Mayai ya mwanamke ni mojawapo ya
viungo ambavyo vimeshatengenezwa kabla hata mwanamke hajazaliwa, yaani tangia
akiwa fetus ndani ya tumbo la mama yake.
Haya mayai yanakuwa tayari pale
msichana anapopata menstruation yake ya kwanza average ya miaka 12 hadi 14.
Kuanzia hapo hadi pale atakapofikia menopause/kikomo cha menstruation kwa
mwanamke (average miaka 51) mayai yake na fertility yake hupungua anavyozidi
kuzeeka.
Yaani katika ujana wake, teenage na
20s ni muda ambao ni rahisi zaidi kutunga mimba. Na kuanzia miaka 30 had 51
uwezo huu unapungua kwa kiasi kikubwa mpaka unapoisha kabisaa.
Wakati kwa wanaume wao sperm cell
zinaanza kutengenezwa pale wanapo balehe(puberty age) mpaka siku atakayo kufa.
Hii inamaanisha kama mwanaume akiwa katika hali nzuri ya kiafya anaweza kumpa
mimba mwanamke hadi afikapo uzeeni iwapo mwanamke bado hajafikia menopoase na
ni fertile.
Zingatia mambo haya
sasa
Moja, Ingawa unene unaweza kumzuia
mtu asishike mimba lakini kufanya mazoezi sana na kuwa na uzito mdogo sana wa
zaidi ya kilo 50 huweza pia kumsababisha mtu asishike mimba. Mazoezi ya
kupindukia pia huathiri homoni mwiilini.
Pili, Kuwa na fikra nyingi na msongo wa mawazo
'stress' huweza pia kauthairi uwezo wa mtu wa kushika mimba.
Tatu, Kutokula vizuri na kutopenda
kula kwani humkosesha mwanamke au hata mwanamme baadhi ya virutubisho muhimu
vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanikisha suala la kushika mimba (nitazungumzia
vyakula vinavyosaidia kushika mimba baadaye)
Nne, Sigara, marijuana na pombe ni
miongoni mwa vitu ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa kubeba mimba. Mwanamke
anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara.
Mwanamume pia anashauriwa kuacha kuvuta sigara kwani sigara huathiri kiwango cha
mbegu za kiume za mwanamme.
Tano, Endelea tu na tendo la ndoa
bila kuchoka au kukata tamaa, lakini ni bora nguvu zihifadhiwe kwa siku chache
kabla ya Ovulation na siku kadhaa baada ya hapo ili mwanamume aweze kuboreshe
na kuhifadhi mbegu zake kwa ajili ya siku hizo, Usikimbie chooni au bafuni
baada tu ya kukutana kimwili na mwenzio.
Sita, Kulala kwa dakika kadhaa baada
ya tendo la ndoa huongeza uwezo wa mbegu ya kiume kuweza kuendelea kukutana na
yai la kike na hivyo kuongeza uwezekano wa kubeba mimba.
Saba, Jiepushe kunywa kahawa na
vinywaji vinginevyo vyenye caffeine. Waataalamu wanasema caffeine huweza
kukuongezea matatizo ya kushindwa kushika mimba.
Nane, Jiepushe na kutumia dawa za
aina yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinazonunulika maduka ya dawa bila
ulazima wa cheti cha daktari au Over-the-counter drugs inabidi zitumiwe baada
ya kushauriana na daktari.
Tisa, Usitumie baadhi ya vitu
vinavyoufanya uke uwe na hali itakayoua mbegu za kiume au kupunguza majimaji
yake. Vitu hivi ni kama spray mbalimbali na tampons zinazotumiwa na wanawake
ili kuufanya uke uwe na harufu nzuri. Mafuta ya aina mbalimbali na jeli kwa
ajili ya kulainisha sehemu za siri, mafuta ya kula (vegetable oils) glycerin na
mate. Vitu kama hivi kufanya Ph ya uke isiwe ya kawaida na huweza kuua mbegu ya
kiume, kusababisha baadhi ya magonjwa ya wanawake au kupunguza majimaji ya
ukeni ambayo yanatakiwa ili kusafirisha mbegu za kiume.
Kumi, Hakisha mwenzi wako hafanyi
kazi au hawi katika mazingira yenye mada hatari ambazo hupunguza uwezo wa mbegu
za kiume au kutungwa mimba.
0 comments:
Post a Comment