Thursday 1 May 2014

KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


Wanaume wengi hapa duniani
huamini kuwa, mwanaume hasa ni
yule anayeweza kufanya tendo
hilo kwa muda mrefu na mara
nyingi ndio maana vijana wengi
utawasikia wakijisifu kuwa,
mpenzi wake hakulala usiku
mzima kutokana na dozi ya maana
aliyompa na ukimuuliza mtu wa
namna hii atakwambia kuwa
alikwenda mizunguko sita usiku
mzima.

Hata hivyo, ukweli ni kuwa, watu
wengi hufikia hatua ya kusema
uongo ili waonekana kuwa ni
wanaume hasa mbele ya wenzao
huku wangine wakigubikwa na
nadharia kuwa ukubwa wa uume
unaashiria jinsi gani walivyo
wanaume kitu ambacho si kweli.
Ni mtazamo huu ndio
unaowafanya wanaume
wakitaniwa au kuambiwa kuwa
wako kama wanawake wanaweza
waue mtu. Tunaamini kuwa
uanamke ni udhaifu na uanaume
ni ushujaa fulani hivi.
Wakati hali ikiwa hivyo, hivi sasa
wanaume wengi wamekuwa
wakihangaika na jambo moja
kubwa, kutafuta dawa za
kuongeza nguvu za kiume ili
kujiongezea heshima faragha!
Ukitaka kuthibitisha hili jaribu
kuangalia karibu katika kila gazeti
utakalo soma, ni nadra sana
kukosa tangazo dogo la biashara
lililotolewa na mganga wa kienyeji
anayejigamba kuwa anazo dawa
za kuongeza nguvu za kiume, na
matangazo hayo hayaishii
magazetini tu, bali hata redioni pia
yapo.

Mbaya zaidi dawa zinazoongelewa
hupewa majina mengi ya
`kusisimua` kama kombora, simba
na nyati siushasikia mziki wa nyati
akikasirika sasa jenga picha nuvu
ya hiyo dawa, hata hivyo, dawa
nyingi ni uzushi tu na hupewa
majina hayo ili kuwavuta wateja
na kuwashawishi kuzijaribu,
enewei ndivyo biashara zilivyo.
Wingi huu wa matangazo
umeanza kuonekana katika miaka
ya hivi karibuni, na kadiri siku
zinavyozidi ndivyo idadi ya
waganga wanaojigamba kuwa na
dawa hizo inavyozidi kushamiri,
kuna waganga wenye dawa za
Kiswahili, Kiarabu na za Kichina
ndio usiseme!
Binafsi utitili wa matangazo haya
umenifanya niamini kuwa, kuna
tatizo kubwa la wanaume
kupungukiwa nguvu hizo, na
ingawa hakuna utafiti wa
kitaalamu uliofanywa rasmi, lakini
inaonyesha kuwa tatizo hilo kwa
sasa ni kubwa sana na si Tanzania
tu, bali ni dunia nzima.

Kutokana na hali hiyo ndipo
waganga wa kienyeji pamoja na
makampuni mengi makubwa
duniani hujaribu kuelekeza nguvu
zao katika kufanya utafiti wa
kutengeneza dawa za kusaidia
watu wenye tatizo hilo, na bahati
nzuri kwa makampuni na
waganga hao ni kwamba
inaonekana kama biashara
inawaendea vizuri.
Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi
moja ya biashara ya dawa za aina
hiyo nchini Uingereza, imebainika
kuwa asilimia 46 ya wanaume
nchini humo hutumia dawa hizo,
hata hivyo wengi wao huzitumia
bila ya kupata ushauri wa daktari
na maduka mengi ya dawa
yametozwa faini kwa kuwauzia
dawa hizo bila ya kuwa na vyeti
vya daktari.
Kupungua kwa nguvu miongoni
mwa wanaume wengi
kumesababisha wengi wao waishi
katika maisha na hali ya
usononekaji na wengine
wamekumbwa na umauti
kutokana na hali hiyo ya kuishi na
sononi kwa muda mrefu.
Kuna mambo mengi
yanayosababisha wanaume wengi
wajikute wakipungukiwa nguvu za
kiume, wataalamu wa masuala ya
saikolojia wanaamini kuwa mara
nyingi suala hilo, hasa kwa watu
wenye umri wa chini ya miaka 45,
husababishwa na msongo wa akili
kuliko ufanyaji kazi wa misuli ya
mwili.
``Watu wengi wanaofikiri kuwa
wamepungukiwa na nguvu hizo
huwa hawako hivyo,`` inasema
sehemu moja ya utafiti uliofanywa
na wataalamu wa Chuo Kikuu cha
Havard, nchini Marekani na
kufafanua kuwa:
``Tatizo la watu hao huwa ni
kushiriki tendo hilo kwa wakati
usio muafaka kwao, wanashiriki
wakati bado hawajajitayarisha
kiakili au wanapokuwa
wamejitayarisha, basi `njiani`
hukutana na wenzi ambao
hawaafiki mwelekeo wa `safari`
yao``.
Wataalamu wa masuala ya
vyakula nao wanaeleza kuwa
tatizo hilo huwapata wanaume
wengi kwa sababu ya utumiaji wa
vyakula vyenye kuongeza kiwango
kikubwa cha mafuta mwilini
ambao hawashiriki katika mazoezi
ya viungo ambayo huifanya misuli
ya damu mwilini kutokufanya kazi
vizuri na hivyo kusababisha
matatizo mengi ya mwili
kushindwa kufanya kazi zake
vizuri.
Kumbukumbu yangu inaonesha
kuwa, Mheshimiwa Mbunge wa Viti
maalumu kuputua tiketi ya Chama
Cha Mapinduzi, Janet Bina Kahama,
10 Aprili 2007 katika kikao cha
saba cha bunge aliulizwa swali
ambalo lilikuwa namba 8 lenye
kipengele a, b, na c ambapo
kwenye kipengele b aliuliza: Je,
serikali inafahamu ni sababu gani
zinasababisha kupungua kwa
nguvu za kiume kunakotangazwa
sana na waganga wa jadi?
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, wakatik huo
Prof. David Homeli Mwakyusa
alijibu kuwa, Upungufu wa nguvu
za kiume unasababishwa na
mambo mengi, baadhi yao ni lishe
duni hasa mboga za majani,
kutokula aina mbalimbali za jamii
ya karanga (nuts), matumizi
yasiyofaa ya ulevi kama pombe,
sigara na dawa za kulevya, dawa
zinazotibu baadhi ya magonjwa
kama kisukari, shinikizo la damu,
magonjwa ya akili na vilevile
kutopumzika kunakosababishwa
na shughuli nyingi za kijamii hivyo
kusababisha uchovu.
Lakini ni kweli dawa hizi za asili
zinauwezo wa kutatua tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume?
Pro. Mwakyusa anathibitisha kwa
kusema kuwa, dawa nyingi za tiba
asili ni virutubisho ambavyo
muhitaji angeweza kuvipata
endapo angekula vyakula vyenye
virutubisho hivyo.
Pamoja na kuwa dawa hizo
hazijafanyiwa utafiti wa sayansi ya
leo na kutokana na unyeti wa usiri
wa watumiaji wa dawa hizo
zingekuwa na madhara
zisingetumiwa na wananchi hata
huko zinakotoka yaani maeneo
yake ya asili.
Na kusisitiza kuwa, Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii haijapokea
taarifa ya tukio kutoka kwa
walalamikaji wanaotumia dawa
hizo za kuongeza nguvu za kiume.
Hata hivyo, hali ni tofauti kidogo
katika nchi zilizoendelea kama
Marekani na baadhi ya nchi za
Ulaya, matumizi ya dawa hizi
hutolewa kwa watu baada ya
kuandikiwa cheti na daktari, na
watu wenye matatizo ya
msukumo wa ndamu (BP), mara
nyingi wamekuwa wakishauriwa
kutotumia dawa hizo kwa sababu
ni hatari kwa maisha yao.

Hii ni kwa sababu dawa nyingi,
kama Viagra, Ciallis, Levitra,
Yohimbine na nyingine mbali ya
kuwa na nafasi ya kusababisha
magonjwa ya moyo, kwa watu
wasiokuwa nayo, pia yana
madhara mengine kama vile
kusababisha upofu na kuleta hali
ya mwili kuwa na kitetemeshi.
Madhara mengine ya dawa hizo ni
pamoja na kumsababishia
mtumiaji hali ya kuumwa na
kichwa mara kwa mara, macho
kuwa mekundu, kuziba kwa hewa
puani na maumivu ya tumbo
pamoja na kuharisha.

Haya ni aina ya madhara
yanayotokana na dawa za kizungu,
ambazo kabla ya kuingia
madukani kufanyiwa utafiti wa
kina kuangalia madhara yake kwa
watumiaji, na ingawa hayo yote
yanafanyika lakini bado athari
zake kwa watumiaji zinaonekana.
Mwandishi na muandaaji
mkongwe wa filamu nchini
ambaye kwa sasa anaishi
Marekani, Chemi Che-Mponda
alishawahi kuandika makala
isemayo ‘kukosa nguvu za kiume si
mwisho wa dunia!’ na katika
makala hiyo kulikuwa na hadithi
hii isome ili ujue kinachoweza
kukutokea kwa kujifanya mjuaji na
kuagiza dawa za kuoneza nguvu
kwenye mtandao.
Chemi alianza hivi: “Jamani,
jamani, jamani, kuna jirani yangu
kafa hivi majuzi. Alikuwa ni baba
wa makamu, mmarekani mweusi.
Alikuwa mcheshi na ilikuwa kila
tukionana lazima tusalimiane.
“Mara ananinunulia kahawa halafu
tunakaa namsimulia kuhusu Afrika.
Yule baba, alionekana mzima na
mwenye afya fiti kabisa. Nilibakia
kushangaa kusikia kafa na si kwa
ajali. Mke wake alifariki mwaka
juzi, lakini miezi ya karibuni
alikuwa anaonekana mwenye
furaha kwa vile alipata mpenzi,
dada mwenye miaka 25 hivi.

”Story niliyosikia ni hivi: Kumbe
jamaa alikuwa na matatizo ya
moyo. Alifia kitandani akiwa
kwenye shughuli ya kufanya tendo
la ndoa na mpenzi wake. Tena
wanasema alifariki mara alipofikia
kilele cha tendo.“Navyosikia
ilikuwa ni ‘massive heart attack’.
Kama ni massive bila shaka na
utamu wa shughuli hakujua kuwa
yuko hatarini. Mpenzi wake alipiga
sana kelele, majirani walipigiga
simu 911 (polisi) kwa vile
walidhania wameingiliwa na
majambazi.
“Kumbe jamaa alikuwa mtumizi
wa Viagra, yaani vile vidonge vya
kuongeza uume, na kumpa
mwanaume uweza wa kufanya
tendo la ndoa. Ndugu zake
wanalamika kweli, maana
hakuzipata kwa prescription
(maelezo) ya daktari, alizaiagiza
kwenye mtandao (internet).
Hiyo ni baadhi ya mifano hai
inayoonesha wazi madhara
unayoweza kupata kwa kuamua
kutumia tu dawa bila maelekezo
kutoka kwa daktari!
Binafsi nina hofu juu ya dawa ‘za
kienyeji’ zinazotengenezwa na
waganga na kuuzwa kama
karanga kila kona ya miji
mbalimbali ya Tanzania bila ya
kufanyiwa utafiti wa kina, ni wazi
kama kanuni za kiafya
zinavyosema, kuwa kila dawa ina
madhara yake, lakini je, ni nani
anapima madhara mabaya
yatokanayo na dawa hizi za
kienyeji zinazouzwa kama njugu?
Ukiacha madhara yatokanayo na
dawa hizo, pia wanaume wengi
hukumbwa na tatizo hili la
kupungukiwa nguvu kwa sababu
ya uvutaji wa sigara kwa wingi,
utafiti mbalimbali wa kitabibu
duniani unaonyesha kuwa
matumizi ya bidhaa zitokanazo na
tumbaku huwasababishia
wanaume upungufu wa nguvu
hizo.
Ni kweli ulio wazi kwamba tatizo
la wanaume wengi kupungukiwa
nguvu za kiume nchini kwetu na
duniani kote linazidi kushika kasi
na tiba mbadara zinahitajika ili
kurudisha heshima na furaha
miongoni mwa wanaume wengi
duniani, lakini utumiaji wa dawa
za kuongeza nguvu haupaswi
kufanyika kiholela kwa kuzingatia
kuwa matatizo yake kiafya ni
makubwa kuliko faraja ya muda
mfupi anayopata mtumiaji!
Siku moja nilikuwa nimekaa
kwenye kijiwe cha kahawa
Kariakoo jijini Dar es Salaam
nikachokonoa wazee kwa
kuchomekea mada hii, mambo
mengi walinieleza lakini kubwa
zaidi ni kuwa, vijana wa siku hizi
wanakubwa zaidi na tatizo hili
kutokana na kufakamia vyakula
visivyo vya asili na kusahau kuwa,
miogo, asali, karanga na pweza
huweza kukusaidia ukawa na
nguvu kama nyati. Vyakula vingi
vinavyoingizwa nchini vikiwa
vimesindikwa ambavyo vijana
wengi hukimbilia na kujiona kuwa,
babu kubwa wakivila hivyo na
kumcheka mzalendo anayepata
muogo wa kuchoma na chachandu
huku akishushia na juisi ya mua
pale Kariakoo bila kujua kuwa
sehemu kubwa ya aina nyingi ya
vyakula wanavyokula ni sumu
yenye ladha nzuri
inayonenepesha!
Madhara yake ni
mengi na miongoni mwake ni
kuwasababishia watumiaji kukosa
nguvu za kurudia tendo.
Hata hivyo, kuna wakati pia
upendo unapopungua na mvuto
unapungua baina ya wanandoa,
mwanaume anaweza kujikuta kila
akiwa faragha anashindwa
kuendesha gari kwa muda mrefu
na anaweza kudhani kuwa ana
matatizo kumbe hali hiyo
inamkumbwa kutokana na
kutokuvutiwa na mwenzi wake.
Tatizo kama hili linaweza
kutatuliwa kwa kumueleza wazi
mkeo ama mpenzi wako jinsi gani
anaweza kujipanga na kuonekana
na mvuto wa hatari utakaokufanya
uchanganyikiwe kila umuonapo na
hata mkiingia kwenye mambo
fulani basi kwa hakika
utahamasika na kutoa dozi ya
maana.
Uchovu wa kazi za ajira
Mkufunzi wangu wa saikolojia
katika Chuo Kikuu cha Tumaini
Iringa ambaye ameshatanulia
mbele za haki, Pro. Samuel Mshana
(Mungu amlaze mahali pema
peponi) aliwahi niambia kuwa
wanawake wanataka security
kutoka kwa mwanaume nami
nikamtania Pro. Sasa mbona mimi
na mwili mdogo nitampa ulinzi
gani mwanamke akacheka kisha
akaniambia ulinzi naouzungumzia
ni wa jumla ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha mambo yanakwenda
sana ndani ya nyumba yani watoto
wanakwenda shule na mambo ya
mlo wa uhakika.
Hivyo ni wazi kuwa wanaume
huhangaika kwa kiasi kikubwa
kuhakikisha wanamudu majukumu
yao ya kila siku na huko makazini
kuna mauzauza mengi na usiombe
ufanye kazi kwenye kampuni
binafsi kila kukicha wewe upo
roho juu sasa katika hali kama hiyo
ukikutana na mwenzi wako
kunako majambozi utahisi una
upungufu wa nguvu za kiume
kwani mara tu baada ya kumaliza
mshindo wa kwanza hutoweza
kurudia tena! Hali ni hivyo hivyo
kwa watu wanaofanya kazi nzito
zinazosababisha wajikute
wanarudi majumbani wakiwa
wamechoka.
Hivyo basi, endapo nawe ni
miongoni mwa watu
wanaokumbana na tatizo la
kushindwa kurudia majambozi
kwa sababu ya uchovu na msongo
wa mawazo kutoka kazini
hakikisha unapanga muda
muafaka na mwenzi wako
kupeana raha.
Mfano kama Jumamosi unafanya
kazi nusu siku ukitoka usiende
kulewa kama ni mtu wa kinywaji
bali nenda kapumzike kisha kesho
yake waweza kumtoa out mama
na kwenda mazingira tofauti
kupeana kitu roho inapenda
hakika utajishangaa jinsi
utakavyomudu majambozi.
Kuchacha
Nakumbuka vema miaka ya 1990
enzi hizo Redio Tanzania pekee
ndio ilikuwa ikitupa burudani na
moja kati ya nyimbo ambazo
ilikuwa ikinikuna ni ‘kuchacha
usiombee’ iliyoimbwa na Juwata
Jazz na hichi ni kibwagizo chake
‘Maradhi yote ugua lakini kuchacha
usiombe…’ ebwana usije ukawa
katika hali mbaya kifedha na kila
jambo unalolipanga linakwenda
ndivyo sivyo hali
inayokusababishia uchache kisha
mwenzi wako akakuomba
unyumba hapa kuna mawili ama
kuchelewa sana kufika safari yenu
ama kumaliza halaka kisha jamaa
analala chapchap na hataki tena
kuonesha ushirikioano hata
mamaa akimbembeleza vipi!

Hivyo basi, si vema kukutana
kimwili na mwenza wako kipindi
ukiwa umechacha kwani wanaume
wengi pindi wanapokuwa na
msongo wa mawazo hukimbilia
kuomba unyumba kwa wenzi wao
wakiamini kuwa, wao ndio
watawasaidia kuwapunguzia
mawazo badala ya kutafuta njia
mbadara ya kumaliza tatizo.

Kuishiwa hamu ya nyama na
mapishi yale yale kila siku
Uzoefu wangu unanionesha kuwa
wanaume wengi hujikuta
wakikosa hamu ya kurudia tendo
la ndoa mara bada ya kumnaliza
mzunguko wa kwanza kutokana
na wake zao kutowaonesha
ubunifu yaani kila siku ni kifo cha
mende tu hakuna jipya
linaloongezwa hata nakshi za
miguno ni ile ile hali
inayosababisha wanaume wakose
hamy ya kuendelea mara baada ya
kumaliza mzunguko wa kwanza.
Wanaume wengi hujikuta
wanalazimika kutafuta kimada ili
kupata radha mpya na huko
mambo huwa mulua kwani
hufanikiwa kwenda raundi hadi
tatu na bado akawa na hamu kwa
vile tu amekutana na vitu adimu
hivyo basi, mwanaume anapaswa
kumueleza wazi mkewe kuwa
anahitaji wakutane faragha
ambapo anataka vutu hadimu vya
kabatini na si kumsaliti mwenza
wako kwani uwezo wa kumfanya
awe bora kunako majambozi unao
wewe mnwenyewe mwanamme.
Mfano siku akikwambia
anakwenda kwenye kitchen party
mruhusu kisha akiwa huko
mtumie meseji kuwa, “mpenzi
najiandaa kumalizia sehemu ya pili
ya soma ulilojifunza yaani la
vitendo, hakika leo nitafaidi”
asikdanganye mtu hapo hata kama
bi. Harusi mtarajiwa
hakufundishwa mambo fulani ya
kumpagawisha mumewe
atahakikisha hakuangushi atakuja
na mambo mapya na hapo ndipo
mwanaume hujikuta akiganda
kifuani.
Nimalize kwa kusema kuwa,
hakuna haja ya kukurupuka na
kukimbilia kununua dawa za
kuongeza nguvu ya kiume bila
kutafakari kwa kina chanzo cha
tatizo lako kwani yawezekana
tatizo ulilonalo linaweza kutatulika
kwa njia nyingine ambazo
hazitakufanya uwe hatarini.

0 comments:

Post a Comment