Thursday 1 May 2014

UKWELI KUHUSU VITAMINI A NA MAABUKIZI YA MINYOO.



 VITAMINI A NI NINI?
Vitamini A ni moja wapo ya virutubisho muhimu katika kipindi chote cha masiha ya binadamu. Vitamini A huhitajika mwilini kusaidia macho kuona vizuri, ukuaji na maendeleo ya mtOto na kuimarisha kinga ya mwilini dhidi ya maradhi mbalimbali.

Mwili wa binadamu hauwezi kutengeneza vitamin A, hivyo vitamin A inapatikana kwenye vyakula tu. Aidha vyakula vyenye viatamini A kwa wingi vitokanavo na wanyama, mfano maziwa ya mama na maziwa ya wanyama wengine, mtindi, siagi, jibini, smaki, ini, kiini cha yai na vile vitokanavyo na mimea kama vile, mboga za majani zenye rangi ya kijani kibichi, matunda yenye rangi ya majano, mafuta ya mawese, mazao ya mizizi kaka karoti na viazi vitamu vyenye rangi ya majano.
Lakini pia vitamin A hupatikana kwenye vyakula vilivyoongezewa kirutubishi hiki kwa watoto wachanga na wadogo chanzo bora zaidi cha vitamin A ni maziwa ya mama.
 
KWANINI UPUNGUFU WA VITAMINI A NI TATIZO NCHINI TANZANIA.
Maziwa ya mama ni chanzo pekee cha vitamin A kwa motto kwa miezi 6 ya mwanzo;
·        Lakini watoto wachache tu Nchini Tanzania wananyonyesha maziwa ya mama pekee bila kupewa kinywaji au chakula kingine hadi wanapofikia umri wa miezi 6 na kasha kuendelea kunyonyesha maziwa ya mama hadi kufikia umri wa miaka miwili au zaidi.
·        Vyakula wanavyopewa watoto wadogo havina vitamin A ya kutosheleza mahitaji yao kwa sababu hula kiasi kidogo cha chakula na familia nyingi hazifahamu vyakula vyenye vitamin A kwa wingi.
·        Familia haziwezi kumudu kuwapa watoto wao vyakula vyenye vitamin A kwa wingi.
·        Vyakula vya gharama nafuu vyenye vitamin A kwa wingi havipatikani kwa misimu yote katika mwaka
·        Vitamini A iliyomo kwenye chakula hupotea wakati wa matayarisho.
·        Maradhi kama vile kuharisha, surua na maradhi ya mfumo wa hewa husababisha upungufu wa vitamin A mwilini.
 
KWA NINI MAAMBUKIZI YA MINYOO NI TATIZO NCHINI TANZANIA?
·        Maambukizi ya minyoo hutokea kwa kula chakula chenye minyoo hai au manyai ya minyoo (kama vile kachumbari) au kissichopiwa vya kutosha.
·        Kunywa maji ya kunywa yenye minyoo hai au mayai ya minyoo au maji yasiyochemshwa.
·        Kutembea bila viatu au kuchezea udongo uliochafuliwa na kinyesi
·        Uchafuzi wa mwili na mazingira, hasa kwa mtayarishaji na vyombo vya kulia chakula na mazingira ya kulia chakula.
 
WAATIRIKA WAKUBWA WA TATIZO LA UPUNGUFU WA VITAMINI A NA MAAMBUKIZI YA MINYOO NI AKINA NANI?
·        Watoto wadogo huathirika zaidi na tatizo la upungufu wa vitamin A na maambukizi ya minyoo kutokana na sababu mbalimbali. Aidhaa wanawake wajawazito huathirika zaidi na tatizo la upungufu wa vitamin A.
·        Watoto wanahitaji vitamin A kwa ukuaji na maendeleo mazuri na kuimarisha kinga dhidi ya maradhi mbalimbali ya utotoni, upungufu wa vitamin A kwa watoto unaweza kusababishwa na ulaji duni ikiwa ni pamoja na kutonyonya vizuri maziwa ya mama, kuwalisha watoto vyakula vya nyongeza visivyokuwa na vitamin A kwa wingi au maziwa mbadala wa maziwa ya mama, kuwaachisha watoto kunyonya maziwa ya mama mapema kabla ya kutimiza umri wa miaka miwili, kiwango kisichokidhi cha vitamin A kwenye maziwa ya mama kutokana na lishe duni na maambukizi ya maradhi,
·        Watoto wenye umri chini ya miaka mitano hupata maambukizi ya minyoo mara kwa mara kutokana na tabia ayao ya kucheza kwenye kwenye udongo na mazingira machafu.
·        Wanawake wanahitaji vitamin A mwilini kwa ajili ya kusaidia ukuaji wa mimba. Pia wanahitaji vitamin A mwilini ili kuboresha hali ya vitamin A ya mama anayenyonyesha.
 
MADHARA YA UPUNGUFU WA VITAMINI A NA MAAMBUKIZI YA MINYOO WA WATOTO NA WANAWAKE NI YAPI?
Vitamin A inahitajika kwa ajili ya ukuaji na maendeleo mazuri ya motto, ikiwa ni pamoja na mifupa na macho.Upungufu wa vitamin A unahusishwa na ongezeko lavifo vya wanawake vinavyotokana na uzazi na vifo vya watoto, kutoona vizuri katika mwanga hafifu, watoto kuzaliwa kabla ya miezi 9 ya ujauzito, kasi ndogo ya ukuaji na maendeleo ya motto na kuongezeka kwa uwezekano wa mtoto kupata maradhi kama vile kuharisha na magojwa ya mfumo wa hewa.
Aidha madhara ya maambukizi ya minyoo yanatofautiana kutegemeana na aina ya minyoo, umri wa aliyeambukizwa, wingi wa ninyoo na afya na lishe kwa ujumla.
Madhara ya maambukizi ya minyoo kwa wanawake na watoto ni pamoja na kusababisha upungufu wa virutubishi hasa madini ya chuma na vitamin A mwilini, kupungua uzito, ukuaji na maendeleo duni ya mtoto na kuziba kwa utumbo. Matokeo ya ukuaji na maendeleo duni kwa kwa mtoto  ni udumavu huathiri uwezo wa akili, ubunifu na utambuzi wa mambo mbalimbali.
 
 
NJIA ZA KUZUIA UPUNGUFU WA VITAMINI A NA MAAMBUKIZI YA MINYOO NI HIZI.
Kuna njia mbalimbali za kuzuia tatizo la upunguf wa vitamin A na minyoo kwa watoto ambazo ni;
·        Unyonyeshaji maziwa ya mama pekee katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo ya mtoto na kuendelea kunyonyesha hadi miaka miwili na zaidi na kumpa mtoto chakula cha nyongeza ama ziada chenye vitamin A kwa wingi.
·        Kumlisha chakula mchanganyiko na cha kutosha, ikijumuisha vya vyenye vitamin A kwa wingi.
·        Kutoa nyongeza ya vitamin A kwa watoto yaani matone ya vitamin A
·        Kuongeza vitamin A kwenye vyakula.
·        Kupata elimu ya lishe kuhusu umuhimu wa vutamini A na inakopatikana kwa wingi.
·        Kuzingatia usafi wa mwili na mazingira ikiwemo matumizi ya choo ili kidhibiti maambukizi ya minyoo.
·        Kutumia dawa za minyoo kwa makundi yaliyo kwenye hatari ya kuambukizwa.
·        Kutayarisha na kula chakula kwenye mazingira masafi na salama.
Matumizi ya matone ya vitamini A pamoja  na dawa ya minyoo yameonyesha kuwa ni nyia ya gharama nab yenye ufanisi inayoweza kutumiwa na nchi ili kuzuia na kutibu  upungufu wa vitamin A mwilini na maambukizi ya minyoo.
Utoaji wa matone ya vitamini A unafaida kwa mwili wa binadamu unauwezo wa kuhifadhi kiasi kikubwa cha vitamin A kwenye Ini. Hifadhi hii ya vitamin A mwilini inaweza kutumika kwa kipindi cha miezi minne hadi sita , hivyo utoa wa matone ya vitamin A kwa watoto kila baada ya miezia  6 ni mbinu bora ya kuwakinga dhidi ya athari mbaya za uoungufu wa vitamin A mwilini.
Ni muhimu mtoto apate matone ya vitamin A kila baada ya miezi 6, vinginevyo akiba ya vitamin A iliyopo kwenye Ini lake inaweza kupungua na kuisha kabisa.
 
KWANINI UTOAJI WA MTONE YA VITAMINI A NA DAWA YA MINYOO NI MUHIMU.
Matone ya vitamin A huokoa maisha ya watoto kwa kuwalinda dhidi ya maradhi ikiwemo kuharisha, surua, na ya mfumo wa hewa na husaidia kuzuia upofu. Watoto wasiopata matone ya vitamin A wanauwezekano mkubwa zaidi wa kuugua maradhi, kupofuka na hata kufariki dunia. Hali kadhalika, dawa ya minyoo huua minyoo na kuhakikisha virutubisho vilivyomo kwenye chakula alacho motto vinamfikia mtoto peke yake.
 
WAZAZI WANAPASWA KUFAHAMU NINI?
Kila mzazi/mlezi wa motto mdogo anapaswakufahamu umuhimu wa vitamin A na dawa ya minyoo kwa ukuaji, Maendeleo mazuri, afya na uhai wa mtoto. Vilevile vyakula tulavyo havikidhi mahitaji ya vitamin A ya watoto kwani hula kiasi kidogo wakati mahitaji yao ni makubwa na hivyo ni muhimu wapatiwe matone ya vitamin A na dawa ya minyoo mara mbili kila mwaka.
 
AKINA NANI WANAHITAJI VITAMINI A YA NYONGEZA NA DAWA YA MINYOO.
Kila motto mwenye umri wa kati ya miezi 6 na miaka mitano anahitaji kupewam matone ya vitamin A mara mbili kwa mwaka. Aidha, watoto wote wenye umri wa mwaka mmoja hadi miaka mitano wanahitaji kupewa dawa za minyoo mara mbili kwa mwaka.
Nchini Tanzania matone ya vitamin A hutolewa kwa watoto mara mbili kwa mwaka mwezi wa 6 (juni) na mwezi wa 12 (dicember) wakati wa zoezi la utoaji wa matone ya vitamin A watoto wote wenye umri wa mwaka Mmoja hadi miaka mitano hupatiwa pia dawa ya minyoo.

0 comments:

Post a Comment