwa, anayeanza kufanya hivyo ni mgonjwa wa akili na matokeo yake
wengine wanaiga.
Ubakaji
wa watoto wachanga
Wengi
wamekuwa wakihusisha ugonjwa huu na imani za kishirikiana, lakini ukweli ni
kuwa, wale wanaowabaka watoto wadogo au kuwalawiti wana matatizo ya akili
ambayo kitaalamu yanaitwa pedophilia (paedophilia).
“Katika
hali ya kawaida si rahisi mtu mzima akamtamani kimapenzi mtoto wa miezi
mitatu,” anasema mtaalamu huyo.
Ugonjwa
huu unatokea pale mtu anapokuwa na hali ya kupata raha ya ngono kwa watoto
wadogo wenye umri wa chini ya miaka mitano.
“Watoto
wa jinsi zote huweza kuathiriwa na tatizo hili. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza
kuamua kumuingilia mtoto au tu kuamua kumchezea via vyake vya uzazi,”
Mhadhiri
wa Saikolojia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Kitila Mkumbo anasema sababu kuu
za maradhi hayo ya akili ni pamoja na mazingira ya mtu wakati wa balehe,
aliambiwa nini kuhusu tendo la ndoa na makuzi yake kwa jumla.
“Kwa
mfano inategemea kijana anaambiwa nini
wakati wa balehe au yeye mwenyewe anaelewa nini maana ya tendo hilo” anaeleza
Dk Mkumbo.
Anatoa
mfano kuwa, wapo baadhi ya wanaume wanaamini au kufananisha kila shimo na uke.
“Huu
ni ugonjwa mkubwa sana. Ndiyo maana utasikia mtu kambaka mbuzi. Yeye anaamini
kila shimo linaweza kutumika kama uke”,
Anafafanua
kuwa magonjwa mengi ya akili ya ngono hujitokeza wakati wa balehe na hukua kadri mtu anavyokosa matibabu.
Yapo
matukio kadhaa yaliyowahi kutokea hapa nchini yanayoeleza watu waliowabaka
watoto wadogo.
Kwa
mfano, Desemba 2012, Yakobo Raymond alifikishwa mahakamani huko wilayani
Muheza, Mkoani Tanga kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu.
Pia,
huko mkoani Arusha, mwezi Januari mwaka jana, David Samweli mkazi wa Moivaro Wilaya ya Arumeru,
aliwabaka watoto wawili wa kike wa jirani yake na mtoto wake wa kumzaa kwa nyakati tofauti chumbani kwake.
Licha
ya matukio kama haya kuripotiwa zaidi
kwa wanaume wenye tabia hii, Dk Godman anasema wapo wanawake ambao pia huwabaka
watoto wadogo wa kiume.
“Mwanamke
anaweza kumvua nguo mtoto mdogo na kuanza kumshikashika tu, hapo huwa
amepata raha yake. Lakini pia anaweza
kuamua kumwacha mtoto akiwa uchi,”
Mtu
mwenye ugonjwa huu humrubuni mtoto kwa vitu vidogo vidogo ili ampende na
kumweka karibu naye na wakati mwingine baada ya kumfanyia vitendo hivyo
humtishia kuwa akisema, atamdhuru.
Tafiti
mbalimbali zinaeleza kuwa, wapo watu katika nchi zilizoendelea ambao
huasili watoto, kisha kuwatendea vitendo
hivi vya upedofilia.
Kufanya
mapenzi na maiti
Ni
jambo ambalo huzungumzwa au kutajwatajwa, lakini kumbe lina ukweli ndani yake.
Wengine
wamekuwa na hisia kuwa linahusiana na imani za kishirikina au utumiaji wa dawa
za kulevya lakini kumbe ni miongoni mwa magonjwa ya akili.
Wapo
watu ambao hujisikia raha ya ngono kwa kufanya mapenzi na maiti. Watu hawa kwa
kitaalamu huitwa ‘necrophilia’.
“Kwa
kawaida ugonjwa huu huwa hauripotiwi mara kwa mara kwa sababu ya hofu ya kukiri
kuwa umefanya mapenzi na maiti pia wanaotenda matendo hayo”
magonjwa
haya ya akili yana tiba ambazo zaweza kuwa ni za kisaikolojia, sosholojia na kwa dawa.
“Kisaikolojia
tiba ya watu hawa ni kupewa unasihi wajue kuwa wao ni binadamu na waache tabia
ambazo kwa kawaida hazifanywi na binadamu” anasema Dk Mkumbo.
HII
NI SEHEMU YA KWANZA YA MAKALA HII YA MAGONJWA YA AKILI YA NGONO YANAYOSUMBUA
WATANZANIA WENGI; EXHIBITIONISM
Itaendelea
kwenye post itakayofata na tutaanza kuzungumzia
watu wanaobaka wanyama!!!!!!!!
0 comments:
Post a Comment