Saturday 3 May 2014

MSAIDIE MTOTO KUCHAGUA VYAKULA




MOJA kati ya mambo makubwa ambayo
mzazi anapambana nayo katika kazi ya
 
malezi ni namna mtoto anavyokula. Kuna
matatizo mengi katika hili.

 
Wapo watoto wanaopenda kula aina ya
vyakula ambavyo si vizuri kwa afya zao.
 
Hawa ni wengi sana. Lakini wapo watoto
ambao wanapenda kula kupita kiasi na
wapo ambao hawapendi kula.
 
Haya ni matatizo ambayo mzazi anaweza
kukabiliana nayo kwa kumfundisha mtoto
namna bora ya kula.

Hii inahusisha aina ya vyakula anavyopaswa
kula, kiwango chake na wakati gani wa kula.
 
Kama hili halifanyiki vema, kuna hatari mtoto
akakabiliwa na matatizo yanayotokana na
kutokula vizuri.
 
Aidha mtoto atakuwa na uzito mkubwa au
atakuwa na uzito pungufu au hata utapia
mlo.
 
Wapo baadhi ya watu wazima leo hii ambao
wanahangaika sana kupunguza uzito wao
aidha kwa kufanya mazoezi au kupangilia
milo yao.

Ukichunguza kwa umakini unaweza kubaini
kuwa asili ya matatizo ya uzito
 
wanayokumbana nayo leo yanatokana na
tabia mbaya ya ulaji walipokuwa watoto
wadogo.
 
Hivyo, ni vizuri wazazi wakaweka mkazo
mkubwa katika suala la kuwafundisha
 
watoto wao namna bora ya kula kwa
sababu iwapo hawatakula vizuri hivi sasa,
 
matatizo yanaweza yasijionyeshe sasa hivi
bali baadaye sana katika maisha yao.
 
Wakati utakapokuwa unamfundisha mtoto
wako namna bora ya kula, kumbuka kuwa
mambo yote unapaswa kuyaonyesha kwa
vitendo.

Kama kula ‘ice cream’ kupita kiasi ni jambo
baya, basi mtoto asikuone wewe ukizila
 
kupita kiasi wakati yeye anakatazwa
kufanya hivyo.
 
Kama ukiwa unamkataza yeye kula ice
cream kupita kiasi wakati wewe mwenyewe
 
unakula, atakuona kuwa ni mchoyo na
mdanganyifu. Hatoshika mafundisho yako
sawasawa.

Lakini suala la namna bora ya kula si tatizo
kwa watoto wadogo tu.
 
Ni tatizo pia miongoni mwa vijana. Utafiti
uliofanywa na taasisi kadhaa duniani
 
umeonyesha mathalani zaidi ya nusu ya
vijana wa kike na zaidi ya theluthi mbili ya
 
vijana wa kiume wana tabia ya kula vitu
ambavyo vinadhuru afya zao, hasa kwa
upande wa uzito wa mwili.

Kuna mambo ambayo wewe mzazi
unapaswa kuwafundisha watoto wako
 
kuhusiana na jinsi ya kuchunga uzito wao.
Mambo haya yanaweza kukusaidia hata
wewe mwenyewe iwapo unakabiliwa na
tatizo la uzito.
 
Kumbuka kuwa unapofanya wewe yale
unayowafundisha watoto, nao watashika
mafundisho vizuri zaidi na kwa wepesi.
 
Haya ni baadhi ya mambo ambayo unaweza
kuyafanya na kuwafundisha watoto.
Usiwalazimishe watoto kufanya ‘diet’
 
Ingawa kwa watu wazima kufanya ‘diet’ ni
kitu ambacho kinashauriwa pale
unapopanga kupunguza au kuongeza uzito,
kwa watoto ni jambo lisilofaa.
 
Na njia bora zaidi ya kuliepuka ni
kuhakikisha kuwa milo inapangiliwa kwa
namna ambayo haitalazimisha hapo
 
baadaye mtu kufanya diet kama njia ya
kudhibiti uzito wake.

Mazoezi yawe jambo la kawaida
Tangu awali mazoezi yafanywe kuwa jambo
la kawaida katika maisha ya mtoto.
 
Mazoezi yasiingizwe kama programu
maalumu kwa ajili ya jambo fulani, ionekane
kuwa ni sehemu ya kawaida ya maisha.
 
Mazoezi si lazima yawe ya kufanya kwenye
gym. Kuna aina ya mazoezi ambayo yanaleta
pia furaha kwa familia kama vile kuendesha
 
basikeli pamoja, kucheza mpira, kuruka
kamba pamoja na mambo yanayofanana na
hayo.

Kuwe na mazungumzo chanya
Linapokuja suala la afya na hasa kuhusu
uzito msiwe na mazungumzo
 
yanayoonyesha kumtania mmoja wenu
ambaye ana uzito mkubwa. Mazungumzo
pia yasiwe ya kuonyesha kushindwa
 
kudhibiti uzito au afya kwa ujumla.
Mnachozungumza mara nyingi ndicho
ambacho mtakifanya na huenda kikatokea
hivyo hivyo.

Kwa hiyo, mkizungumzia kushindwa
kudhibiti uzito, kuna uwezekano mkubwa
kweli mtashindwa suala hilo.
Msiwacheke wenzenu
 
Nimeeleza hapo juu kuwa mazungumzo
yawe ni chanya na hiyo ijumuishe pia
kutowatania ambao hawajafanikiwa
 
kudhibiti uzito au afya zao. Watu asiitwe
majina yanayotokana na umbile lao.
Baada ya kutaja mambo hayo, ni muhimu
 
pia kwa mzazi kufahamu kuwa unene kwa
baadhi ya watu ni kitu cha kurithi.

Hivyo, mnapohangaika kumwezesha mtoto
kupunguza uzito ni vema pia kuangalia
 
kama hali ya uzito wake inatokana na kula
tu au na sababu nyingine.
Mnaweza kubaini kuwa unene wake
 
unatokana na vinasaba ambavyo amerithi
kutoka kwa wazazi wake.
Na suala hili la kurithi vinasaba vya wazazi
liangaliwe kwa upana pia.
 
Mzazi anaweza kuwa na vinasaba alivyorithi
kutoka kwa wazazi wake ambavyo sifa zake
hazionekani kwa wazazi wake na kwake
pia.

Mtoto anaweza kuonyesha sifa ya vinasaba
vya vizazi hata vinne au zaidi vilivyopita.
Hivyo, mzazi usishangae wakati mtoto wako
anaonyesha unene uriokithiri wakati wazazi
wake wote ni wembamba.

0 comments:

Post a Comment